Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nashangaa kwanini watu wanaumiza kichwa juu ya ahadi za Raisi Magufuli wakati wa ziara zake za kampeni kuwa ni rushwa au la.
Labda kwanza nikubaliane na Rais Magufuli kwamba ni kweli yeye bado ndio wa raisi wa Tanzania, na ana haki ya kutoa hizo ahadi kama raisi - ingawa ni jambo la kushangaza kwamba baadhi ya hizo ahadi ni miradi mikubwa ya kitaifa ambayo lazima bajeti yake ipitishwe na Bunge, lakini tumeona jinsi Magufuli kwa makusudi ya kukiuka katiba kaamua kujiba mamlaka ya mihimili miwili ya taifa - Raisi na Bunge.
Sasa kwa Lissu, hili suala wala halipaswi kumuumiza kichwa. Anachoweza kufanya ni kupita kila sehemu ambazo Raisi Magufuli ametoa hizi ahadi kama raisi, na kuwaambia wananchi wa sehemu hizo kwamba msiwe na wasiwasi, kama Raisi wa sasa ameahidi hili, hata mimi mkinichagua kuwa raisi basi nitawatekelezea hiyo ahadi aliyotoa raisi wa sasa, kwa sababu ndio utaratibu wa kukabidhiana ofisi ya uraisi!
Awaambie hata mikataba ambayo Rais amefanya kwa niaba ya Tanzania, hata kama yeye Lissu haipendi itabidi aitekeleeze tu kwa kuwa sheria zinambana. Sembuse iwe mambo mazuri aliyowaahidi raisi kama barabara!
Hivyo Magufuli ataendelea kutoa ahadi wakati wa kampeni, na Lissu ataendelea kuahidi kutekeleza ahadi zake mwenyewe za zile za Magufuli, na wananchi tutafaidika!
Kama umesikia kumkaanga samaki kwa mafuta yake mwenyewe ndio hivyo tena! Ningekuwa Lissu ningetembea na ki-notebook cha ahadi za raisi Magufuli ili kwenda kuwahahkikishia wananchi kwamba zitatekelezwa kwa ufanisi zaidi na mimi mkinichangua kuwa Raisi. Tena kama Mgufuli kaahidi km 70 mie nitawaongezea km 10 za bonasi!