Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 4,994
- 9,625
Mungu ametuandalia wanawake bora zaidi ya hawa wa duniani. Jicho halijawahi kuona, Sikio halijawahi kusikia wala nyoyo haijawahi kuwaza uzuri wa wanawake hao. Kama ametupa wanawake wazuri hapa duniani kwanini ashindwe kutupa wanawake wazuri zaidi huko Akhera?
Mungu ametuandalia wanawake bora zaidi ya hawa wa duniani. Jicho halijawahi kuona, Sikio halijawahi kusikia wala nyoyo haijawahi kuwaza uzuri wa wanawake hao. Kama ametupa wanawake wazuri hapa duniani kwanini ashindwe kutupa wanawake wazuri zaidi huko Akhera?
Thibitisha uwepo wa huyu Mungu na ueleze kinagaubaga kanuni za huyo Mungu nasi tuzijue.Kwa mantiki yako hapa mkuu unamaanisha Mungu ashushe Mvua ya Dhahabu na Tanzanite ili watu wote wafaidike sio?
Sasa thamani ya hayo madini itatoka wapi tena kama ni hivyo? Maana kila mtu atakuwa nayo mengi kwahiyo yatakuwa kama mchanga wa kawaida sasa?
Faida ya madini yaliyo mbinguni itakuwa ni mapambo tu sasa kama tunavyotumia sisi kutengeneza vito vya thamani.
Ukisoma maandiko utajua kwamba watu wa Mungu sio maskini wala hawapaswi kuwa maskini, ni swala tu la kutokujua kanuni za Mungu.
Dhumuni la kuwepo wewe hapa duniani ni lipi? unawezaje kuthibitisha kuwa ni kweli upo kwa dhumuni hilo?Huwezi kumuelewa Mungu ikiwa hujui kusudio lako kuwepo hapa Duniani.
Kwanini leo hii upo hapa dunianj? Nini dhumuni la uwepo wako?
Je ni kwanini tunakufa?
Je dhumuni letu hapa duniani ni kutafuta mali na kujilimbikizia dhahabu na fedha?
Ikiwa dhahabu ni kitu cha maana sana, kwanini tunaiacha hapa hapa duniani?
Huwezi pinga namna hiyo qmamae?Mbingu haipo.
Jehanam haipo.
Mungu hayupo.
Shetani hayupo.
Biblia na Quran ni hekaya za kutungwa.
Tunapoanza safari ya elimu kuanzia shule ya msingi hadi tunapohitimu Shahada ya Uzamili (Masters), kwa kiasi kikubwa huwa tunajifunza namna ya kusoma na kufikiri kwa mitazamo ya wengine. Tunasomeshwa fikra, nadharia na uelewa wa wasomi mbalimbali kuhusu fani tofauti za elimu. Hadi kufikia hatua hiyo, mtu huwa bado ni msomaji wa mawazo ya watu wengine. Ni pale mtu anapoanza kufanya utafiti wa kina juu ya jambo maalum—akichunguza, kuhoji na kutoa mchango mpya wa maarifa—ndipo hufikia ngazi ya juu ya usomi, yaani Shahada ya Uzamivu (PhD).Lazima tuulizane maswali yenye mantiki hapa. Tulienda shule ili tupate ufahamu tusibaki kule au kuwa walewale wa zamani au kama babu zetu wa enzi zile.
Usomapo Biblia hasa kuhusu uzuri wa mbinguni/Peponi au paradiso unakuta panaelezwa kuwa ni pazuri sana na hakuna mfano wa kupafananisha!
Kuhusu uzuri wala si shida zetu. Nachowaza iwapo kuna wingi wa madini kiasi kwamba...
•Barabara zote ni dhahabu
●Malango ni ya Lulu safi
●Mji wenyewe umejengwa kwa dhahabu safi angavu kama kioo.
Halafu huku watu wa Mungu wanataabika hata watumishi wake maisha si mazuri kama utajiri aliona nao wanayemtumikia.
Zaidi soma mwenyewe hapa ufunuo 21:19...
19Mawe ya msingi wa ukuta huo yalikuwa yamepambwa kwa kila aina ya mawe ya thamani. Jiwe la kwanza la msingi lilikuwa jiwe la thamani jekundu, la pili johari ya rangi ya samawati, la tatu kalkedoni, la nne zumaridi,
20la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolito, la nane zabarajadi, la tisa topazi, la kumi krisopraso, la kumi na moja yasintho, na la kumi na mbili amethisto.
21Na ile milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili; kila mlango ulikuwa umetengenezwa kwa lulu moja. Barabara kuu ya mji ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo.
Maandiko yanamtambulisha Mungu ni mwenye
●Upendo
●Huruma
●Na sifa zote nzuri nzuri ni za Mungu. Sikatai.
Sasa ikiwa huyu Mungu ni mwenye Upendo na mwenye huruma Je hatuhurumii huyu Mungu mwenye huruma?
●Je haya madini na mawe ya thamani kede kede anayojengea misingi ya mji yafaa nini kama watu wake alio waumba kwa mfano wake wanakufa njaa Na umaskini wakutopea?
Imagine watu wanakufa migodini wakitafuta mawe ya dhahabu na pengine hata gram1 tu ya dhahabu anakesha na haipati huyu mtu lakini kwa Mungu huko zinakanyagwa kwenye mabarabara.
●Ya faa nini basi?
Hajui kuna watu wanakufa machimboni wakitafuta dhahabu?
Mifano ya kuona kwa macho yangu wachimbaji wakifa machimboni ni pale
Nyangalata karibu na kakola walikufa mamia ya watu pale wakitafuta dhahabu.
Mfano mwingine huu nilikuwa mdogo sana japo ufahamu ulikuwepo ni pale Bulyanhulu kabla mgodini haujanzishwa watu walikufa wengi sana wakifukiwa maduarani!
Je Mungu haya haoni aktoa ridhiki kwa waja wake maana yeye daima hawezi kuishiwa.View attachment 3519231View attachment 3519232View attachment 3519233
Jibu hoja kwa hoja.Huwezi pinga namna hiyo qmamae?