Kama David Silinde aliitumikia CCM kwa siri kwa miaka 5 aliyokuwa Bungeni inawezekana sasa anaitumikia CHADEMA akiwa CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Maneno huumba.

David Silinde kwa kutamka hadharani kwamba yeye ni "Chawa" kwa miaka 5 aliyokuwa Bungeni alikuwa akiitumikia CCM kwa siri amefungua mlango kwa maadui wa CCM kuweza kumtumia kwa sababu anaweza "kutumika"

Binafsi sikutegemea kauli kama hii itoke kwa mwanasiasa kijana, hata hivyo nawapongeza wajumbe wa Tunduma kwa kulijua hilo na kufanya maamuzi sahihi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hata hivyo amepata kura nyingi sana tofauti na tulivyodhani.

Naona Kama ana nafasi kubwa ya kupitishwa na mamlaka za juu.

Kama alitumika CCM akiwa chadema unategemea anaipenda chadema? Yaani awe CCM aitumikie chadema?

Sidhani.
 
Hata hivyo amepata kura nyingi sana tofauti na tulivyodhani.

Naona Kama ana nafasi kubwa ya kupitishwa na mamlaka za juu.

Kama alitumika CCM akiwa chadema unategemea anaipenda chadema? Yaani awe CCM aitumikie chadema?

Sidhani.

Huyo ni double agent wa tumbo lake.
 
Hawa ndio wanaitwa wanasiasa malaya a.k.a Kahaba
 
Kuwa mzalendo ni pamoja na kuwa wakweli hivyo tusiudanganye ulimwengu.

Kwa vilivyoorozeshwa vingi tunastahili kabisa kuongoza ila kwa Airport, beach destination na bodi yetu ya utalii bado tuko nyuma sana hivyo tuweni tu wawazi.

Ukiona nimepotosha ruksa kuuliza nikufafanulie vizuri.
 
Tuaendelea kupoteza vijana ambao ndio kesho yetu kisiasa, mpaka pale ambapo tutasafisha taratibu za kuendesha nyumba yetu, ikiwa pamoja na kwenda na muda.

Kama tutakuwa na lack of dynamism katika kuendesha chama tutapoteza sana mitaji. Na tujitahidi kuvumilia michango ya mawazo ambayo itaboresha chama.

Tusiwachukie wenye kutuonyesha mapungufu yetu na kama kweli yapo, kukataa kwetu kutatufanya tufikie tukose uwakilishi wa kutosha.
 
Yote ni mema kwa kila pande ila naimani muosha huoshwa.. alicho fanya CCM 2015 kwa upinzani ndicho kitakacho mrudia sina hakika ni lini ila muda utaoa majibu sahihi kama tutakuwa hai
 
Alikuwa anajipendekeza tu kwa Wajumbe, ccm yenyewe kaingia wiki wiki tu alafu anataka kujifanya anaijua sana, eti kaka piga goti

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…