Adverse Effect
JF-Expert Member
- Oct 8, 2017
- 3,700
- 9,570
CHADEMA ya sasa itajisimamia kupitia wananchi na wanachama wake watiifu, waaminifu na wakweli. Hakuna kurudi nyuma.
Chadema sio lazima awe na Mbowe japo naungana na hoja yako , ichi chama kina watu so back up kwa chama hichi sio shida, wenyeviti wa chadema wa kanda wote ni balaa,hujaweka mikoa ,wilaya ,muundo wa chama cha chadema ni wakipekee sana that's kukiua ichi chama ni ngumu, na mbaya ambacho watu na wapinzani wao hawajui chadema imejijenga kama familia.Kwa kiasi kikubwa agenda ya No reforms No election imefanikiwa kupenya na kuwavuruga watawala. Kukataa kwamba haiwasumbui itakuwa ni kujidanganya
Watu wanaweza kudharau yanayoendelea mitandaoni lakini huo ndio uhalisia wa yanayoendelea kwenye jamii kwasababu walioko mitandaoni ndio walioko kwenye jamii. Pengine huko mitandao wako huru zaidi kuliko nje
Unaweza kuona namna Heche na wenzake walivyoisukuma No reforms No election wakati Tundu Lisu akiwa katikati ya nondo za keko halafu unawaza huu mziki angekuwepo na yeye ingekuwaje sasa hivi?
Ni wazi kabisa Heche na wenzake walipofikia wanahitaji "back - up" itakayowarahisishia kazi hasa ukizingatia Oktoba bado ni mbali sana na wanaweza kuzidiwa na dola humo katikati
Yawezekana mwanzo Mbowe hakuamini kama watu wataipokea No reforms No election kama walivyoipokea. Huko aliko "mapumzikoni" ameona mwitikio wa watu. Naamini anafaa kuwa "back - up" ya muhimu sana hapo katikati kwasababu kuna kila dalili ya Tundu Lisu kucheleweshwa kumaliza kesi yake hadi uchaguzi upite
Hali ilivyo hawawezi kumuachilia wala kumuhukumu kwa sasa kabla ya uchaguzi. Aliyebaki mwenye uzoefu wa nginja nginja na dola ni Freema Aikael Mbowe. Kwangu mimi naona waweke tofauti zao pembeni aingie ulingoni kama asaidie vijana ili dola ipate funzo la kuheshimu nguvu ya umma