Ila kweli ubinadamu kazi, uyu mh. magufuri hata kama ana kauli mbaya, ila watu wa CHATO hawana shukrani kwa uyu jamaa.
Kiukweli hapa tanzania kwa sasa hakuna wilaya inayopaa kwa maendeleo kama chato, tuachane na mambo ya kisiasa, chato kwa sasa ni wilaya ya mfano katika Tanzania, kwanza ni wilaya yenye miaka 6, yaani imeanzishwa mwaka 2007 ila mpaka sasa ni wilaya inayotegemea kuwa na maji ya bomba kuja kufika mwezi wa tisa,
Ni wilaya ambayo barabara zake zote zinapitika kwa wakati wote katika mwaka, Ni wilaya yenye umeme ingawa ni wa jenereta, ni wilaya yenye barabara ya rami yenye urefu wa zaidi ya Km 100,
Ni wilaya yenye rami karibia mitaa yote ya chato mjini. Jamaa kajitahidi kufanya vitu hivi vyote lakini watu hata hawamkubali pamoja na mapungufu yake.
Jamaa kaleta miradi ya kutosha hapa wilayani iliyotoa ajira kwa vijana, ila kumbuka nabii hathaminiwi nyumbani hat siku moja.
Pia haya majungu yanatoka kwa vijana wa vijiweni hasa pale chato mjini ambao wanataka kila jamaa akija wampe umbea ili awape angalau vijisent, ila jamaa hana tabia ya kugawa ela, yeye anataka watu wafanye kazi kuliko kukaa kijiweni.
Kitu kingine ni kuwa hawa watu wa chato ni wavivu sana, kukaa sana vijiweni pamoja na majungu! Hawataki kufanya kazi wamekalia majungu tu!
Pia jamaa aliwaambia kuwa kamwe hawatakaa waajiriwe Halmashauri kwa kuwa kulikuwa na kiwanda cha pamba hapa chato ambacho kilikuwa na wazawa wa kutosha toka hapa chato ila badala ya kufanya kazi na kukiendeleza hiki kiwanda, wao walijikita katika kukifilisi, kuiba mafuta, vifaa mbali mbali vya kiwanda mpaka kikafa
Hapo sasa ndo hasira zilimjaa na kuwaambia " Kwa kuwa mmekifilisi na kukiua hiki kiwanda kamwe hamtaajiriwa katika halmashauri hii" hapo ndo kikawa chanzo cha kumchukia ingawa jamaa alikuwa anawaambia ukweli.
Nayasema haya kwa kuwa 2011 nilikuwa chato na nilikaa hapo miaka 3.