Huhitaji kukaa madarakani miaka mingi ili ukete mabadiliko.
Kwa mujibu wa katiba, (sikumbuki kifungu), Rais aliyepo madarakani akifariki, makamu wa Rais ataapishwa kuwa Rais, na huyo Rais aliyeapishwa, kama muda uliobakia wa Rais aliyefariki si chini ya miaka 3, kipindi anachomalizia cha Rais aliyefariki, kitahesabika ni kipindi chake cha kwanza. Hivyo kwa mujibu wa katiba, Mama Samia atakuwa amebakiwa na kipindi kimoja cha kugombea. Hiyo ndiyo sababubua Serikali hii kuitwa awaku ya 6.
Hiyo miaka 9, na hata akiamua asigombee, ndani ya hii miaka yake 4, akijishughulisha zaidi na kujenga taasisi imara, akianzia na katiba bora mpya, nchi itakwenda vizuri na kwa mafanikio makubwa. Nchi haitarudi kwenye utawala ule dhalimu wa awamu ya 5.