Kama binguni kuna madini ya kila aina na ya thamani.Je yanafaida gani ikiwa hayatumiki?

Kama binguni kuna madini ya kila aina na ya thamani.Je yanafaida gani ikiwa hayatumiki?

Quran 67: 1-2

" AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha"
 
Huwezi kumuelewa Mungu ikiwa hujui kusudio lako kuwepo hapa Duniani.

Kwanini leo hii upo hapa dunianj? Nini dhumuni la uwepo wako?

Je ni kwanini tunakufa?

Je dhumuni letu hapa duniani ni kutafuta mali na kujilimbikizia dhahabu na fedha?

Ikiwa dhahabu ni kitu cha maana sana, kwanini tunaiacha hapa hapa duniani?
 
Ili ujue ukubwa, ufalme na utajiri wa Mungu ni lazima ukae chini utafakari.... Mtoa post umejaribu kuonesha dhana yako kuwa Mungu ni maskini, mbahili wa kutoa riziki (dhahabu) na asiye na huruma kwa waje wake.

Umeonesha kuwa umemfikiria Mungu kijuu juu pasi na kutafakari.

Kama unakubali kuwa Mungu ndiye wa kwanza na wa mwisho ni lazina ukiri kuwa kila kitu unachokiona humu Duniani ni cha kwake na kinafuata amri na mfumo aliouweka yeye.

Lazima ukubali kuwa mamlaka yote ni ya kwake, hana mshirika wala mshauri katika maamuzi yake. Anafanya alitakalo, anampa amtakae na anamnyima amtakae kwa elimu na hekima zake.

Mwanadamu ni kiumbe dhaifu sana huzaliwa hapa duniani akiwa hana chochote anachomiliki, kila anachokitafuta na kukusanya katika maisha yake anakipata humu duniani na mwisho wa siku hufa na kukiacha hapahapa duniani.

Hivyo lazima ukubali kuwa mwisho wa yote hays MUNGU ndiye MRITHI wa kila kitu. Kwasababu yeye ndiye wa mwanzo na wa mwisho. Kila kitu hutoka kwake na kila kitu kitarejea kwake yeye.

Mungu ndiye mmiliki wa hazina zote za dhahabu hapa duniani na humpa amtakae na humnyima amtakae. Hapangiwi wala haulizwi kwanini amefanya hivyo. Kwanini? kwasababu kila kitu ni chake yeye na anampa anayemtaka.

Mungu sio mbahili wala haishiwi na utajiri labda uchague kutizama neema zake katika jicho chongo. Kuna neema Mungu amezitawanya kwa watu wote....HEWA, MAJII,MACHO,MASIKIO,PUA n.k unaanzaje kumdhania Mungu ni bahili au masikini wakati hizi neema zote ametugawia bure pasi na kumuomba?

Tambua kuwa maisha haya ya duniani ni MTIHANI kwetu, na hayana maana yoyote ukilinganisha na ufalme uliopo baada ya maisha haya ya duniani.

Mungu anachoangalia ni Imani na matendo yako si dhahabu zako ulizozikusanya...na kuonesha kuwa hazina thamani yoyote mbele yake ni pale unapokufa na kuziacha hapahapa duniani.
 
Mungu ametuandalia wanawake bora zaidi ya hawa wa duniani. Jicho halijawahi kuona, Sikio halijawahi kusikia wala nyoyo haijawahi kuwaza uzuri wa wanawake hao. Kama ametupa wanawake wazuri hapa duniani kwanini ashindwe kutupa wanawake wazuri zaidi huko Akhera?

Ametuandalia na vumbi la Congo, sisi every day ni kupiga kipara tu. Wasichana warembo hawasemi No hao, ukiomba tu unapewa style zote. I can't wait to die bro
 
😂😂😂😂
Africa kuna madini kwani mna faidika na nini maana umasikini bado umetamalaki au ni laana ya umasikini?
 
Kwa mantiki yako hapa mkuu unamaanisha Mungu ashushe Mvua ya Dhahabu na Tanzanite ili watu wote wafaidike sio?
Sasa thamani ya hayo madini itatoka wapi tena kama ni hivyo? Maana kila mtu atakuwa nayo mengi kwahiyo yatakuwa kama mchanga wa kawaida sasa?

Faida ya madini yaliyo mbinguni itakuwa ni mapambo tu sasa kama tunavyotumia sisi kutengeneza vito vya thamani.

Ukisoma maandiko utajua kwamba watu wa Mungu sio maskini wala hawapaswi kuwa maskini, ni swala tu la kutokujua kanuni za Mungu.
Thibitisha uwepo wa huyu Mungu na ueleze kinagaubaga kanuni za huyo Mungu nasi tuzijue.
 
Huwezi kumuelewa Mungu ikiwa hujui kusudio lako kuwepo hapa Duniani.

Kwanini leo hii upo hapa dunianj? Nini dhumuni la uwepo wako?

Je ni kwanini tunakufa?

Je dhumuni letu hapa duniani ni kutafuta mali na kujilimbikizia dhahabu na fedha?

Ikiwa dhahabu ni kitu cha maana sana, kwanini tunaiacha hapa hapa duniani?
Dhumuni la kuwepo wewe hapa duniani ni lipi? unawezaje kuthibitisha kuwa ni kweli upo kwa dhumuni hilo?
 
Lazima tuulizane maswali yenye mantiki hapa. Tulienda shule ili tupate ufahamu tusibaki kule au kuwa walewale wa zamani au kama babu zetu wa enzi zile.

Usomapo Biblia hasa kuhusu uzuri wa mbinguni/Peponi au paradiso unakuta panaelezwa kuwa ni pazuri sana na hakuna mfano wa kupafananisha!

Kuhusu uzuri wala si shida zetu. Nachowaza iwapo kuna wingi wa madini kiasi kwamba...
•Barabara zote ni dhahabu
●Malango ni ya Lulu safi
●Mji wenyewe umejengwa kwa dhahabu safi angavu kama kioo.

Halafu huku watu wa Mungu wanataabika hata watumishi wake maisha si mazuri kama utajiri aliona nao wanayemtumikia.

Zaidi soma mwenyewe hapa ufunuo 21:19...

19Mawe ya msingi wa ukuta huo yalikuwa yamepambwa kwa kila aina ya mawe ya thamani. Jiwe la kwanza la msingi lilikuwa jiwe la thamani jekundu, la pili johari ya rangi ya samawati, la tatu kalkedoni, la nne zumaridi,

20la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolito, la nane zabarajadi, la tisa topazi, la kumi krisopraso, la kumi na moja yasintho, na la kumi na mbili amethisto.

21Na ile milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili; kila mlango ulikuwa umetengenezwa kwa lulu moja. Barabara kuu ya mji ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo.

Maandiko yanamtambulisha Mungu ni mwenye
●Upendo
●Huruma
●Na sifa zote nzuri nzuri ni za Mungu. Sikatai.

Sasa ikiwa huyu Mungu ni mwenye Upendo na mwenye huruma Je hatuhurumii huyu Mungu mwenye huruma?

●Je haya madini na mawe ya thamani kede kede anayojengea misingi ya mji yafaa nini kama watu wake alio waumba kwa mfano wake wanakufa njaa Na umaskini wakutopea?

Imagine watu wanakufa migodini wakitafuta mawe ya dhahabu na pengine hata gram1 tu ya dhahabu anakesha na haipati huyu mtu lakini kwa Mungu huko zinakanyagwa kwenye mabarabara.

●Ya faa nini basi?
Hajui kuna watu wanakufa machimboni wakitafuta dhahabu?


Mifano ya kuona kwa macho yangu wachimbaji wakifa machimboni ni pale
Nyangalata karibu na kakola walikufa mamia ya watu pale wakitafuta dhahabu.

Mfano mwingine huu nilikuwa mdogo sana japo ufahamu ulikuwepo ni pale Bulyanhulu kabla mgodini haujanzishwa watu walikufa wengi sana wakifukiwa maduarani!

Je Mungu haya haoni aktoa ridhiki kwa waja wake maana yeye daima hawezi kuishiwa.View attachment 3519231View attachment 3519232View attachment 3519233
Tunapoanza safari ya elimu kuanzia shule ya msingi hadi tunapohitimu Shahada ya Uzamili (Masters), kwa kiasi kikubwa huwa tunajifunza namna ya kusoma na kufikiri kwa mitazamo ya wengine. Tunasomeshwa fikra, nadharia na uelewa wa wasomi mbalimbali kuhusu fani tofauti za elimu. Hadi kufikia hatua hiyo, mtu huwa bado ni msomaji wa mawazo ya watu wengine. Ni pale mtu anapoanza kufanya utafiti wa kina juu ya jambo maalum—akichunguza, kuhoji na kutoa mchango mpya wa maarifa—ndipo hufikia ngazi ya juu ya usomi, yaani Shahada ya Uzamivu (PhD).

Binadamu hufahamu mambo kupitia ulinganisho wa mifano ambayo akili yake inaweza kuichanganua. Ili mtu ajue jambo kikamilifu, ni lazima pia ajue kinyume chake. Huwezi kuelewa maana ya huruma bila kushuhudia au kupitia ukatili; huwezi kujua shibe bila kuwahi kuwa na njaa; huwezi kuitambua furaha pasipo kuijua huzuni; wala huwezi kuithamini faida bila kuwahi kukutana na hasara.

Kwa mtazamo huo, kama sisi wanadamu tungeishi maisha ya moja kwa moja ya mbinguni bila kupitia maisha ya duniani, nina uhakika tusingeweza kuyaelewa wala kuyathamini maisha hayo. Neema na furaha za huko zisingekuwa na maana kubwa kwetu pasipo uzoefu wa maisha ya duniani. Mfano mzuri ni dhahabu: ni madini kama madini mengine, lakini thamani yake kubwa inatokana na ugumu wa upatikanaji wake na mchakato mrefu wa kuitengeneza hadi iwe tayari kutumika. Vivyo hivyo, madini mengine hutokana na miamba ya mawe au viumbe wa baharini, yote yakiwa chini ya mfumo aliouweka Muumba mwenyewe.

Kwa hekima hiyo hiyo, Muumba ameandaa mfumo wa maisha ya duniani ili kumjenga mwanadamu kimaadili, kiakili na kiroho. Hivyo, pale atakapowapa wanadamu uzima wa milele katika Paradiso, haitakuwa vigumu kwao kufurahia neema hizo wala kukubali haki ya malipo hayo, kwa kuwa watakuwa wameishi duniani kwa kumtii na kumuabudu Mungu wao. Mwisho wa safari hiyo huwa ni uzima wa milele, thawabu ya utii na imani ya kweli.
 
Faida yake ni kuyaangalia tu mkuu na kufurahi nafsi,mfano matako makubwa kwa pisi Kali yanafaida Gani kwetu wenye macho?
 
Back
Top Bottom