VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
CCM imeishiwa katika kupika viongozi wajao ndani ya UVCCM. Kwa watia-nia wanaoendelea kujitokeza majimboni kila uchao, ni wazi kama ngazi kuwa CCM inakuwa na wagombea 'bomu' uchaguzini.
Kwakuwa ushindi umeshapangwa na kupangika, Bunge lijalo litakuwa dhaifu lakini nadhifu kama mkufu. Litakuwa na Wabunge wasiojua lolote, vyovyote na popote. Watakuwa wapokea mishahara tu.
Katika hali hiyo, kama akiibuka tena mshindi hapo Oktoba, Rais Magufuli atategemea tena nafasi zake 10 za kuteua Wabunge na kuwapa Uwaziri/Unaibu Waziri kutoka nje ya Majimbo ili kuwa na Baraza la Mawaziri la kueleweka. Rais Magufuli atalazimika kuwa na akina Kabudi na Mpango wengine. Majimbo yatazalisha Wabunge mbumbumbu wa hoja na wasio na tija. UVCCM imebaki kuwa kichaka cha kusaka vyeo badala ya kutumika kama kiwanda cha kuzalisha viongozi cha CCM.
Watia-nia ndani ya CCM wanasikitisha sana na kutishia mustakabali wa Taifa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Nyasa, Ruvuma)
Vijitu kama steven nyerere navyo vinataka ubunge vkafanye ukuadi Bungeni badala ya kuwatumikia wapiga kuraCCM imeishiwa katika kupika viongozi wajao ndani ya UVCCM. Kwa watia-nia wanaoendelea kujitokeza majimboni kila uchao, ni wazi kama ngazi kuwa CCM inakuwa na wagombea 'bomu' uchaguzini.
Kwakuwa ushindi umeshapangwa na kupangika, Bunge lijalo litakuwa dhaifu lakini nadhifu kama mkufu. Litakuwa na Wabunge wasiojua lolote, vyovyote na popote. Watakuwa wapokea mishahara tu.
Katika hali hiyo, kama akiibuka tena mshindi hapo Oktoba, Rais Magufuli atategemea tena nafasi zake 10 za kuteua Wabunge na kuwapa Uwaziri/Unaibu Waziri kutoka nje ya Majimbo ili kuwa na Baraza la Mawaziri la kueleweka. Rais Magufuli atalazimika kuwa na akina Kabudi na Mpango wengine. Majimbo yatazalisha Wabunge mbumbumbu wa hoja na wasio na tija. UVCCM imebaki kuwa kichaka cha kusaka vyeo badala ya kutumika kama kiwanda cha kuzalisha viongozi cha CCM.
Watia-nia ndani ya CCM wanasikitisha sana na kutishia mustakabali wa Taifa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Nyasa, Ruvuma)
Mnapanga ushindi lakini ya Mungu hamtaweza kuyapanga.
China ambao hufadhili pesa zote za uchaguzi na uchakachuaji hawajatoa cent wana mgomo kisa CCM kuwahujumu kwenye Bandari ya BagamoyoCCM itapata pigo kuuuuubwa sana pigo moja tu pigo takatifu pigo lililonyooka kabla ya uchaguzi mkuu ujao
Safari ijayo utasikia kibajaji na Msukuma ni mawaziri wa wizara nyetiHata Mimi nimemshangaa mno tu kwani kwa jinsi alivyosema na huku akipanga utadhani CCM na Magufuli wake Wao ni zaidi ya Malengo ya Mola.
Dkt Bashiru ana kazi kubwa sana ya kujenga viongozi kutoka uvccm From scratch na CCM wasipofanya hivi naamini miaka kumi ijayo watapata tabu sana
Na sasa Cyprian Musiba anahaha kubuni mbinu mpya za kumhujumu Tundu lisu mara atake apelekwe jela wamumpandikizie mgonjwa wa corona amuambukize, mara atake shambulio jipya, cyprian Musiba hana Aman akisikia Tundu lisu anarejea tena kwani atamtaja ni miongoni mwa watu waliokwenda Dodoma kumshambuliaHawatakaa wayajue matokeo ya Mungu
Mungu huyuhuyu uliyemkejeli pale Magufuli aliposema tufunge na kuomba kwa ajili ya janga la corona?Mnapanga ushindi lakini ya Mungu hamtaweza kuyapanga.
Kwahiyo unafikiri kwa sababu hiyo uchaguzi hautafanyika?. Ndugu jiandae tu kwa kipigo hapo oktoba!China ambao hufadhili pesa zote za uchaguzi na uchakachuaji hawajatoa cent wana mgomo kisa CCM kuwahujumu kwenye Bandari ya Bagamoyo
Ila nahofia kitu kimoja, hawa jamaa kwa tamaa ya madaraka, wanaweza kubadilisha katiba na kumuongea mtukufu muda wa kubaki madarakani. Wale akina Nkamia, Ndugai na Kibajaj wanaoshadidia kuongezewa muda huenda wana watu nyuma yao. TAKE NOTE of this, kuna wakati tutarejea andiko hili.Hata hivyo anaweza kulibadilisha kuanzia sasa maana yeye ndio atakayeteua wagombea.
Ila kwa kuwa yeye atakuwa muhimili uliojichimbia chini tena, hana budi kuwateua hawa mambumbu wa UVCCM.
CCM itapata pigo kuuuuubwa sana pigo moja tu pigo takatifu pigo lililonyooka kabla ya uchaguzi mkuu ujao
Na mimi hilo naliona Mkuu.CCM itapata pigo kuuuuubwa sana pigo moja tu pigo takatifu pigo lililonyooka kabla ya uchaguzi mkuu ujao
Amen!Mkuu DOUGLAS SALLU na iwe hivyo bila kupungua