Baadhi ya magari wameshaanza kusimamisha watu japo kwa kuibia ibia..gari za Kawe, Mbezi, hata Mawasiliano pia.
Sidhani kama inahitaji kuruhusiwa kwa sababu naona hii inatokea automatically ni suala la muda tu.kikubwa uvumilivu.
Kusimamisha abiria sio sahihi hata kama hakuna Corona.
Ni Umasikini, Ujinga na kutokuwa makini kufanya mipango na kujali afya za watu ndio kumepelekea watu kujazana mpaka kusimamishwa kwenye daladala na mwendo kasi.
Nunua pukipiki acha kulialia Mkuu
MAWAZO YA KIMASIKINI NDO HAYA
Nunueni baiskel,wabongo bana
Hapana seat level iendelee hivo hivo, kwanza kuna ustaarabu, usafi, then tunawahi kufika tunakoelekea.
Corona haijaisha bali tumeambiwa imepungua kwa kiasi kikubwa.
Hongera mlala hoi kwa kutoa comment. Ni ukweli usiopingika kwamba katazo la kusimama limetugharimu wengi wetu tusio na vyombo vya usafiri. Hali ni mbaya kwa kweli maana unafika kazini saa tatu asubuhi boss anakuangalia tu mpaka unajionea aibu mwenyewe. Waruhusu tu tusimama maana walala hoi wengi ndio hukaa chanika, mbande na wengine hata kisemvule ila huja tu mjini kujitafutia riziki. LATRA waruhusu tu watu wasimame kama zamani ila tu kwa sharti la kuvaa barakoaHivyo basi mheshimiwa sana Rais wa JMT tunaomba uruhusu magari yaanze kusimamisha abiria bila kujali kelele za Mabeberu maana hii ni vita ili tuchape kazi