Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
Lazima tuulizane maswali yenye mantiki hapa. Tulienda shule ili tupate ufahamu tusibaki kule au kuwa walewale wa zamani au kama babu zetu wa enzi zile.
Usomapo Biblia hasa kuhusu uzuri wa mbinguni/Peponi au paradiso unakuta panaelezwa kuwa ni pazuri sana na hakuna mfano wa kupafananisha!
Kuhusu uzuri wala si shida zetu. Nachowaza iwapo kuna wingi wa madini kiasi kwamba...
•Barabara zote ni dhahabu
●Malango ni ya Lulu safi
●Mji wenyewe umejengwa kwa dhahabu safi angavu kama kioo.
Halafu huku watu wa Mungu wanataabika hata watumishi wake maisha si mazuri kama utajiri aliona nao wanayemtumikia.
Zaidi soma mwenyewe hapa ufunuo 21:19...
19Mawe ya msingi wa ukuta huo yalikuwa yamepambwa kwa kila aina ya mawe ya thamani. Jiwe la kwanza la msingi lilikuwa jiwe la thamani jekundu, la pili johari ya rangi ya samawati, la tatu kalkedoni, la nne zumaridi,
20la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolito, la nane zabarajadi, la tisa topazi, la kumi krisopraso, la kumi na moja yasintho, na la kumi na mbili amethisto.
21Na ile milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili; kila mlango ulikuwa umetengenezwa kwa lulu moja. Barabara kuu ya mji ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo.
Maandiko yanamtambulisha Mungu ni mwenye
●Upendo
●Huruma
●Na sifa zote nzuri nzuri ni za Mungu. Sikatai.
Sasa ikiwa huyu Mungu ni mwenye Upendo na mwenye huruma Je hatuhurumii huyu Mungu mwenye huruma?
●Je haya madini na mawe ya thamani kede kede anayojengea misingi ya mji yafaa nini kama watu wake alio waumba kwa mfano wake wanakufa njaa Na umaskini wakutopea?
Imagine watu wanakufa migodini wakitafuta mawe ya dhahabu na pengine hata gram1 tu ya dhahabu anakesha na haipati huyu mtu lakini kwa Mungu huko zinakanyagwa kwenye mabarabara.
●Ya faa nini basi?
Hajui kuna watu wanakufa machimboni wakitafuta dhahabu?
Mifano ya kuona kwa macho yangu wachimbaji wakifa machimboni ni pale
Nyangalata karibu na kakola walikufa mamia ya watu pale wakitafuta dhahabu.
Mfano mwingine huu nilikuwa mdogo sana japo ufahamu ulikuwepo ni pale Bulyanhulu kabla mgodini haujanzishwa watu walikufa wengi sana wakifukiwa maduarani!
Je Mungu haya haoni aktoa ridhiki kwa waja wake maana yeye daima hawezi kuishiwa.