Kama Gari lilishawahi kukuaibisha, Pita hata utupe experience yako

Ikawaje ulivorud kwa baba mdogo
 
Hayo ni ya kuazima?
Sidhani kama utanunua gari usipende kujua moja mbili tatu kabla gujaanza endesha
 
Mwanzo wa kuendesha gari, ilikuwa mshua mkubwa akitoka job mm nashika maji naiosha sasa siku hiyo akanijaribu, "unajua kuendesha gari"? Nikajibu ndiyo...

Akanipatia niende kukagua n'gombe (kuna umbali kidogo kutoka home)..

Ile nimechomeka funguo na kuiwasha kisha kuweka "D" ili niondoke naona gari ina-force kuondoka ila inatitia chini, kanyaga mafuta gari inaita tu ila kuondoka bila bila, mzee nikan'gan'gana ili iondoke lakini wapi......

Mara paap,! Mshua katoka ndani na kupiga kelele (maana eneo lote kulikuwa kumejaa moshi wa zile vurumahi).....

"Wewe gari ipo kwenye handbrake"....aiseeeeeee.!
 
Somo hapa kama umepewa gari hujawahi kuiendesha au muundo wake tofauti na gari ulizozizoea, chukua dakika 5 kuangalia vitu vyo msingi ikiwezekana zama youtube, mengine usione noma kuuliza hata gear zinaingizwaje kama ni manual maana principle za uendeshaji ni zilezile wakati mwingine uingizaji gear hutofautiana (hapo umepewa staff gear).

Hizi issue za kutafuta sehemu za kufungulia mfuniko wa mafuta au kulaza kitu au kuwasha taa za ziada za mbele na kuongeza mwanga wa ziada huwa ni majanga unapopewa gari alafu ulizoea gari za mfumo wa zamani ambazo zipo nyingi
 
Hivi hizi manual staff gears patterns zake zimekaaje??? Natamani sana nizijue...
 
Tairi iliniumbua pabaya Sana enzi hizo nipo kidato cha tatu,mshua alikua gari yake haitumii sana ,inakaa nyumbani muda mwingi kwa kua alikua akitumia ya ofisini.siku hiyo nikasema ngoja nile misele kidogo,nikaoshee kwa manzi wangu,baada ya apo nipitie kwa washikaji,Rav 4 old model nikafika nayo fresh,nikapiga story kidogo na manzi nikasepa .nikiwa njiani kuelekea kwa washikaji mara ghafla puuuh pacha hiyoo...kubadili tayari siwezi,gari nimeibaa,kijasho kinanitoka na kiherehere changu,nikasema apa sisimamii naunga mpaka home.njia nzima gari makelele tu khokhooooo,kila mtu anashangaa uyu chizi nini,nikawahi faster,nikalipark,nikaingiza msumari kidogo kwenye tairi ,mshua akija akute ilikua Ina slow pancha.nikabaki najuta Sana n kuomba Mungu mshua asisanuke,na kweli ilo nalo likapita,kwa muda nikaigopa hiyo gari Kama ukoma.
 
Hahahaaaa noma sana..
 
First time naendesha Crown royal salon aisee niliazima kwa jamaa yangu mda kidogo.Niende nje ya mji akaniambia nitie tu wese alinipa tayari Lina kawese so nikaenda kuongezea..

Mbele kidogo kufika mahali nilipo kuwa naenda muda wa kurudi Sasa niwashe nirudi zangu weka Ile smart key nikipush start kitu hakiwaki nikampigia jamaa simu.akaniambia..

Nicheki labda wese Hamna nikaagiza 5ltrs Ili nifike road kuu..
Maana nilipokuwepo na barabara kuu 20km nikaweka lile ..
Wese haiwaki! Ikabidi nimpigie Tena mshkaji akaniambia
Nicheki Ile smart key kama nimeweka sawa[emoji1] kumbe...
Nilikuwa nimeigeuza kuweka nikatekenya kitu kimewaka[emoji16][emoji23]

Nilijiona mshamba kinoma siku Ile bahati nzuri na niliokuwa
Nao pale hawakuelewa kwanini iligoma kustart.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu uzi inaonesha vijana wengi wameanza kujua kuendesha gari wangali wadogo tena kwa kuibia ibia sana watu wanavizia baba kalala dogo anaiba gari anaenda kutambia masela, mjomba sijui kalisahau parking kaenda kazini kwa miguu, n.k... Yote ikichangiwa na UJUAJI wa kutaka kujua jambo hata mtu kama hajui au anaona tu anataka kujihakikishia..

Kifupi ukikaa na ndugu/mzazi ana gari na ukaacha kujua gari wewe ni wa kupgwa KELBU ya kichwa..
 
Hii ndio ilikua tabia yangu ya kuiba gari na kula misele tena nikawa na advantage ya kuendesha mara kwa mara kwa sababu nyumbani hamna uzio so gari tukawa tunapeleka kulaza zile sehemu wanapolaza magari na mm ndo nikawa nalilaza usiku nalitoa asubuhi,

kuna siku siku niliiba nikaenda kula misele duh nilipata majanga sana
 
Kipindi hichoooo! RVR kitchen_party natoka mitaa ya nyumbani, kuingia barabarani hapohapo kwnye junction kuna kituo cha daladala[emoji23][emoji23] asubuhi kila mtu ana wahi na kipindi hicho sio kama sasa daladala ni nyingi, kulikua na gari chache sasa kipande cha morogoro road kila kituo ni mtiti wa raia, hivyo ilikua kila ukifika kituoni unazoa majirani kadhaa lift unaenda nao town, sasa kabla sijaingia mainroad nikawachukua kabisa watu kadhaa nikaanza kuondoka, nikaingia main road vzr nafika size ya kituo na mtiti ule wa watu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] la'haullaah nilisikia kishindo kama cha bomu na baada ya sekunde kama mbili nikawa nasikia sauti ya makorokocho ya vyuma vinavyo pandiana kwa fujo[emoji16][emoji16][emoji1782] nikawahi kona kali kabla mwendo haujawa zero nikaingia kituoni, kushuka kukagua, nikabaini diff nyuma ndio imesha changanya vyuma [emoji2959][emoji2959][emoji2959] kabisa, wale walio panda wakapiga chini habari ikaishia hapo huku jasho likinitoka! Magari haya mazuri yakiwa yanatembea ila c liamue kukuletea ushenzi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…