Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Niliwapakia wakwe niwawahishe Ubungo terminal saa 11:00 alfajiri, kumbe battery imekauka chaji, mvua inanyesha, fanya nifanyalo haikuwezekana gari halikuwezekana kuwaka, nikamwambia mama mkwe naomba nikuelekeze cha kufanya ili mimi na baba mkwe tusukume yeye alishtue... Baba mkwe akang'aka akasema yeye na mama mkwe wanashuka kusukuma mimi nishtue ...ndiyo ikawa pona yetu