Kama Gari lilishawahi kukuaibisha, Pita hata utupe experience yako

Kama Gari lilishawahi kukuaibisha, Pita hata utupe experience yako

Ahahahh, umenikumbusha hiyo ya wese ilikuwa kitambo sana, ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuendesha Gari (Toyota Corona) tena nimefanya kuliiba Gari la Baba mdogo. Akiwa anaendesha mm huwa namsoma tu siunajua Automatic halina mambo mengi

Sasa kuna siku nikaliotea yeye alikuwa chumbani na mke wake na mvuq inanyesha siku hiyo, nikajua tu Hawa watakuwa wanafanya yao saa hizi, nilichofanya nikapita na funguo juu ya fridge uzuri parking ilikuwa mbali kdogo kiasi kwamba nikitekenya hawezi kusikia, Basi Mimi yuleee Hadi kwa washkaji siunajua tena kutaka sifa ,

Njiani nikipishana na gari natoka Nje ya Barabara kabisa, uzuri Barabara za tabora zilikuwa hazipo busy hivyo, Gari halina AC halafu nimepandosha vioo ili police wasinione maana nilikuwa mdogo sana,

Basi kumbe gari halina wese bana na Mimi sijui kumpandisha rafiki yangu anaangalia Dashboard ananiambia "hili gari litakuzimimikia muda wowote" nikamuuliza kwanini? Ananiambia we huoni mshale upo chini kabisa Yani umepita na E yenyewe. Yan mm sielewi chochote hapo, Nikamwambia funga mlango huo twenzetu siku hyo nilipanga kufanya tour ya marafiki zangu wote, kosa nililofanya tulipofika kwa rafiki yetu mwingine mm si nikazima Gari bhana (nimesema kosa coz jamaa alinambia eti kama nisingelizima basi tungesepa nalo fresh) Ngoma ikagoma kuwaka

Pesa ya mafuta ninayo Sasa, ilibidi nikope, (Nakumbuka hii pesa nilimrudishia jamaa baada ya mwaka, alinipa 5,000 nikampa 10,000) Basi nikapatiana kidumu kwa Daladala Baiskeli akatuletea wese fresh, shughuli ikaanzia hapo Sasa, Mabeshte zangu wananiambia nifungue fuel tank me nabaki kuwakodolea macho, dah walinishangaa sana, Rafiki yetu wapili tuliomfuata hapo ukiacha yule nilienda nae akanambia "Nina wasiwasi hili gari kama utalirudisha salama, kwanza siamini kama ni ww ndio ulikuwa unaendesha" amesema hivyo coz alishtukia tu gari limepakiwa Nje kwao, Sasa mm Nikawaambia basi nisaidieni kama mnajua kumbe nao patupu, tulitafutana kwenye Ile gari hakuna Mahali tuliacha kugusa, yule beshte yangu wa kwanza akapaotea sehemu. Akanambia Bora hata ulivyolizima maana hii aibu ingekutokea Petrol Station
Ikawaje ulivorud kwa baba mdogo
 
Kama ndio itakuwa mara yako ya kwanza kuendesha Gari hasa hizi za Kijerumani usipokuwa makini zinakuaibisha wazi wazi, mimi binafsi haya magari yamenitoa nishai kiasi chake, matukio yangu ni kama haya yafuatayo

1. Siku ya kwanza kuendesha Polo sikujua mahali ya kufungulia fuel tank, (nilikuwa na mshkaji wangu nae hajui chochote) My friend tulizunguka hiyo gari karibu tutoe kiti.only to realise you need to just press the cap gently.

2. Niliwahi endesha gari na dim lights mwezi mzima, Kuna siku rafiki yangu nikampa aendeshe ilikuwa usiku akaweka full, nilijichukia sana siku hiyo

3. Siku nyingine tena (hizi zote ni German cars) nilikaribi kona nataka ku indicate asee!wacha wipers zifanye kazi yao, halafu nilikuwa na demu aliniuliza "kwani kunaanza kunyesha?" Nilizuga kumwambia Kuna mdudu nilikuwa namtoa kwa windshield

4. Kuna hizi Benz GL 350 nilitafuta gear stick nusu saa nzima napekua kila Mahali, uzuri nilikuwa mwenyewe na kilichonisaidi ni YouTube maana ningetia aibu kuanza kuuliza

Tujitahidi kuendesha haya magari ya Kijerumani tofauti tofauti ili tuwe na uzoefu nayo, Some of these machines can really embarrass a person.

View attachment 2255218
Hayo ni ya kuazima?
Sidhani kama utanunua gari usipende kujua moja mbili tatu kabla gujaanza endesha
 
Mwanzo wa kuendesha gari, ilikuwa mshua mkubwa akitoka job mm nashika maji naiosha sasa siku hiyo akanijaribu, "unajua kuendesha gari"? Nikajibu ndiyo...

Akanipatia niende kukagua n'gombe (kuna umbali kidogo kutoka home)..

Ile nimechomeka funguo na kuiwasha kisha kuweka "D" ili niondoke naona gari ina-force kuondoka ila inatitia chini, kanyaga mafuta gari inaita tu ila kuondoka bila bila, mzee nikan'gan'gana ili iondoke lakini wapi......

Mara paap,! Mshua katoka ndani na kupiga kelele (maana eneo lote kulikuwa kumejaa moshi wa zile vurumahi).....

"Wewe gari ipo kwenye handbrake"....aiseeeeeee.!
 
Somo hapa kama umepewa gari hujawahi kuiendesha au muundo wake tofauti na gari ulizozizoea, chukua dakika 5 kuangalia vitu vyo msingi ikiwezekana zama youtube, mengine usione noma kuuliza hata gear zinaingizwaje kama ni manual maana principle za uendeshaji ni zilezile wakati mwingine uingizaji gear hutofautiana (hapo umepewa staff gear).

Hizi issue za kutafuta sehemu za kufungulia mfuniko wa mafuta au kulaza kitu au kuwasha taa za ziada za mbele na kuongeza mwanga wa ziada huwa ni majanga unapopewa gari alafu ulizoea gari za mfumo wa zamani ambazo zipo nyingi
 
Ila huu ujuaji, mwaka 2008

Nilikua nimezoea gari za manual zile ambazo gear level ipo katikati, siku hiyo tupo kanisani maeneo ya tabata ikatokea emergency kumuwahisha mtumishi maeneo ya kinyerezi akafanye ibada huko pia, sasa mshirika mmoja akatoa gari, huku na dereva wa haraka ni mimi, bwana ee kumbe gari ni staff gear [emoji23][emoji23][emoji23], hand brake yake yenyewe ndo ile ya kuvuta ipo pembeni ya uskani, ilibidi jamaa aje anisaidie kutoa ( aibu nilipata mimi), uzuri muda huo mtumishi na watu wengine walikua pembeni kidogo ,

Haya safari ianze, sijui moja ikwapi maana gear level ilikua imefutika, badala ya kuweka moja mi naweka tano, mara gari izime, kujitahidi huku na kule nikaotea namba moja, nimekaribia kufika getini, naangalia kwenye side mirror naona mtu anatukimbilia kumbe ni mwenye gari alijua hapa mtumishi ataingizwa mtaroni, ikabidi jamaa aje achukue gari awapeleke, tangu siku hiyo nikawa mnyonge na aibu tele, lakini nilifanikiwa kuzoea staff gear, ni nzuri sana sema ukute bado ni nzima
Hivi hizi manual staff gears patterns zake zimekaaje??? Natamani sana nizijue...
 
Tairi iliniumbua pabaya Sana enzi hizo nipo kidato cha tatu,mshua alikua gari yake haitumii sana ,inakaa nyumbani muda mwingi kwa kua alikua akitumia ya ofisini.siku hiyo nikasema ngoja nile misele kidogo,nikaoshee kwa manzi wangu,baada ya apo nipitie kwa washikaji,Rav 4 old model nikafika nayo fresh,nikapiga story kidogo na manzi nikasepa .nikiwa njiani kuelekea kwa washikaji mara ghafla puuuh pacha hiyoo...kubadili tayari siwezi,gari nimeibaa,kijasho kinanitoka na kiherehere changu,nikasema apa sisimamii naunga mpaka home.njia nzima gari makelele tu khokhooooo,kila mtu anashangaa uyu chizi nini,nikawahi faster,nikalipark,nikaingiza msumari kidogo kwenye tairi ,mshua akija akute ilikua Ina slow pancha.nikabaki najuta Sana n kuomba Mungu mshua asisanuke,na kweli ilo nalo likapita,kwa muda nikaigopa hiyo gari Kama ukoma.
 
Tairi iliniumbua pabaya Sana enzi hizo nipo kidato cha tatu,mshua alikua gari yake haitumii sana ,inakaa nyumbani muda mwingi kwa kua alikua akitumia ya ofisini.siku hiyo nikasema ngoja nile misele kidogo,nikaoshee kwa manzi wangu,baada ya apo nipitie kwa washikaji,Rav 4 old model nikafika nayo fresh,nikapiga story kidogo na manzi nikasepa .nikiwa njiani kuelekea kwa washikaji mara ghafla puuuh pacha hiyoo...kubadili tayari siwezi,gari nimeibaa,kijasho kinanitoka na kiherehere changu,nikasema apa sisimamii naunga mpaka home.njia nzima gari makelele tu khokhooooo,kila mtu anashangaa uyu chizi nini,nikawahi faster,nikalipark,nikaingiza msumari kidogo kwenye tairi ,mshua akija akute ilikua Ina slow pancha.nikabaki najuta Sana n kuomba Mungu mshua asisanuke,na kweli ilo nalo likapita,kwa muda nikaigopa hiyo gari Kama ukoma.
Hahahaaaa noma sana..
 
First time naendesha Crown royal salon aisee niliazima kwa jamaa yangu mda kidogo.Niende nje ya mji akaniambia nitie tu wese alinipa tayari Lina kawese so nikaenda kuongezea..

Mbele kidogo kufika mahali nilipo kuwa naenda muda wa kurudi Sasa niwashe nirudi zangu weka Ile smart key nikipush start kitu hakiwaki nikampigia jamaa simu.akaniambia..

Nicheki labda wese Hamna nikaagiza 5ltrs Ili nifike road kuu..
Maana nilipokuwepo na barabara kuu 20km nikaweka lile ..
Wese haiwaki! Ikabidi nimpigie Tena mshkaji akaniambia
Nicheki Ile smart key kama nimeweka sawa[emoji1] kumbe...
Nilikuwa nimeigeuza kuweka nikatekenya kitu kimewaka[emoji16][emoji23]

Nilijiona mshamba kinoma siku Ile bahati nzuri na niliokuwa
Nao pale hawakuelewa kwanini iligoma kustart.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Huyu ni mimi kabisa... Dem wa broo kaja na dogo lake wako na ndinga lao ni age mate wangu..

Nikaagizwa buchani... parking ilikua ndogo gari ya shemeji imeblock kutoa gari ya broo kwa mbele..shemeji akasema niende tu gari yake direct.. broo akachomekea na shemeji mdogo anisindikize "alikua pisi [emoji3][emoji3]"

1-Tumepanda na shemeji mdogo naanza kutafta sehemu ya funguo kwene dashboard sioni "akaniambi una press hapohapo tu "
2-Na press haiwaki [emoji2][emoji3] "akaniambia kanyaga brake kwanza "
Asee nlimbuka.. nlikia nimezoea li mark II la braza.


Ya pili - nliba gari ya uncle nkaenda kuoshea kwa demu angu nikakuta ndo anawasindikiza mashosti zake wapande daladala kidume nkasema pandeni niwapeleke
wese likakatikia njiani sina ata kumi "shosti ake mmoja akanipa 10,000 mbiombio sheli na kidumu hii ndo ilikua aibu kubwa kuliko"
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu uzi inaonesha vijana wengi wameanza kujua kuendesha gari wangali wadogo tena kwa kuibia ibia sana watu wanavizia baba kalala dogo anaiba gari anaenda kutambia masela, mjomba sijui kalisahau parking kaenda kazini kwa miguu, n.k... Yote ikichangiwa na UJUAJI wa kutaka kujua jambo hata mtu kama hajui au anaona tu anataka kujihakikishia..

Kifupi ukikaa na ndugu/mzazi ana gari na ukaacha kujua gari wewe ni wa kupgwa KELBU ya kichwa..
 
Huu uzi inaonesha vijana wengi wameanza kujua kuendesha gari wangali wadogo tena kwa kuibia ibia sana watu wanavizia baba kalala dogo anaiba gari anaenda kutambia masela, mjomba sijui kalisahau parking kaenda kazini kwa miguu, n.k... Yote ikichangiwa na UJUAJI wa kutaka kujua jambo hata mtu kama hajui au anaona tu anataka kujihakikishia..

Kifupi ukikaa na ndugu/mzazi ana gari na ukaacha kujua gari wewe ni wa kupgwa KELBU ya kichwa..
Hii ndio ilikua tabia yangu ya kuiba gari na kula misele tena nikawa na advantage ya kuendesha mara kwa mara kwa sababu nyumbani hamna uzio so gari tukawa tunapeleka kulaza zile sehemu wanapolaza magari na mm ndo nikawa nalilaza usiku nalitoa asubuhi,

kuna siku siku niliiba nikaenda kula misele duh nilipata majanga sana
 
Kipindi hichoooo! RVR kitchen_party natoka mitaa ya nyumbani, kuingia barabarani hapohapo kwnye junction kuna kituo cha daladala[emoji23][emoji23] asubuhi kila mtu ana wahi na kipindi hicho sio kama sasa daladala ni nyingi, kulikua na gari chache sasa kipande cha morogoro road kila kituo ni mtiti wa raia, hivyo ilikua kila ukifika kituoni unazoa majirani kadhaa lift unaenda nao town, sasa kabla sijaingia mainroad nikawachukua kabisa watu kadhaa nikaanza kuondoka, nikaingia main road vzr nafika size ya kituo na mtiti ule wa watu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] la'haullaah nilisikia kishindo kama cha bomu na baada ya sekunde kama mbili nikawa nasikia sauti ya makorokocho ya vyuma vinavyo pandiana kwa fujo[emoji16][emoji16][emoji1782] nikawahi kona kali kabla mwendo haujawa zero nikaingia kituoni, kushuka kukagua, nikabaini diff nyuma ndio imesha changanya vyuma [emoji2959][emoji2959][emoji2959] kabisa, wale walio panda wakapiga chini habari ikaishia hapo huku jasho likinitoka! Magari haya mazuri yakiwa yanatembea ila c liamue kukuletea ushenzi wake
 
Back
Top Bottom