Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo!
Huyu jamaa bhana. Kiukweli wengi hata wasiompenda, au wanaomuona kama kikwazo. Na wale wanaompenda. Wote tunakubaliana jambo moja, huyu jamaa sio level zetu hasa kimsimamo.
Ni watu wachache sana Duniani wenye ujasiri na msimamo kama wa Tundu Lisu.
Fikiria mpaka Rais Samia aliomba Yule Simba wa Zanzibar aitwe Lisu. NI Kwa sababu Lisu ni jasiri kama Simba. Sio muoga. Anamsimamo mkali.
Kama lile tukio la kupigwa risasi lingefanikiwa 2017, na Lisu akauawa. Leo hii Lisu angekuwa ameshasahaulika na kama ni kukumbukwa ingekuwa mara mojamoja sana.
Embu fikiria watu waliokufa miaka tisa, saba, none, sita nne iliyopita. Ni kwamba wamesahaulika. Na ndivyo kifo kilivyo. Kuondoa duniani na kuhakikisha unasahaulika.
Lakini jamaa sasa hivi anaishi kwa kujenga Ulegendari. Na mpaka sasa yupo kwenye nafasi nzuri ya kuwa Legend.
Unajua kufa kila mtu atakufa. Hilo ni hakika.
Ila wachache sana hufa wakiwa na ujasidi uleule na kukataa kumuinamia au kujisaliti.
Wengi wanakufa wakiondoa misimamo yao waliyoiamini ni sahihi. Wengi hufa wakiwainamia mahasimu wao.
Kwa sababu mbalimbali.
Wapo wanaoinama kwa sababu ya mambo ya kiuchumi, hali ngumu ya maisha.
Wapo wanaoinama kwa sababu ya uhuru wao.
Wapo wanaoinama kwaajili ya familia zao.
Wapo wanaoinama kwaajili ya uhai na usalama wao.
Wapo wanaoinama kwaajili ya maumivu, na kuona hakuna faraja na matumaini.
Wapo wanaoinamia adui zao kwa sababu ya vyeo na maslahi ya kiuchumi na kisiasa.
Lakini ni wachache sana. Sana. Ambao wapo tayari kufa na Tai shingoni.
Watu aina ya Sadam Hussein, Muhammar Ghadafi, Ayatolla Khomeini na wengineo ni wachache sana.
Sasa Lisu amefuata njia hiyo. Hiyo ni njia ngumu sana. Na kila mtu anajua hilo.
Sisi kama watazamaji, mashuhuda, wasimulizi, tunaangalia haya mambo yatafika mpaka wapi.
Kikawaida adui unapokabiliana naye atakuweka katika nafasi moja kati ya hizi;
a) Adui wa Heshima.
b) Adui Mpumbavu(uchwara)
Lisu ni wale watu ambao ukiingia naye kwenye uadui basi utamuweka kwenye nafasi ya Adui wa heshima.
Adui wa Heshima ni yule ambaye unajua kabisa anachokipigania ni sahihi lakini wewe hukubaliani naye kwa sababu maslahi yako yanaguswa. Na jamaa anakuwa na msimamo hata kifo. Huyo ni Adui wa heshima.
Adui uchwara ni yule ambaye anajifanya ni ngangari anatetea haki. Lakini kumbe hayupo tayari kulipa gharama. Kumbe anamaslahi yake ambayo ukitaka kuyagusa anarudi nyuma na kubadili msimamo. Hiyo ni adui uchwara.
Kikawaida maadui uchwara hata ukiwadhuru haikuumi sana kama adui wa heshima. Kwa sababu adui uchwara utajijengea defensive mode kwamba alikuwa mnafiki, hakuwa anamaanisha. Naye ni kama wewe.
Watu wabaya wanavipimo vyao. Na ukifeli kwenye kipimo chochote wanakuondoa kwenye adui wa heshima.
Wahuni wanatabia za kutafuta dosari au ubaya Kwa wale wanaowadhuru. Ili kupata kisingizio na tulizo la moyo kwamba hawakukuonea.
Wema na ujasiri vinaenda sambamba.
Mtu ambaye sio jasiri hawezi kuwa mwema.
Ndio maana katika kanuni za kitibeli za haki na ukweli. Ujasiri ni moja yanayofundishwa.
Mtu asiye jasiri hawezi kuwa Mwema wala mwenye Haki.
Kwa sababu akitishwa kidogo atafanya yaleyale wanayoyafanya watu waovu.
Ili mtu awe muovu sharti awe muoga.
Ayaogope maisha.
Aiogope kesho na future,
Aogope Watu,
Woga ni msingi mkuu wa uovu. Kwa sababu ukishakuwa mwoga utakosa Imani, haki na ukweli. Na ukikosa hayo utakosa upendo. Na ukikosa upendo basi mambo hayatabiriki tena.
Lisu ni adui wa heshima. Lakini tusimalize mate ulimini, au wino kalamuni. Subiri tuone mwisho wake.
Nilikuwa nataka kusema, mtu muovu na yule muoga wa kushindwa kuusema uovu wote ni kundi moja. Tofauti yao ni muda na nafasi tuu.
Mimi nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam