Kama Corona imeisha magari yaruhusiwe kusimamisha abiria, hasa Dar es Salaam

Kama Corona imeisha magari yaruhusiwe kusimamisha abiria, hasa Dar es Salaam

Hata mm jana niliona
Baadhi ya magari wameshaanza kusimamisha watu japo kwa kuibia ibia..gari za Kawe, Mbezi, hata Mawasiliano pia.

Sidhani kama inahitaji kuruhusiwa kwa sababu naona hii inatokea automatically ni suala la muda tu.kikubwa uvumilivu.
 
Ungejua hiyo route ilivyo na uhaba wa magari hata usingeshauri hivyo muhimu naona hiyo route magari yangeongezwa tu
Kusimamisha abiria sio sahihi hata kama hakuna Corona.

Ni Umasikini, Ujinga na kutokuwa makini kufanya mipango na kujali afya za watu ndio kumepelekea watu kujazana mpaka kusimamishwa kwenye daladala na mwendo kasi.
 
Nunua pukipiki acha kulialia Mkuu

Dah mkuu sijui umefikiri vyema kabla ya kuandika au umeandika tu bila ya kufikiri, unadhani kila anaiyeishi DSM anaweza kununua pikipiki? unajua madhara ya pikipiki kwa raia wa jiji hili? Umewahi kufikiria nini kitatokea kama kila mtu atakuwa na pikipiki?
 
MAWAZO YA KIMASIKINI NDO HAYA

Kweli ni mawazo ya kimaskini yapi yakwako ya kitajiri? mkuu usipende kujionesha mjinga kati ya watu. Ni ujinga kukosoa hoja ya mtu bila ya kutoa hoja mbadala hata kama hiyo hoja ni ya kijinga
 
Nunueni baiskel,wabongo bana

Aksante ila mkuu mimi siongelei huko kwenu wilayani uvinza , naongealea dsm kama umewahi kufika huku ukiendesha baiskeli mwaka mzima kwa route ya Gongo la Mboto Posta au Chanika Machinga Complex (50+kms) au mbagala posta bila kusindikizwa ahera kwa kugongwa na gari au wenye pikipiki basi nawe utakuwa mwanaume. Huku si kama chato gari moja baada ya lisaa
 
Hapana seat level iendelee hivo hivo, kwanza kuna ustaarabu, usafi, then tunawahi kufika tunakoelekea.

Sikatai mkuu ila nini suluhisho la haraka kumaliza tatizo la ukosefu wa magari kwasasa? halafu kwa miundombinu yetu ya barabara wingi wa magari pia inachangia foleni . Tungeweza barabara zetu zingekuwa nzuri matajiri wangewekeza kwenye magari makubwa ya abiria kama Eichers ili haya magari madogo kama coaster zitoke njiani- hapa unapunguza wingi wa magari njiani ka kuchukua watu wengi zaidi kwenye gari moja
 
Hivyo basi mheshimiwa sana Rais wa JMT tunaomba uruhusu magari yaanze kusimamisha abiria bila kujali kelele za Mabeberu maana hii ni vita ili tuchape kazi
Hongera mlala hoi kwa kutoa comment. Ni ukweli usiopingika kwamba katazo la kusimama limetugharimu wengi wetu tusio na vyombo vya usafiri. Hali ni mbaya kwa kweli maana unafika kazini saa tatu asubuhi boss anakuangalia tu mpaka unajionea aibu mwenyewe. Waruhusu tu tusimama maana walala hoi wengi ndio hukaa chanika, mbande na wengine hata kisemvule ila huja tu mjini kujitafutia riziki. LATRA waruhusu tu watu wasimame kama zamani ila tu kwa sharti la kuvaa barakoa
 
Back
Top Bottom