Mi mwenyewe nashangaa kuna watu sijui huwa wanatoa wapi hizi mambo
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kuna light, kuna year. Ukiandika light year ni muunganiko wa maneno mawili, nayo ni light + year
Mwendokasi wa light ni 300,000 km/s. Umbali uliopo kati ya Mwezi na Dunia ni 384,500Km. Hii inamaanisha nini? Tukitizama hizo "Km" ya mwendokasi wa Light na umbali wa Dunia na Mwezi zote zipo laki tatu ila ya Dunia na Mwezi imezidi kwa kiasi chake. Hapa tunapata kuona Light kasi yake ni kubwa sana. Kwa mfano, mwanga wa Jua kufika Duniani unatumia dakika 8 na sek 19. Na umbali uliopo kati ya Jua na Dunia ni 149,597,871 Km, ukiikadiria inafika 150,000,000 Km. Ila kwa kasi ya mwanga "Light" inachukua dakika 8 na sek 19. Mpaka hapa tumeshaona kasi ya Light jinsi ilivyo.
Light year, nini?
Ni mwendokasi wa mwanga "light" unaosafiri kwenye ("space") ndani ya mwaka mmoja. Na 1 light year ni = na 9.5 trillion Km. Yaani;
1 light year(wastani wake) ni 9.5 trillion Km.
Unapotizama usiku angani na kuona Nyota zinang'aa basi ujue mwanga wake umesafiri kutoka mbali, na hii ni kwa sababu nyota zenyewe zipo mbali. Na mwanga wa hizo nyota kusafiri hazichukui siku moja, wala mwezi, zinachukua mpaka mwaka/ miaka. Inategemea na umbali wa nyota zenyewe. Hapa tunapata mantiki ya " Year" mwaka. Kwa vile mwanga unasafiri mwaka, miaka kwa mwendokasi wake ndiyo tunapata kitu kinachoitwa "Light year" Na mwaka unajumuisha siku, wiki,mwezi mpaka mwaka. Na ndani ya hayo tunapata Masaa. Yaaani;
Mwaka una siku= 365.25
Siku ina saa= 24
Saa ina dakika = 60
Dakika ina sek= 60
Huo ni mfano tu ili tuweze kufahamu light year ina maana gani.