Kama akishinda tena, Rais Magufuli atategemea wateule wake 10 kuunda Baraza la Mawaziri la kueleweka

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
CCM imeishiwa katika kupika viongozi wajao ndani ya UVCCM. Kwa watia-nia wanaoendelea kujitokeza majimboni kila uchao, ni wazi kama ngazi kuwa CCM inakuwa na wagombea 'bomu' uchaguzini.

Kwakuwa ushindi umeshapangwa na kupangika, Bunge lijalo litakuwa dhaifu lakini nadhifu kama mkufu. Litakuwa na Wabunge wasiojua lolote, vyovyote na popote. Watakuwa wapokea mishahara tu.

Katika hali hiyo, kama akiibuka tena mshindi hapo Oktoba, Rais Magufuli atategemea tena nafasi zake 10 za kuteua Wabunge na kuwapa Uwaziri/Unaibu Waziri kutoka nje ya Majimbo ili kuwa na Baraza la Mawaziri la kueleweka. Rais Magufuli atalazimika kuwa na akina Kabudi na Mpango wengine. Majimbo yatazalisha Wabunge mbumbumbu wa hoja na wasio na tija. UVCCM imebaki kuwa kichaka cha kusaka vyeo badala ya kutumika kama kiwanda cha kuzalisha viongozi cha CCM.

Watia-nia ndani ya CCM wanasikitisha sana na kutishia mustakabali wa Taifa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Nyasa, Ruvuma)
 
Huo ushindi mnaoamini umeshapangwa na kupangika majibu yake mtayapata hiyo October, wapiga kura wana hamu na nyie kama mtoto anavyoitamani peremende, nawaambia mtamumunywa hamtaamini.

Hao wakurugenzi wa kutangaza matokeo hawataamini hali watakayokutana nayo hiyo siku ikifika, wasipoangalia wengi watadondoka kwa pressure.
 
CCM imeishiwa katika kupika viongozi wajao ndani ya UVCCM. Kwa watia-nia wanaoendelea kujitokeza majimboni kila uchao, ni wazi kama ngazi kuwa CCM inakuwa na wagombea 'bomu' uchaguzini.

Kwakuwa ushindi umeshapangwa na kupangika, Bunge lijalo litakuwa dhaifu lakini nadhifu kama mkufu. Litakuwa na Wabunge wasiojua lolote, vyovyote na popote. Watakuwa wapokea mishahara tu.

Katika hali hiyo, kama akiibuka tena mshindi hapo Oktoba, Rais Magufuli atategemea tena nafasi zake 10 za kuteua Wabunge na kuwapa Uwaziri/Unaibu Waziri kutoka nje ya Majimbo ili kuwa na Baraza la Mawaziri la kueleweka. Rais Magufuli atalazimika kuwa na akina Kabudi na Mpango wengine. Majimbo yatazalisha Wabunge mbumbumbu wa hoja na wasio na tija. UVCCM imebaki kuwa kichaka cha kusaka vyeo badala ya kutumika kama kiwanda cha kuzalisha viongozi cha CCM.

Watia-nia ndani ya CCM wanasikitisha sana na kutishia mustakabali wa Taifa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Nyasa, Ruvuma)

Kwani ameshapita na ameshaapishwa kuwa Rais kwa Muhula wa Pili? Sikatai kuwa itakuwa hivyo ila tusisahau kuwa Mola nae ana Mipango yake.
 
CCM imeishiwa katika kupika viongozi wajao ndani ya UVCCM. Kwa watia-nia wanaoendelea kujitokeza majimboni kila uchao, ni wazi kama ngazi kuwa CCM inakuwa na wagombea 'bomu' uchaguzini.

Kwakuwa ushindi umeshapangwa na kupangika, Bunge lijalo litakuwa dhaifu lakini nadhifu kama mkufu. Litakuwa na Wabunge wasiojua lolote, vyovyote na popote. Watakuwa wapokea mishahara tu.

Katika hali hiyo, kama akiibuka tena mshindi hapo Oktoba, Rais Magufuli atategemea tena nafasi zake 10 za kuteua Wabunge na kuwapa Uwaziri/Unaibu Waziri kutoka nje ya Majimbo ili kuwa na Baraza la Mawaziri la kueleweka. Rais Magufuli atalazimika kuwa na akina Kabudi na Mpango wengine. Majimbo yatazalisha Wabunge mbumbumbu wa hoja na wasio na tija. UVCCM imebaki kuwa kichaka cha kusaka vyeo badala ya kutumika kama kiwanda cha kuzalisha viongozi cha CCM.

Watia-nia ndani ya CCM wanasikitisha sana na kutishia mustakabali wa Taifa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Nyasa, Ruvuma)
Vijitu kama steven nyerere navyo vinataka ubunge vkafanye ukuadi Bungeni badala ya kuwatumikia wapiga kura
 
Dkt Bashiru ana kazi kubwa sana ya kujenga viongozi kutoka uvccm From scratch na CCM wasipofanya hivi naamini miaka kumi ijayo watapata tabu sana
 
Hawatakaa wayajue matokeo ya Mungu
Na sasa Cyprian Musiba anahaha kubuni mbinu mpya za kumhujumu Tundu lisu mara atake apelekwe jela wamumpandikizie mgonjwa wa corona amuambukize, mara atake shambulio jipya, cyprian Musiba hana Aman akisikia Tundu lisu anarejea tena kwani atamtaja ni miongoni mwa watu waliokwenda Dodoma kumshambulia
 
China ambao hufadhili pesa zote za uchaguzi na uchakachuaji hawajatoa cent wana mgomo kisa CCM kuwahujumu kwenye Bandari ya Bagamoyo
Kwahiyo unafikiri kwa sababu hiyo uchaguzi hautafanyika?. Ndugu jiandae tu kwa kipigo hapo oktoba!
 
Hata hivyo anaweza kulibadilisha kuanzia sasa maana yeye ndio atakayeteua wagombea.

Ila kwa kuwa yeye atakuwa muhimili uliojichimbia chini tena, hana budi kuwateua hawa mambumbu wa UVCCM.
Ila nahofia kitu kimoja, hawa jamaa kwa tamaa ya madaraka, wanaweza kubadilisha katiba na kumuongea mtukufu muda wa kubaki madarakani. Wale akina Nkamia, Ndugai na Kibajaj wanaoshadidia kuongezewa muda huenda wana watu nyuma yao. TAKE NOTE of this, kuna wakati tutarejea andiko hili.
 
Back
Top Bottom