Niliujua unafiki wa Bulembo alipo kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa FAT au TFF siku hizi. Huyu yeye anacho angalia maishani make ni FEDHA tu basi. Ni halali au ni haramu hilo utajua wewe.
Wakati ule alikuwa CHAWA wa Ndolanga na ndio alikuwa anamwambia kwa jinsi wajumbe wanavyo mpenda atadumu pale FAT milele.
Siku zile wajumbe wa mkutano mkuu walikuwa 62 tu, sasa yeye Bulembo , Marehemu Makanjira na Mwingine kutoka Rukwa nimemsahau jina, walikuwa wanamshauri Ndolanga awahonge wajumbe 37 tu ili hawa wakimpa kura zao tayari anakuwa mshindi na anakuwa Mwenyekiti wa FAT siku hizi TFF. Kwahiyo walipewa rushwa kubwa kupitia huyu Bulembo na Makanjira aliye kuwa mjumbe wa kamati kuu akitokea Iringa.
Serikali ilipo ona kuwa kumtoa Ndolanga kwa kura isingewezekana , walicho fanya kupitia BMT wakaongeza idadi ya wapiga kura mpaka kufikia 120. Katika uchaguzi ulio fuata serikali walikuwa upande wa LEODIGA CHILLA TENGA , na kumwaga TAKUKURU kila kona kuhakikisha Ndolanga na hawa akina Bulembo hawapati fursa ya kuwa rubuni wajumbe kwa RUSHWA. Ndolanga akashindwa katika uchaguzi ule.
Baada ya hapo huyu Bulembo aka akahamia kwenye siasa.....na kamwe hakuacha kuwa CHAWA. Ni mtu anaye angalia tumbo lake.
Nilicho jifunza katika maisha CHAWA ni wabaya kuliko SHETANI. Shetani ana huruma kwasababu akijua wewe unampambania Mungu , anakuacha uendelee na Mungu anakubali kushindwa. CHAWA huwa hawakubali kushindwa, ni wabaya.
Hapo alipo fikishwa Polepole ni lazima akubali kushindwa. Hawa darasa la saba akina Bulembo watammaliza siyo tu kisiasa lakini anaweza akajikuta amepoteza vingi including life.
ATAKWENDA POLISI, ATASHANGAA, HAWATA MSIKILIZA KWASABABU WATAKUWA WANASOMA UPEPO WAJUE WALIO MFANYIA HAYO NI CCM AU CHAWA WA TAIFA??
Polepole akubali kuwa Magufuli is No More, na huo ndio mwisho wao popote walipo, iwe bandarini, Dodoma au kwenye Siasa ndio mwisho wa ENZI.
Huyu CHAWA mbobevu amejua hilo, amesha jua ahamie shati lipi. Kwasasa yupo na Samia , kabla alikuwa kwa Kikwete. Huyo ndio Bulembo ninaye mjua mimi.