Kama Gari lilishawahi kukuaibisha, Pita hata utupe experience yako

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wesee. Mzee unatoka na chuma alafu hubebi akiba
 
Mimi sijawahi kuaibika maana napendaga sana kuuliza na kusoma kama kitu sikijui ila Mara yangu ya kwanza kuendesha gari ile feeling sijawahi isahau kamwe.

Ilikua hivi siku hiyo nipo room bro akanipigia simu nimsindikize kwa jamaa ake anaumwa hivyo atanipitia ndani ya muda mfupi ilikua majira ya saa 10 jioni.Basi punde mwamba huyu kaja na Chervelolet zile kama Suzuki tukapanda tukafika sehemu inaitwa kiguza tukaacha lami then tukaingia ndani kutoka road hadi kwa jamaa alipojenga barabara ya vumbi ni kama KM 10+ ,sasa kabla hatuja ingia ndani tulisimama akanunua vocha ndo akaniuliza vipi umewahi kuendesha gari? hapo nilikua niko first year ikamwambia hapana akasema njoo ukae huku nikufundishe kweli nikahamia upande wa dereva basi bwana akanipa maelekezo kanyaga breki then weka D kisha achi breki dude hilo likaanza kuserereka mdogomdogo huku ananipa maelekezo.

Tukafika kwa jamaa tukapiga stori hadi saa 1 usiku inaelekea saa 2 tukaondoka basi akasema tutaenda hadi home na kwanza hakuamini kama ile ilikua mara yangu ya kwanza kuendesha jinsi nilivyokua nimetulia..nikaendesha hadi road nikamwambia achukue akasema hapa wewe twende tu mdogomdogo basi hao tunaenda njiani taa zikinipiga yeye ananipunguzia na kuongeza maana mimi sijui hata jinsi ya kuongeza na kupunguza,,tukafika pale mathew kulikua na carry ananyata basi si nikaovertake dah alishoot oya acha ujinga tutakufa maana nilitoka kama ngiri ila alhamdulillah niliovertake fresh sasa tukafika hadi mtaani.

Kituko sasa ni hiki ile gari sehemu inapotakiwa kulala ni kama KM 1 kwenda home ila sikuridhika nikata kufika hadi home wanione naendesha gari [emoji16][emoji16] nikafika nikashuka nikaacha mlango wa dereva wazi ili wajue mimi ndo jilikua naendeaha nikaingia ndani nikachukua chaja watu wananicheli huyo nikaingia tena nikageuza nikaenda kulaza bro anacheka tu,akaniachia funguo kesho mapema nimsogezee gereji basi walahy sikulala nikatamani pakuche.Saa 12 huyo nikaenda kuiosha hadi gereji ,baada ya hapo nikawa kichaa na magari kila wikiend naweka hela namfuata natia wese niendeshe then nikajifunza manual kupitia hiace 3L na 2L.
 
I feel you bro hiyo kitu noma sana

Nilikua najua kuendesha gari tangu nikiwa form one lakini kwenye vumbi tu sikuwahi kuendesha kwenye lami sasa siku moja tumetoka na mzee tumeenda kusalimia kwa aunt

Muda wa kuondoka nikamwambia mzee niachie niendeshe hapa kwenye vumbi tukifika kwenye lami nakupa akaniachia nikasogeza chuma mpaka sehemu ya kuingia njia ya lami nikasimama nimpishe nashangaa ananiambia we twende tu

Nikaingiza chuma kwenye lami dah ilikua experience nzuri sana...kwenye lami unateleza tu shwaaaaa maana nilishazoea kuendesha njia ya vumbi nginja nginja kibao hata hupati ladha ya gari


Tumeenda mbelee kidogo kuna restaurant akaniambia Ingia hapo kwanza tupige msosi mwanaume nikawasha indicating light nikaingia kushoto tukashuka tukala

Muda wa kutoka naona akaniachia tena nikakamata lami aah ni kuteleza tu nikaona maisha ndo nishayapatia hapa duniani[emoji28]
 
Uko sahihi, siyo dhambi kutofahamu kitu...
Pia usipofahamu ni vyema ukauliza, ukijifanya mjuaji utaumia....
Fedheha inauma kweli na huu uzi umenifanya nicheke kweli, lakini huwezi kufa....
 

Staff gear Noma sana hasa ukute umeshazoea floor gear
 

Enzi hizo niko primary
Mzee alikuwa ana vi carina kadhaa
Sasa nkavizia home mzee kaenda church ikabaki 1 home ile naangalia huku na kule nmebaki pekeangu funguo ipo mezani nkasema isiwe taabu acha niende kwa wanangu niwape hi..nmeingia fresh nkawasha chuma uyoo kufika barabarani kumbe side mirror zimekunjwa naitafuta lock ya kuzikunjua siioni ebwaanaaa[emoji23][emoji23][emoji23]

Nlitembea kwa kutumia kioo cha ndani huku nageuka nyuma.nlifika mwanangu mmoja ndo akanionesha jinsi ya kuzikunjua daaah sitasahau[emoji28]
 
Mwaka 2012 nimeiba gari home nimeenda kumchukua manzi yangu sehemu.Nikadrive kwa mikogo hadi sehemu flani nje ya mji, nikapark tukawa tunapiga story kwenye gari mara tupigane vibusu-busu tushikane hapa na pale. Huku gari nimeweka switch-on nimewasha redio tunasikiliza miziki romantic hivi. Mara kigiza kikaanza kuingia gari ikazima ghafla, nataka niwashe gari nimuwahishe manzi kwao, gari kagoma,piga start gari hata haiitiki.Pambana na tochi ya gari fungua bonnet hapa na pale kitu kinagoma.

Nikaanza kusweat kijasho chembamba, mara paap simu tunayotumia kama tochi ikakata charge, nilidata. Bahati nzuri ikapita gari ya tanesco.Washkaji wakanitukana kichizi then wakaniboost nikasepa. Ila bimetoka hapo hata manzi sina hamu nae kabisa
 
Ulikuaa na betri kimeo
 
Yaani hili la kukanyaga brake ndo uwashe gari ni hatari sana.
Kuna jamaangu yeye alinunua gari wayback sijui ni forester nini(sio mtaalamu wa magari) ila ile gari ni push to start.

Sasa tumekutana maeneo akanambia twenzetu tukale nyama sehemu alikuwa na pisi mbili watoto JJ mkunda , me sikuwa najua kuendesha gari jamaa akanambia chukua funguo mzee twenzetu. Nilishindwa kukataa sababu kuna ile washikaji zako huwa wanakuaminia unajua vingi.

Kufika chuma imetulia ndani button naiona ila kila nkibonyeza mzigo hauwaki, mwana akakanyaga brake akapush ikawaka, nilimwambia hizi chuma mimi sizijui tusijeenda pitia miti.

Mshikaji alicheka sana kwanza hakuamini kama sijui kuendesha gari na zile pisi zilicheka balaa ila mmoja akasema hata yeye amejua kuendesha gari miezi michache iliyopita so sio big issue kabisa.
Tumeenda kwenye nyama mzuka wote umeisha yanii nilipoa kinoma.

Ila next day jamaa alinicheki nkaenda jifunza kuendesha gari. Sitasahau ile aibu aiseee.
 
Baada ya 2yrs bila gari nikamuomba mshikaji gari nimpick demu. Nimensubiri kituo cha daladala. Alivyoshuka tukaanza kutembea kuelekea nilipopaki. Wakati wa kuingia nikajikuta nakaa kiti cha codriver kwa kudhani mimi abiria tu 😁. Nilivyokumbuka nikazugia kama kuna kitu nakiweka sawa upande huo kumbe jamaa nimesahau kuwa mimi ndo dereva.
 
Dah [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…