Kama Alikupa Mimba, akakutelekezea mtoto. Unahaki ya kumnyima huyo Mtoto

Kama Alikupa Mimba, akakutelekezea mtoto. Unahaki ya kumnyima huyo Mtoto

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KAMA ALIKUPA MIMBA, AKAKUTELEKEZEA MTOTO. UNAHAKI YA KUMNYIMA HUYO MTOTO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Hivi ndivyo Watibeli tunavyofanya. Hasa mabinti zetu wakifanya zinaa na uchafu huko. Wakapata watoto wa zinaa(starehe).

2. Hatuwezi kuukataa Ukweli. Hata kama ukweli unatugusa Sisi wenyewe. Ukiwa mtoto wa zinaa isikuume. Bali jifunze kutoka katika makosa ya Wazazi wako. Wewe usilete watoto wa zinaa kama wewe ulivyo.

3. Wapo Watibeli wengi tuu ni watoto wa zinaa. Waliozaliwa katika Hali ya uchafu, Hali ya dhambi, lakini wao wakaamua kuwa waadilifu.

4. Kwenye Biblia moja ya watu hao ni Mfalme Daudi, ambaye katika historia ya Waisrael ndiye Mfalme pekee mwenye jina kubwa kuliko mfalme yeyote.
Daudi pia ni mtoto wa matokeo ya zinaa.
Na hii ilimpa mgogoro Sana na familia yake ikiwemo Baba na ndugu zake.

5. Najaribu kuelezea mtoto akishazaliwa amezaliwa. Bila kujali ni mtoto aliyezaliwa kiharamu au kwa njia halali kama ndoa na upendo.

6. Kiharamu ni Ile Hali mtoto anazapatikana kwa uongouongo, wazazi wake wanadanganyana, wanatapeliana. Huku mmojawao au wote wakiwa hawanalengo la kuwa Mume na mke.

7. Mtoto aliyepatikana kwa tamaa za mwili za wazazi wake. Yaani unakurupuka na nyege zako hapo, unaenda huko barabarani, unadandia mwanamke/mwanaume akutulize nyege zako. Unamaliza haja yako. Then wiki nbili baadaye unagundua unamimba haramu, mimba ya nyegezi, mimba ya tamaa.

8. Ni kweli mlikutana kwa nyege zenu. Ninyi sio wanandoa, sio mume na mke. Hamkuwahi kupatana mzae. So automatically inajulikana mnafanya starehe.
Mimba yatoka wapi yakhee?

9. Sasa ndio imeingia.
Mwanaume hakutaki. Na anahaki ya kukukataa kwa sababu alikuwa na tamaa tuu au nyege kama wewe ulivyokuwa nazo.
Usiseme alikudanganya. Hapana ninyi wote ni wahuni, asingetaka kudanganywa usingempa angefuata taratibu.

10. Kwa Sisi Watibeli, umeshamtia Mimba binti yetu mjinga, mkaidi, Malaya, asiyetii wazazi wake. Sasa kwa ukaidi wake yamemkuta.

11. Na umemkataa kwamba huwezi kumuoa na wala huitambui mimba yake.

12. Jambo la Kwanza Watibeli, Wanawake pia Wana power, ni viongozi. Nao wanauwezo wa kuendeleza ukoo wa baba zao.

13. Yaani Binti Yangu, Binti ya Robert Mtibeli anapozaa watoto anaouwezo wa kuwaita majina ya ukoo wa Mimi Babaake.

14. Na huyo mtoto akawa ni mtoto WA ukoo wetu Watibeli. Kwa sababu mtoto anachukua vinasaba vya Baba na Mamaake. Hiya ni kisayansi na natural

15. Kumaanisha kwamba mwanamke pia anaaweza kukuza ukoo na jina la Baba zake, alipotoka.

16. Hivyo kitu cha Kwanza, Sisi watibeli tunakata utambulisho wa nje ambao ni Jina.

17. DNA ambayo ni ndani itaonyesha ni Mtoto ni wamwanaume Fulani, lakini ni mpaka wampime. Na wewe ukitoka mfano Arusha kwenda Dar ukasema unaitwa Labda Peter Kimaro, hakuna atakayekupima DNA, watajua ni mchaga, ingawaje DNA ya Babaako ni Mayala ambaye ni msukuma.

18. Hatuwezi kukupa heshima ya jina la mtoto ambaye hukumlea au ulimkimbia.
Au ulimzaa kwa starehe yaani bila mapatano.

19. Binti atapitia madhara ya makosa yake ya kujifanyia umalaya na kuzaa kwa kukejeliwa, kuishi kwa lawama, kuishi na mumewe mpya(kama ataolewa) kwa migogoro inayosababishwa na mtoto wake wa Kwanza.

Lakini wewe je? Utalipiaje?
Kwamba uje tuu mtoto amekuwa mkubwa useme tuu mtoto wangu, namtaka.

20. Thubutu! Lazima Kila mtu alipie Kwa matendo Yake. Mama alidhalilika kwa miaka na miaka. Now it's your turn.

21. Kwanza jina sio lako. Pili lazima akukatae.

22. Kwa sababu wapo wanaume ni washenzi Sana. Haya ni kweli mlifanya zinaa wala hamkuwa na mpango wa kuzaa. Ukamkimbia. Wakati huo unajigamba kijiweni ninawatoto kibao.
Kulea hutaki,
Utasema mwanamke anakupelekesha anakupelekeshaje mtoto wa kike?

Nenda Polisi dawati la jinsia, waambie nataka kulea na kumhudumia mwanangu kwa namna hii na hii. Hakuna atakayekuzuia.
Na sio kutafuya visingizio vya kutohudumia mwanao.

23. Dada anatumikia kifungo chake cha kudhalilishwa huko mitaani, kuitwa majina ya Kila namna. Kupata mwanaume wa kumuoa kipengele. Kisa ujinga wake na wako.
Wewe unakula Raha na hulipii chochote.

24. Kwa Sisi Watibeli utalipia. Labda usije kumchukua mtoto. Lakini ukija lazima unyanyaswe.
Lazima usemwe,
Lazima ukejeliwe.
Lazima ukosewe heshima
Na mtoto bado hutompata.

25. Haki bin Haki.

26. Hakuna cha oooh! Nilikuwa sijui busy, sijui baba ni Baba, sijui wanawake wanalisha sumu watoto. Hakuna cha visingizio.

27. Wanawake, hasa wale wanaotaka kuwa kama Binti za tibeli. Ambao sasa hivi ni single mother, kwanza lazima mkubali ukweli kuwa mlicheza daily, hamkuwa wasikivu kwa wazazi na wakubwa wenu, mlifanya umalaya.
Hivyo mnayoyapitia mnastahili, lawama kejeli, manyanyaso ni haki yenu.
Ukifanya blunders lazima ulipie.

28. Pili, Msicheke na kima. Kila mtu avune alichopanda. Kama unalea mwenyewe mtoto. Badilisha majina. Pilli, usikubali mtoto aende kwa babaake mtoto aliyefikisha miaka zaidi ya 15.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Wakati umefika kwa watunga sheria na serikali kwa ujumla kulichukulia hili swala kwa uzito unaostahili. Deadbeat fathers wote wafuatiliwe na watoe huduma ya matumizi kwa watoto wao. Huku mtaani dada zetu wanalea watoto wao kwa tabu sana
 
Utibeli sio kizio ya Utimilifu, anza kuleta mada bila hizi hoja sasa mkuu.
 
Wote wawili wafanye umang'amang'a wao halafu baadaye mmoja ajipe haki zote?Ngoja tusikie milio mbalimbali.


Kama hutimizi wajibu na majukumu yako haki zako lazima zichukuliwe Mzee baba
Huwa yanawashinda na kurudisha mipira kwa kipa.

Kwa ambao hawana kazi

Alafu Siku hizi unajua hata wanaume kazi hawana.
Pia uwezo wa kufikiri ni kama unalingana

Siku wanawake mawazo ya utemegezi yakiisha kuna watu wataishi maisha magumu
 
Kama hutimizi wajibu na majukumu yako haki zako lazima zichukuliwe Mzee baba


Kwa ambao hawana kazi

Alafu Siku hizi unajua hata wanaume kazi hawana.
Pia uwezo wa kufikiri ni kama unalingana

Siku wanawake mawazo ya utemegezi yakiisha kuna watu wataishi maisha magumu
Mwanaume asiye na njuluku ndiye huwa anakosa nguvu za kiume na anakuwa hana fikra mbadala.
 
Back
Top Bottom