Kama atatawala juu ya damu je! Hataloa na kulowesha wengine?

Criss

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Posts
1,959
Reaction score
3,172
Wakati naitafakari J2 yangu tulivu chini ya kivuli cha mti niliyoupanda kwa mkono wangu mwenyewe nikawa nawaza kumbe matokeo ya kesho yetu yapo mikononi mwetu.

Moyoni nimejikuta najiuliza hivi Mama amejiandaa kweli kutawala kwenye hili dimbwi za Damu za hawa jamaa waliyopata uhuru pasipo kumwaga damu nayeye kuamua kuwamwaga kwa mtindo wa kivita ,atatoboa ?

Kunamtu utawasikia aah! Hakuna jipya hapo , unesahau ya 2000 yaliyowakuta Zanzibar? Watu waliuliwa kama kuku na hakuna kitu walifanya ,chezea dola wewe ,huwa nacheka tu ninapozisikia hizo tambo , moyoni huwa nawaambia ,nyie acheni kufananisha nchi na Kijiji .wale kweli ni ndugu zetu na kwa namna yoyote hatuwezi kuyafurahia mapito yao ila huku walikogusa ni kubaya zaidi .

Kelele ya chumba kimoja ni tofauti na kelele ya nyumba nzima.

Nijuavyo ,ili kiongozi ayatimize majukumu yake atahitaji watu ,Najiuliza kwa namna hali ilivyo kunadiwani anaweza kupata ujasiri wa kusimama katikati ya kundi ambalo jamii nzima inakilio na serikali anayoiongoza?

Najiuliza kwa namna hali ilivyo kuna mbunge atakaeweza kupata ujasiri wa kusimama katikati ya kundi ambalo jamii nzima inakilio na serikali anayoiongoza?

Najiuliza kwa namna hali ilivyo kunadiwani anaweza kupata ujasiri wa kusimama katikati ya kundi ambalo jamii nzima inakilio na serikali anayoiongoza?

Najiuliza kwa namna hali ilivyo Rais anaweza kupata ujasiri wa kusimama katikati ya kundi ambalo jamii nzima inakilio na serikali anayoiongoza?

anaweza kanyaga pale Arusha ,Mwanza ,Mbeya na Dar es salaam na akatoka na roho yake?

Labda awe anatembea na jeshi zima , vinginevyo thubutuuuu ,aisee hali siyo poa , jamii imechafukwa , jamii imepoteza hofu ya kifo kabisa ,minakwambia tunayoyasikia nikidogo sana kuwianisha na yanayoongeleka .

Zipo kada nyingi na ngumu ambazo sauti na misimamo yao imefikia tamati .

Huu msiba niwakitofauti sana wazee .

Huu msiba umegusa nyanja zote.

Kunawanajeshi wamefiwa na watoto wao ambao kimsingi ndiyo lilikuwa tumaini lao .
Wapo waliyofiwa na wadogo zao ambao ndiyo yalikuwa malipo ya shukrani kwa family kuwafikisha walipo nao walikuwa wakiwapambania ili kesho waje kugawana majukumu huko mbeleni.

Nao wanavidonda vibichi.

Wapo wanasiasa wa chama tawala na upinzani waliyofiwa na wapendwa wao ambao kimsingi wengine ni miongoni mwa wanaoshiriki kuunda serikali .

Wapo Askari waliyofiwa na wadogo zao ,Mama zao ndugu na wanafamily wengine .

Nao wanavidonda vibichi.

Wapo wanasheria , wapo Walimu , wapo wakulima , wapo waganga wa kienyeji lakini pia wapo wanachama wa chama husika waliyopoteza ndugu na wategemezi wao .

Najaribu kuwaza kwa sura hii ya ubabe ya unataka hutaki lazima utii ,atatoboa?

Ngoja tuone mbinu mpya ya uongozi ili Dunia ijifunze kupitia wao.
 
Haya matokeo yameonyesha kuna uzuzu wa kufikiri wa hali ya juu mno kwa viongozi wa Tanzania, ni nani anaweza kupata 98% ! Hata Mwenyezi Mungu akipigiwa kura, kuna binadamu watamkataa tu......Kwanza waliojitokeza walikuwa wachache kushinda chaguzi nyingi zilizopita. Akili za kawaida tu hata wangetaka kuzipika wengeweka hata angalau range ya 69% to 82%. Wengine wanasema Mama aligoma kabisa kupata chini ya 98%! Alitaka awe juu kuliko viongozi wote waliomtangulia! The highest form of inferiority complex.

Katika mengi ambayo nimejifunza katika Uchaguzi huu, ni kuwa uwezo wa viongozi wa CCM kufikiri, kuisoma jamii uko nyuma mno! Kwa wao (wana CCM) Tanzania badi iko miaka 70! Utategemea nini kama kina Mzee Wasira ndio ndio wapanga mikakati (strategist) wa CCM! Namshangaa sana hata Kikwete ambaye anaonekana anazijua siasa za ndani, kweli amekuwa kipofu na kushindwa kuiona jamii inabadilika.

Matokeo haya yametufanya Watanzania kuwa vituko mno! Hata kama Mama kama atakuwa na roho ya paka na kuendelea kutawala, brand yake imeshuka mno! Na bahati mbaya mno media za nje zimelibebea bango, sioni kama tutakuwa na Waziri wa Mambo ya nje wa kuweza kumuosha Mh Samia, huyu Thabit Kombo ni mtupu mno kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.......Maana mojawapo ya kazi kubwa sasa hivi katika serikali itakayoundwa ni kujaribu Kumsafisha Samia na Tanzania kwa Ujumla!

Ukweli ni kwamba damu iliyomwagika itakuwa ngumu mno kusafishika, na hizi kesi za uhaini ndio zinaifanya serikali ya Tanzania kuonekana kituko mbele ya kadamnasi ya Kitaifa!

Kwa mazingira tuliyonayo issue ya kwenye mapercentage huko watu unadhani hata wanahangaika nako basi , watu huko walishatoka kitambo ,hata angelijipa 800% hiyo watu wala isingeliwahangaisha .

Ngoma ni hii kuwagonga vyuma watoto wa watu ambao wengi pale ni wanafunzi wa vyuo na secondary,wengine bodaboda namawinga na wachache wao ni wale wenye umri wa kati waliyoanza hata kuajiriwa pengine mwaka wa kwanza kazini na wapambanaji wengine .

Lakini mbaya zaidi ni wale waliyopigwa risasi wakiwa kwenye makazi yao .

Kinachouma zaidi ni wale waliyokuwa hadi wamejitolea kwenda kukipigia kura chama husika ,aliyekuwa ametoka hadi alikokuwa ili aje kumpigia kura kiongozi wake akitembea mitaani kwa kujiamini kwakuwa anawino kidoleni akajua itamfanya ajihisi ni mwenye nchi ,masikini wee!

Mama akawala vichwa bila kupembua dadadeeki

Ngoja tuone namna atakavyotoka .
 
Back
Top Bottom