Ni ujinga kufikiria tuna utawala wa sheria wakati haupo.
Mbowe alikamatwa namna gani? Sheria ikifuatwa katika ukamataji?
Mbowe ifikishwa mahakama baada ya muda gani? Sheria ilifuatwa?
Tanzania kwani tuna mahakama au tuna kitengo cha Rais kinachofanya kazi ya mahakama? Kuna mahakama ambayo huwa inaambiwa cha kufanya na Rais? Magufuli aliwaambia funga akina Mdude, funga matajiri, piga faini akina Mbowe, ikawafunga na kuwapiga faini ya mamia ya mamilioni akina Mbowe na matajiri. Samia anakuja anaiambia, mnajua nchi yetu imechafuka, waachie akina Mdude, matajiri na akina Mbowe warudishiwe hela yao, na yenyewe inafanya. Hivi hiyo utaiita ni mahakama?