Kama Corona imeisha magari yaruhusiwe kusimamisha abiria, hasa Dar es Salaam

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,876
Amani iwe kwenu wakuu!

Kwa heshima na taadhima nimpongeze mheshimiwa Rais wetu kwa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku vyema. Lakini pia nimpongeze kwa maamuzi yaliyokuwa magumu na ambayo wengi hatukukubaliana nayo kwanza ya kuruhusu watu waendelee na shughuli zao katikati ya janga la corona (COVID-19). Hata hivyo tukubaliane wote kwamba maamuzi yale aliyoyachukua ndiyo yalikuwa maamuzi sahihi maana hata nchi zilizoweka lock down au partial lock down wameona haiwezi tena kuendelea wameamua kufungua nchi zao.

Lakini mheshimiwa baada ya kufungua shule hali ya usafiri hapa jijini imekuwa ngumu sana, Wananchi wanateseka sana kwa adha ya usafiri. Ugumu wa kupata magari umeongeza gharama za maisha kwa Wananchi kwa kiwango kikubwa sana. Mfano usafiri wa Gongo la Mboto Makumbusho ulikuwa shilingi 600 tu lakini kwa sasa ili upate gari ni lazima uamke saa tisa hadi kumi ndiyo upate gari , au upande gari kutoka Gongo la Mboto hadi Mombasa au Banana 400 upande gari urudi nayo hadi Gongo la mboto kisha utoe tena sh 600 ambayo ndiyo nauli ya kawaida (hii inaitwa kuzunguka na gari).

Hali ni mbaya sana kwa wakazi wa Chanika, Mbagala na maneo mengine ya aina hiyo. Mfano kuna ndugu yangu anaishi Chanika huamka asiku wa saa tisa kisha hupanda pikipiki sh 2000 hadi Buyuni au Kinyamwezi ndiyo apate gari la kuzungukia kwenda Machinga Complex ambapo analipa tena sh 1100 (750 nauli ya kawaida na 350 ya kuzungukia ). Hata hivyo siku 4 zilizopita vijana tunaofanya nao shughuli za ajira ndogo ya usafi walifukuzwa kazi kosa la kuchelewa kufika kazini kwa wiki nzima wakidai huko Chanika kwao magari ya Gerezani Machinga Complex sasa hivi hayafiki.

Wanadai wanaamka saa tisa za usiku ila kupata gari labda mpaka saa mbili au saa tatu asubuhi. Mheshimiwa Rais kwa mfanya usafi kama mimi nalipwa mshahara wa chini ya 200,000 huku nikiwa na familia kwa hali hii ya usafiri wa kuzunguka na gari yaani badala ya nauli ya sh 400 natumia sh 1000 hapo ni asubuhi tu huku jioni hali ikiwa mbaya zaidi kweli tutaweza? Je, huku ndiko kuishi kama mashetani au ndiyo mafanikio ya kuingia uchumi wa kati?

Mheshimiwa Rais adha ya usafiri DSM lilisababishwa na katazo la watu kusimama kwenye magari inaleta shida hasa msongo wa mawazo, vurugu katika ndoa, watu kukosa kazi kwa kuchelewa kufika kazini, inaongeza gharama za maisha kwa wananchi masikini na isipoangaliwa vizuri hata wanafunzi wengi watazalishwa na makondakta na madereva wasio wavumilivu lakini pia itaongeza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa shule. Mheshimiwa hali ni mbaya sana kwa raia wako linapokuja suala la usafiri.

Kwa sasa tumeamua kuishi kwa imani au tumeshaamua liwalo na liwe kwa corona tena tuliifanyaia sendoff pale coco beach (hii iliandaliwa na mkuu wa mkoa) na juzi tumefanya harusi kabisa pale Tanganyika Pekars. Lakini hata kwenye magari sasa hivi watu hawavai barakoa, kwenye pantoni hakuna barakoa wala kunawa, Kariakoo na Posta ikiwa na hali hiyo hiyo hata wewe kwenye hotuba zako umesisitiza kwamba corona haipo Tanzania tena tuchape kazi.

Hivyo basi mheshimiwa sana Rais wa JMT tunaomba uruhusu magari yaanze kusimamisha abiria bila kujali kelele za Mabeberu maana hii ni vita ili tuchape kazi walau kufikia 2025 tuwe tumefika uchumi wa kati wa usd 3000 kwa mwaka kwa kila mtu kama ilivyokuwa kwenye mpango wa taifa. Aksante sana kwa muda wako, ni mimi niliye mdogo kati ya wadogo wote.

Kindikwili-
 
Baadhi ya magari wameshaanza kusimamisha watu japo kwa kuibia ibia..gari za Kawe, Mbezi, hata Mawasiliano pia.

Sidhani kama inahitaji kuruhusiwa kwa sababu naona hii inatokea automatically ni suala la muda tu.kikubwa uvumilivu.
 
Baadhi ya magari wameshaanza kusimamisha watu japo kwa kuibia ibia..gari za kawe, Mbezi, hata mawasiliano pia.
Sidhani kama inahitaji kuruhusiwa kwa sababu naona hii inatokea automatically ni suala la muda tu.kikubwa uvumilivu.

Hatutaki waibie ibie waruhusiwe wajaze watu kuokoa hali ya mambo, kumbuka katazo lilitolewa na mamkala na linatakiwa liruhusiwe na mamlaka.
 
Kusimamisha abiria sio sahihi hata kama hakuna Corona.

Ni Umasikini, Ujinga na kutokuwa makini kufanya mipango na kujali afya za watu ndio kumepelekea watu kujazana mpaka kusimamishwa kwenye daladala na mwendo kasi.
 
Mkuu unachokisema ni kweli lakini kwa miundombinu ya barabara za hapa Tanzania (ubovu na uwembemba), magari madogo yanayotumika kusafirisha abiria, umasikini wa wananchi kununua magari binafsi na wingi wa watu katika jiji hili ndilo sababu ya Raia kusimamishwa kwenye magari kama magunia.

Kwa kipindi hiki kifupi solution bado ni kusimamisha watu ila lazima tutafute solution ya kudumu ya jinsi gani raia wetu watasafiri kwa heshima na utu ndani ya magari ya abiria.
 
Corona haijaisha bali tumeambiwa imepungua kwa kiasi kikubwa.
 
Kilichoongezeka si wanafunzi? Wao wasimame ila utaratibu wa level seat kama kawaida.
 
Wameongezeka wanafunzi ambalo ni kundi kubwa, walimu, wauza mihogo, juice, stationery, non professional employees wa mashuleni na mnyororo wote unaoishi mjini kutegemea uwepo wa shule.
 
Sasa hivi magari mengine wanasimamisha abiria ila wengine bado wanaogopa.
 
Maendeleo ya mini ni pamoja na kuwa na usafiri wakiistaarabu kukaa level seat sio kujazana. Jiji liombe uwekezaji binafsi wa mabasi badala ya kurudia acha ya kujaza abiria. School bus binafsi ziruhusiwe nk.
 
Umesema ukweli hadi niltaka kuwasemea wakazi wa huko niandike juu ya hili maana sipachi picha mateso mnayopata na niliwahi kuishi huko na nilikua mhanga sio siri hiyo route sio kwamba tu ni kipindi hichi cha Corona hiyo route ya magari ya G.mboto makumbusho panahitaji kuongezewa magari maana kuna uhaba sana
Amani iwe kwenu wakuu!

Kwa heshima na taadhima nimpongeze mheshimiwa Rais wetu kwa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku vyema. Lakini pia nimpongeze kwa maamuzi yaliyokuwa magumu na ambayo wengi hatukukubaliana nayo kwanza ya kuruhusu watu waendelee na shughuli zao katikati ya janga la corona (COVID-19). Hata hivyo tukubaliane wote kwamba maamuzi yale aliyoyachukua ndiyo yalikuwa maamuzi sahihi maana hata nchi zilizoweka lock down au partial lock down wameona haiwezi tena kuendelea wameamua kufungua nchi zao.

Lakini mheshimiwa baada ya kufungua shule hali ya usafiri hapa jijini imekuwa ngumu sana, Wananchi wanateseka sana kwa adha ya usafiri. Ugumu wa kupata magari umeongeza gharama za maisha kwa Wananchi kwa kiwango kikubwa sana. Mfano usafiri wa Gongo la Mboto Makumbusho ulikuwa shilingi 600 tu lakini kwa sasa ili upate gari ni lazima uamke saa tisa hadi kumi ndiyo upate gari , au upande gari kutoka Gongo la Mboto hadi Mombasa au Banana 400 upande gari urudi nayo hadi Gongo la mboto kisha utoe tena sh 600 ambayo ndiyo nauli ya kawaida (hii inaitwa kuzunguka na gari).

Hali ni mbaya sana kwa wakazi wa Chanika, Mbagala na maneo mengine ya aina hiyo. Mfano kuna ndugu yangu anaishi Chanika huamka asiku wa saa tisa kisha hupanda pikipiki sh 2000 hadi Buyuni au Kinyamwezi ndiyo apate gari la kuzungukia kwenda Machinga Complex ambapo analipa tena sh 1100 (750 nauli ya kawaida na 350 ya kuzungukia ). Hata hivyo siku 4 zilizopita vijana tunaofanya nao shughuli za ajira ndogo ya usafi walifukuzwa kazi kosa la kuchelewa kufika kazini kwa wiki nzima wakidai huko Chanika kwao magari ya Gerezani Machinga Complex sasa hivi hayafiki.

Wanadai wanaamka saa tisa za usiku ila kupata gari labda mpaka saa mbili au saa tatu asubuhi. Mheshimiwa Rais kwa mfanya usafi kama mimi nalipwa mshahara wa chini ya 200,000 huku nikiwa na familia kwa hali hii ya usafiri wa kuzunguka na gari yaani badala ya nauli ya sh 400 natumia sh 1000 hapo ni asubuhi tu huku jioni hali ikiwa mbaya zaidi kweli tutaweza? Je, huku ndiko kuishi kama mashetani au ndiyo mafanikio ya kuingia uchumi wa kati?

Mheshimiwa Rais adha ya usafiri DSM lilisababishwa na katazo la watu kusimama kwenye magari inaleta shida hasa msongo wa mawazo, vurugu katika ndoa, watu kukosa kazi kwa kuchelewa kufika kazini, inaongeza gharama za maisha kwa wananchi masikini na isipoangaliwa vizuri hata wanafunzi wengi watazalishwa na makondakta na madereva wasio wavumilivu lakini pia itaongeza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa shule. Mheshimiwa hali ni mbaya sana kwa raia wako linapokuja suala la usafiri.

Kwa sasa tumeamua kuishi kwa imani au tumeshaamua liwalo na liwe kwa corona tena tuliifanyaia sendoff pale coco beach (hii iliandaliwa na mkuu wa mkoa) na juzi tumefanya harusi kabisa pale Tanganyika Pekars. Lakini hata kwenye magari sasa hivi watu hawavai barakoa, kwenye pantoni hakuna barakoa wala kunawa, Kariakoo na Posta ikiwa na hali hiyo hiyo hata wewe kwenye hotuba zako umesisitiza kwamba corona haipo Tanzania tena tuchape kazi.

Hivyo basi mheshimiwa sana Rais wa JMT tunaomba uruhusu magari yaanze kusimamisha abiria bila kujali kelele za Mabeberu maana hii ni vita ili tuchape kazi walau kufikia 2025 tuwe tumefika uchumi wa kati wa usd 3000 kwa mwaka kwa kila mtu kama ilivyokuwa kwenye mpango wa taifa. Aksante sana kwa muda wako, ni mimi niliye mdogo kati ya wadogo wote.

Kindikwili-
 
Hiyo route ni kibokooo nakumbuka nilikua nadamka saa 9 na natakiwa nifike mlimani saa moja kamili acha tu niliathirika hadi kisaikolojia sina hamu kabisa nilikoma aisee

Back
Top Bottom