Kama akishinda tena, Rais Magufuli atategemea wateule wake 10 kuunda Baraza la Mawaziri la kueleweka

Kama akishinda tena, Rais Magufuli atategemea wateule wake 10 kuunda Baraza la Mawaziri la kueleweka

CCM imeishiwa katika kupika viongozi wajao ndani ya UVCCM. Kwa watia-nia wanaoendelea kujitokeza majimboni kila uchao, ni wazi kama ngazi kuwa CCM inakuwa na wagombea 'bomu' uchaguzini.

Kwakuwa ushindi umeshapangwa na kupangika, Bunge lijalo litakuwa dhaifu lakini nadhifu kama mkufu. Litakuwa na Wabunge wasiojua lolote, vyovyote na popote. Watakuwa wapokea mishahara tu.

Katika hali hiyo, kama akiibuka tena mshindi hapo Oktoba, Rais Magufuli atategemea tena nafasi zake 10 za kuteua Wabunge na kuwapa Uwaziri/Unaibu Waziri kutoka nje ya Majimbo ili kuwa na Baraza la Mawaziri la kueleweka. Rais Magufuli atalazimika kuwa na akina Kabudi na Mpango wengine. Majimbo yatazalisha Wabunge mbumbumbu wa hoja na wasio na tija. UVCCM imebaki kuwa kichaka cha kusaka vyeo badala ya kutumika kama kiwanda cha kuzalisha viongozi cha CCM.

Watia-nia ndani ya CCM wanasikitisha sana na kutishia mustakabali wa Taifa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Nyasa, Ruvuma)
Enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Vijana walianza kuandaliwa tokea chipukizi,Jeshi la JKT ,na baadae Chuo cha Kivukoni au Omulutungulu Ukerewe.
Baada ya hapo walipelekwa kufanya kazi za kujitolea kwenye ofisi za chama,huku wakihamasisha vijana siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Baadhi waliajiriwa kama makamisaa katika sehemu mbali mbali wakiwa macho ya chama sehemu ya kazi.
Lakini kwa sasa wahuni ndio wametwaa bango la vijana kama wasaka madaraka.
Hakuna maandalizi ni ubabaishaji mtupu.CCM inajizika yenyewe.Ndio sababu siku hizi kuna teuzi za hovyo.
 
Kwani ameshapita na ameshaapishwa kuwa Rais kwa Muhula wa Pili? Sikatai kuwa itakuwa hivyo ila tusisahau kuwa Mola nae ana Mipango yake.
Naunga mkono hoja yako kwa 100%
 
Mungu huyuhuyu uliyemkejeli pale Magufuli aliposema tufunge na kuomba kwa ajili ya janga la corona?
Corona ipo watu wanafia majumbani Hosptal ndogo lakini huficha kuwa siyo corona, hakuna aliyemaliza corona Tanzania bado ina inaendelea kuua watu kimya kimya
 
Back
Top Bottom