Kama chanzo cha uhai kinaweza kubadilika basi uhai wenyewe hauna msingi thabiti hadi sasa. Je, ni upi msingi wa uhai?

Ungekuwa umesoma elimu ya atomic energy physics usinge kujakusumbua watu nahisi.
Sijasoma ndio maana nimeileta humu ili mliosoma mtuelezee... Haya lete vitu kutokea upande huo mkuu.
 
Hapa unajibana mkuu na kujipa excuse ya kurudi nyuma katika kuyafikira mambo.
Nimerudi nyuma nikakuuliza hivi...👇

Kama uhai lazima uwe na msingi wake, Je msingi wa "msingi wa uhai" ni nini?

Umeshindwa kujibu.

Sasa najibana vipi?

Au ni wewe umeshindwa kutoa majibu?

Narudia tena kukwambia,

Hatuwezi kujua tusivyo vijua, ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua.

Ndio maana umeshindwa kujua na kujibu msingi wa "msingi wa uhai" ni nini?

Kwa sababu bado hatujui.

Hata wewe mwenyewe umekiri hujui msingi wa uhai ni nini, Ndio maana umeanzisha hii mada.
 
Mbona nimekujibu hilo swali ya kwamba tunajadili msingi wa uhai kwasababu tunaona vyanzo so hatuwezi kuruka hatua ni Bora tuutafute msingi wake kwanza then ndio tuje tujadili huo msingi wa msingi wake ni nini.😅😅😅
 
Chanzo kinaweza kuwepo au vyanzo vinaweza kuwepo bila msingi.

Chanzo hakihitaji msingi.

Maana kuna vitu vinatokea bila msingi wowote ule.
 
Turudi kwenye mada,.. Msingi wa uhai ni nini?

NB: Unalazimisha theory iwe fact, lakini kamwe theory haiwezi kuwa fact mpaka itakapokoma kuwa theory.
 
Upo hapa duniani ili UFE unataka nini tena kufukua mambo ambayo yanafikirisha.?

Ishi ili ufe
 
Turudi kwenye mada,.. Msingi wa uhai ni nini?
Nini maana ya Msingi kwa muktadha wako ? Mimi nimekupa maana ya msingi kwa macho ya Nature (Ecosystem) / Sustainability kama huwezi ku conform na nature basi utakuwa extinct
NB: Unalazimisha theory iwe fact, lakini kamwe theory haiwezi kuwa fact mpaka itakapokoma kuwa theory.
Ni kitu gani huelewi kuhusu neno known (recognized, familiar, or within the scope of knowledge) Hio ndio maana ya known.., Sasa unganisha ni sentesi niliyosema known to be factual..., Je hio ina maana sawa na fact ?!!!!
 
Uhai ni energy.kila kitu ni energy...vyote ni hai kwa mungu kufa ni kitu feki
 
Swali zuri kajifunza energy ni nini na sifa yake ...hapo utajua siri ya mungu ni nini na kaumba vitu vyote kwa mbinu gani?
Ni wapi kwa kwenda kujifunzia? Lakini pia hata kama unachosema ni kweli why huyo Mungu asionekane kama ndio msingi na badala yake yeye huonekana kama chanzo tu?
 
Chanzo halisi ni linear yaani kinakwenda mbele tu not cyclic,yaani ni umilele not kifo na hakina mwanzo maana hata mwanzo uliumbwa pia.
 
Ni wapi kwa kwenda kujifunzia? Lakini pia hata kama unachosema ni kweli why huyo Mungu asionekane kama ndio msingi na badala yake yeye huonekana kama chanzo tu?
Vitu vyote vipo ndani ya mungu vimeumba ndani yake...tupo ndani ya Mungu...sasa unataka kuona msingi gani tena
 
Msingi wa uhai ni Mungu mwenyewe na ndo maana hakuna mtu yeyote au kitu chochote kinaweza kutoa uhai

Biblia inasema
Mungu alimuumba mwanadamu kwa udogo kisha akampulizia pumzi ya uhai mwanadamu akawa hai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…