Kama Gari lilishawahi kukuaibisha, Pita hata utupe experience yako

Kama Gari lilishawahi kukuaibisha, Pita hata utupe experience yako

Boss Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2022
Posts
458
Reaction score
991
Kama ndio itakuwa mara yako ya kwanza kuendesha Gari hasa hizi za Kijerumani usipokuwa makini zinakuaibisha wazi wazi, mimi binafsi haya magari yamenitoa nishai kiasi chake, matukio yangu ni kama haya yafuatayo

1. Siku ya kwanza kuendesha Polo sikujua mahali ya kufungulia fuel tank, (nilikuwa na mshkaji wangu nae hajui chochote) My friend tulizunguka hiyo gari karibu tutoe kiti.only to realise you need to just press the cap gently.

2. Niliwahi endesha gari na dim lights mwezi mzima, Kuna siku rafiki yangu nikampa aendeshe ilikuwa usiku akaweka full, nilijichukia sana siku hiyo

3. Siku nyingine tena (hizi zote ni German cars) nilikaribi kona nataka ku indicate asee!wacha wipers zifanye kazi yao, halafu nilikuwa na demu aliniuliza "kwani kunaanza kunyesha?" Nilizuga kumwambia Kuna mdudu nilikuwa namtoa kwa windshield

4. Kuna hizi Benz GL 350 nilitafuta gear stick nusu saa nzima napekua kila Mahali, uzuri nilikuwa mwenyewe na kilichonisaidi ni YouTube maana ningetia aibu kuanza kuuliza

Tujitahidi kuendesha haya magari ya Kijerumani tofauti tofauti ili tuwe na uzoefu nayo, Some of these machines can really embarrass a person.

Screenshot_20220609-130208.jpg
 
Wewe mtoa mada aibu zote za kishua shua.

Umewahi ishiwa wese unakufunua bonnet? Hafu unamuagiza boda akalete wese wakati we unajifanya unafix engine?

Na kuna siku nipo na pisi asubuhiiii enzi za foreni ya Ubungo Mataa (BF = Before Flyover) sasa ile I know my Car bwana gari ikazima wese. Sina ata mia mbovu. Nikamuomba pesa yake nikamdanganya asubuhi mafuta yanakua ya baridi inabidi tukanunue ya moto sheli.

Nishaenda na pisi Mkoa (Tanga) hafu pump ya maji ikafa ikabidi turudi na Tashriff gari tukaacha.

Nilijifanya najua kudrift roundabout ya Mlimani na Altezz nikakosea nikaingia kwenye mtaro wa pembeni kule nikaja tolewa ilinitoka kama laki 4 na aibu juu.

Yaani.
 
Ahahahh, umenikumbusha hiyo ya wese ilikuwa kitambo sana, ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuendesha Gari (Toyota Corona) tena nimefanya kuliiba Gari la Baba mdogo. Akiwa anaendesha mm huwa namsoma tu siunajua Automatic halina mambo mengi

Sasa kuna siku nikaliotea yeye alikuwa chumbani na mke wake na mvuq inanyesha siku hiyo, nikajua tu Hawa watakuwa wanafanya yao saa hizi, nilichofanya nikapita na funguo juu ya fridge uzuri parking ilikuwa mbali kdogo kiasi kwamba nikitekenya hawezi kusikia, Basi Mimi yuleee Hadi kwa washkaji siunajua tena kutaka sifa ,

Njiani nikipishana na gari natoka Nje ya Barabara kabisa, uzuri Barabara za tabora zilikuwa hazipo busy hivyo, Gari halina AC halafu nimepandosha vioo ili police wasinione maana nilikuwa mdogo sana,

Basi kumbe gari halina wese bana na Mimi sijui kumpandisha rafiki yangu anaangalia Dashboard ananiambia "hili gari litakuzimimikia muda wowote" nikamuuliza kwanini? Ananiambia we huoni mshale upo chini kabisa Yani umepita na E yenyewe. Yan mm sielewi chochote hapo, Nikamwambia funga mlango huo twenzetu siku hyo nilipanga kufanya tour ya marafiki zangu wote, kosa nililofanya tulipofika kwa rafiki yetu mwingine mm si nikazima Gari bhana (nimesema kosa coz jamaa alinambia eti kama nisingelizima basi tungesepa nalo fresh) Ngoma ikagoma kuwaka

Pesa ya mafuta ninayo Sasa, ilibidi nikope, (Nakumbuka hii pesa nilimrudishia jamaa baada ya mwaka, alinipa 5,000 nikampa 10,000) Basi nikapatiana kidumu kwa Daladala Baiskeli akatuletea wese fresh, shughuli ikaanzia hapo Sasa, Mabeshte zangu wananiambia nifungue fuel tank me nabaki kuwakodolea macho, dah walinishangaa sana, Rafiki yetu wapili tuliomfuata hapo ukiacha yule nilienda nae akanambia "Nina wasiwasi hili gari kama utalirudisha salama, kwanza siamini kama ni ww ndio ulikuwa unaendesha" amesema hivyo coz alishtukia tu gari limepakiwa Nje kwao, Sasa mm Nikawaambia basi nisaidieni kama mnajua kumbe nao patupu, tulitafutana kwenye Ile gari hakuna Mahali tuliacha kugusa, yule beshte yangu wa kwanza akapaotea sehemu. Akanambia Bora hata ulivyolizima maana hii aibu ingekutokea Petrol Station
 
Huu uzi umenifanya nikumbuke kituko kimoja 2015 au 2016

Ilikua hv
Kitambo hicho nilikua nakaa na mabro wawili kati ya hao mmoja alitangulia kuwa na gari ila huyu mwingine ambaye tulikua tunajazana ujinga hakua na gari.

Huyu bro miaka hiyo alijikuta ameingia kwenye mfereji wa hela bila kutegemea

Kwakuwa tulikua tunajazana ujinga mi nikamwambia bro saiv umekua mambo ya kutembelea pkpk sio mazuri inabd uvute gari (hapa nilijua hilo gari mm ndo ntakua mtumiaji mkuu)

Yule bro alikua hapindui kitu kwangu the next day tukaenda pale posta(ofisi nimeisahau), tulienda kuagiza gari.

Siku zikapita gari ikawasili bongo.

Nakumbuka hiyo siku nimekaa home sina hili wala lile bro akanitext na kunambia nitoke nje (ilikua suprise ya kunionesha gari).

Sasa kituko kilianzia hapa,

Nilivoingia kwenye gar tu bro akasema twende tukale hotel x leo, sasa mimi kwa kutaka sifa nikamwambia bro kwanini tusiwashe A/C wakat gar ni mpya, kumbe bwana siku nzima ameteseka kuiwasha A/C lakini iliishia kumletea joto tu kwenye gari (aliwasha steam).

Bas akanambia washa wewe hiyo A/C,. na mimi nikarudia kosa lile lile nikabonyeza kakitufe ka nchi zenye barid kali kwaajili ya kuzalisha joto.

Mbaya zaid tulikua tumefunga vioo tukisubiri kupoozwa lakin wapiiii tukaishia kulowana kwa majasho tu.

Hakuna siku tulihangaika kama ile.

Bahat nzuri tulivoenda hotel tukamkuta yule bro mwingne so mi nikamwambia ntabakia hapa kumbe nilikua nakimbia lile joto maana tulijua labda A/C mbovu kumbe sisi wenyewe ndo tumechapia
 
Miaka kadhaa bado sijajua kuendesha gari. Demu katoroka kazini kanifuata maskani na Chuma enzi ndiyo zinaingia Nissan TEANA akasema kachoka mimi nimsaidie kuendesha nikazuga nimesahau leseni yangu na staki uchokozi na traffic. Akaelewa.

Siku ya pili Akaja nalo tena gheto Tukafanya yetu sasa Tumetoka ghetto chuma kipo nje demu kachoka akanipa ufunguo niendeshe, nikashindwa kuchomoa basi kidume nikaaa kwenye usukani huku natetemeka. Kila nikiwasha Inagoma , kila nikiwasha hola. Chuma inagoma kuwaka.

Demu kushtuka kumbe gari gia ipo kwenye Driving badala ya Parking. Aseee pale niliumbuka maana alijua kabisa nilikuwa Ngumbaru.
 
Siku ya kwanza kuendesha push to start key nilitumia nusu saa nzima kupiga start.
Kuuliza naona jau nikasema ngoja nikomae tu. Mpaka nikagundua natakiwa nikanyage brake pedal ndio gari inawaka nilisha sweat.
Mbaya zaidi sikuwa peke yangu kwenye gari. Aibu hii.
 
Ila huu ujuaji, mwaka 2008

Nilikua nimezoea gari za manual zile ambazo gear level ipo katikati, siku hiyo tupo kanisani maeneo ya tabata ikatokea emergency kumuwahisha mtumishi maeneo ya kinyerezi akafanye ibada huko pia, sasa mshirika mmoja akatoa gari, huku na dereva wa haraka ni mimi, bwana ee kumbe gari ni staff gear [emoji23][emoji23][emoji23], hand brake yake yenyewe ndo ile ya kuvuta ipo pembeni ya uskani, ilibidi jamaa aje anisaidie kutoa ( aibu nilipata mimi), uzuri muda huo mtumishi na watu wengine walikua pembeni kidogo ,

Haya safari ianze, sijui moja ikwapi maana gear level ilikua imefutika, badala ya kuweka moja mi naweka tano, mara gari izime, kujitahidi huku na kule nikaotea namba moja, nimekaribia kufika getini, naangalia kwenye side mirror naona mtu anatukimbilia kumbe ni mwenye gari alijua hapa mtumishi ataingizwa mtaroni, ikabidi jamaa aje achukue gari awapeleke, tangu siku hiyo nikawa mnyonge na aibu tele, lakini nilifanikiwa kuzoea staff gear, ni nzuri sana sema ukute bado ni nzima
 
nilipewa funguo nikafungue mlango nikashindwa,aibu ya kwanza, kufunga seat belt sikujua inapitia wapi na kutokea wapi muda huo dereva ananichora tu aibu ya pili

mwisho ya yote akatabasamu tukaendelea na safari niliabika sana

Nusu safari siongei ,nikimuangalia dereva anatabasamu ndipo na mimi nakausha zaidi
 
Nilipewa Toyota Probox niisogeze kuprove kuwa naweza kuendesha manual.

Hakuna kitu nilifanya zaidi ya kuwasha, kutia gear na kuizima wakati nataka iondoke.

Kilichofuata nikashuka na kukabidhi ufunguo kwa aibu. Wakaja wadau wengine watatu wakachemka. Ila tukaja kubain kuwa clutch pedal ipo chini sana kubalance na acceleration pedal.

Yaani ukiwa unaachia clutch huku unabalance mafuta utaona gari haiendi na inaanza kutoa mlio wa kutaka kuzima.

Nikasema duh afadhali maana nikahisi pengine mimi gari manuals siziwezi pengine.
 
Huu uzi umenifanya nikumbuke kituko kimoja 2015 au 2016

Ilikua hv
Kitambo hicho nilikua nakaa na mabro wawili kati ya hao mmoja alitangulia kuwa na gari ila huyu mwingine ambaye tulikua tunajazana ujinga hakua na gari.

Huyu bro miaka hiyo alijikuta ameingia kwenye mfereji wa hela bila kutegemea

Kwakuwa tulikua tunajazana ujinga mi nikamwambia bro saiv umekua mambo ya kutembelea pkpk sio mazuri inabd uvute gari (hapa nilijua hilo gari mm ndo ntakua mtumiaji mkuu)

Yule bro alikua hapindui kitu kwangu the next day tukaenda pale posta(ofisi nimeisahau), tulienda kuagiza gari.

Siku zikapita gari ikawasili bongo.

Nakumbuka hiyo siku nimekaa home sina hili wala lile bro akanitext na kunambia nitoke nje (ilikua suprise ya kunionesha gari).

Sasa kituko kilianzia hapa,

Nilivoingia kwenye gar tu bro akasema twende tukale hotel x leo, sasa mimi kwa kutaka sifa nikamwambia bro kwanini tusiwashe A/C wakat gar ni mpya, kumbe bwana siku nzima ameteseka kuiwasha A/C lakini iliishia kumletea joto tu kwenye gari (aliwasha steam).

Bas akanambia washa wewe hiyo A/C,. na mimi nikarudia kosa lile lile nikabonyeza kakitufe ka nchi zenye barid kali kwaajili ya kuzalisha joto.

Mbaya zaid tulikua tumefunga vioo tukisubiri kupoozwa lakin wapiiii tukaishia kulowana kwa majasho tu.

Hakuna siku tulihangaika kama ile.

Bahat nzuri tulivoenda hotel tukamkuta yule bro mwingne so mi nikamwambia ntabakia hapa kumbe nilikua nakimbia lile joto maana tulijua labda A/C mbovu kumbe sisi wenyewe ndo tumechapia
Sasa mlitembelea Gari likiwa na High temperature kwa muda gani[emoji23] au nani aliwafundisha maujuzi ya kucheza na Air Co
 
Ila huu ujuaji, mwaka 2008

Nilikua nimezoea gari za manual zile ambazo gear level ipo katikati, siku hiyo tupo kanisani maeneo ya tabata ikatokea emergency kumuwahisha mtumishi maeneo ya kinyerezi akafanye ibada huko pia, sasa mshirika mmoja akatoa gari, huku na dereva wa haraka ni mimi, bwana ee kumbe gari ni staff gear [emoji23][emoji23][emoji23], hand brake yake yenyewe ndo ile ya kuvuta ipo pembeni ya uskani, ilibidi jamaa aje anisaidie kutoa ( aibu nilipata mimi), uzuri muda huo mtumishi na watu wengine walikua pembeni kidogo ,

Haya safari ianze, sijui moja ikwapi maana gear level ilikua imefutika, badala ya kuweka moja mi naweka tano, mara gari izime, kujitahidi huku na kule nikaotea namba moja, nimekaribia kufika getini, naangalia kwenye side mirror naona mtu anatukimbilia kumbe ni mwenye gari alijua hapa mtumishi ataingizwa mtaroni, ikabidi jamaa aje achukue gari awapeleke, tangu siku hiyo nikawa mnyonge na aibu tele, lakini nilifanikiwa kuzoea staff gear, ni nzuri sana sema ukute bado ni nzima
Hii ya kwako tena kwa miaka hyo hata mm ningefeli tu
 
Siku ya kwanza kuendesha push to start key nilitumia nusu saa nzima kupiga start.
Kuuliza naona jau nikasema ngoja nikomae tu. Mpaka nikagundua natakiwa nikanyage brake pedal ndio gari inawaka nilisha sweat.
Mbaya zaidi sikuwa peke yangu kwenye gari. Aibu hii.
Huyu ni mimi kabisa... Dem wa broo kaja na dogo lake wako na ndinga lao ni age mate wangu..

Nikaagizwa buchani... parking ilikua ndogo gari ya shemeji imeblock kutoa gari ya broo kwa mbele..shemeji akasema niende tu gari yake direct.. broo akachomekea na shemeji mdogo anisindikize "alikua pisi 😀😀"

1-Tumepanda na shemeji mdogo naanza kutafta sehemu ya funguo kwene dashboard sioni "akaniambi una press hapohapo tu "
2-Na press haiwaki 😃😀 "akaniambia kanyaga brake kwanza "
Asee nlimbuka.. nlikia nimezoea li mark II la braza.

Ya pili - nliba gari ya uncle nkaenda kuoshea kwa demu angu nikakuta ndo anawasindikiza mashosti zake wapande daladala kidume nkasema pandeni niwapeleke
wese likakatikia njiani sina ata kumi "shosti ake mmoja akanipa 10,000 mbiombio sheli na kidumu hii ndo ilikua aibu kubwa kuliko"
 
Huyu ni mimi kabisa... Dem wa broo kaja na dogo lake wako na ndinga lao ni age mate wangu..

Nikaagizwa buchani... parking ilikua ndogo gari ya shemeji imeblock kutoa gari ya broo kwa mbele..shemeji akasema niende tu gari yake direct.. broo akachomekea na shemeji mdogo anisindikize "alikua pisi [emoji3][emoji3]"

1-Tumepanda na shemeji mdogo naanza kutafta sehemu ya funguo kwene dashboard sioni "akaniambi una press hapohapo tu "
2-Na press haiwaki [emoji2][emoji3] "akaniambia kanyaga brake kwanza "
Asee nlimbuka.. nlikia nimezoea li mark II la braza.

Ya pili - nliba gari ya uncle nkaenda kuoshea kwa demu angu nikakuta ndo anawasindikiza mashosti zake wapande daladala kidume nkasema pandeni niwapeleke
wese likakatikia njiani sina ata kumi "shosti ake mmoja akanipa 10,000 mbiombio sheli na kidumu hii ndo ilikua aibu kubwa kuliko"

Iyo wese kuisha nmecheka sanaaa[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom