Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kumekuwa na ubishi kuhusu kama kwa sasa Samia Suluhu anaongoza awamu ya tano au ya sita. Labda hilo sio jambo la maana. Jambo la msingi ni kwamba rais Samia Suluhu anaongoza awamu ambayo haitambuliki kikatiba kama ni awamu yake ya kwanza ya uongozi, bali amechukua madaraka ya uraisi kutokana na kifo cha rais aliyekuwapo madarakani. Samia hakuchaguliwa kwa kura, hivyo uraisi wake wa sasa ni wa kuziba pengo tu.
Kwa jinsi hiyo basi, awamu ya kwanza ya Samia Suluhu itakuwa mwaka 2025 ikiwa CCM watampitisha kuwa mgombea wao wa uraisi. Na tukumbuke kwamba CCM wana utaratibu wa kumpitisha raisi aliyepo madarakani kuendelea kuwa chaguo lao la mgombea urais.
Ikiwa Samia atagombea urais mwaka 2025 na kupita, itakapofika uchaguzi wa 2030 atakuwa tena na haki ya kikatiba ya kugombea uraisi kwa awamu yake ya pili, na akipita atakuwa raisi hadi mwaka 2035.
Kwa hiyo basi, Samia anaweza kuwa Mtanzania wa kwanza kuwa rais kwa muda wa miaka 14 kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Hiyo ni habari njema kwa Watanzania wengi, na habari mbaya kwa wengine, lakini ndio ukweli uliopo.