Kama hakuna anayejua siku au tarehe aliyozaliwa Yesu, kama kweli alikuwapo, inakuwaje Desemba 25 iwe siku ya kuzaliwa kwake?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Siku chache zijazo, waumini watasherehekea kuzaliwa kwa Yesu aka Kristo aka Issa Masihi aka Mwana wa Joseph aka Mwana wa Maria aka Issa bin Mariam aka Son of Man aka Mwana wa Adam aka Mwana wa Mungu aka Mkombozi aka Kristo au mpakwa mafuta aka Neno aka Mwana kati ya watatu waundao Mung nk. Kama kuna mtu mwenye ushahidi anayejua siku au tarehe aliyozaliwa Yesu––––kama kweli aliwahi hata kuwepo––––atusaidie kutujuza siku au tarehe hiyo. Ukisoma Biblia na Quran, hazielezi alizaliwa au kufa lini zaidi ya stori za Pwagu na Pwaguzi, Chizi na Mchizani. Je Yesu alizaliwa tarehe ngapi wanangu?
 
We nawe haya maswali yako yanazungumzwaga humu ndani kila kabla Xmass...

Na yalishajibiwaga ..

We pikeni Pilau mule ...labda uwe msabato ...
Maswali ya kijinga kabisa hayo anayouliza. Hatuadhimishi siku, tunaadhimisha tukio. Hata Christmass ingekuwa mwezi Julai tungekula Pilau na kujumuika na ndugu na jamaa.
 
Unachopaswa kufahamu Yesu Kristo alizaliwa duniani na ushahidi wa kuzaliwa uko kwenye vitabu vya Biblia(Luka1:31-35;2:10-20) na Koran,Q19:16-34
Tarehe ya kuzaliwa kwake haina tija kabisa!
Kwa tarehe yo yote tukio la kuzaliwa Yesu Kristo linaweza kuadhimishwa kama kumbukumbu!
Lakini zaidi sana ni kutukumbusha wanadamu kuwa Yesu Kristo alishazaliwa basi kilichobaki ni kumwamini ili kuipona ghadhabu ya Mungu ambayo iko juu ya kila mwenye dhambi ambaye hataki kutubu dhambi zake ili asamehewe,
(Warumi3:23;6:23)(Yohana3:16-20,36)
(Ufunuo21:8)
Mwamini Yesu Kristo LEO ili UOKOLEWE NA HUKUMU INAYOKUJA.
Asomaye na Afahamu.
 
IKO HIVI :

Sasa unataka Ushahidi gsni kuthibitisha ni 25/12?

Hata kama haikuwa tarehe hiyo kama Wakristo walikubaliana kuwa siku hiyo, Mungu anaheshimu makubaliano ilimradi lengo liwe kukumbuka kuzaliwa kwa Mwokozi.

KWA MFANO, hakuna mahala katika Biblia kunakosema watu wakioana wavae pete kama ishara ya kuoa au kuolewa ila wakristo walikubaliana na sio dhambi

Ukisoma Biblia vizuri, kuna mahali inasema hilo la Mungu kuheshimu Makubaliano yaliyo sahihi au Kiapo, hata kile cha Mahalamani

So Maadhimisho sio lazima yawe Exact day...muhimu ni LENGO

Najua ujuaji utakuwepo ila iko hivyo
 
Mkuu watu wale ubwabwa kwa amani hata kama yesu hayupo kabisa.😁😁
 
Hivi,huwa mnakerwa na hiyo sikukuu au ni ni hasa?Ikikaribia tu ndipo maswali yaleyale huulizwa utadhani mnakaribia kukata roho.Kama haiwahusu na hamuitaki mtulie wengine wafurahie.
 
Maswali ya kijinga kabisa hayo anayouliza. Hatuadhimishi siku, tunaadhimisha tukio. Hata Christmass ingekuwa mwezi Julai tungekula Pilau na kujumuika na ndugu na jamaa.
Acha upumbaff. Kama huna majibu uufyate. Kwani, kuuliza ni ujinga?
 
Ndiyo muwe mnayauliza kila mwaka kipindi sikukuu inapokaribia tu?Huwa hamna maswali mengine?Mkiitwa sadusts mtakataa?Roho zenu zinaonesha ni namna gani hampendi watu wawe na furaha kwa mambo yao.
 
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni ukweli wa kihistoria, na hata kalenda tunayotumia mhimili wake ni kuzaliwa kwa Yesu (BC na AD, kabla na baada ya Kristu). Ni ukweli kwa wote, wenye imani zozote za kidini au wasio na imani. Ni Historia.
 
Siku chache zijazo, waumini watasherehekea kuzaliwa kwa Yesu aka Kristo aka Issa Masihi aka Mwana wa Joseph aka Mwana wa Maria aka Issa bin Mariam aka Son of Man aka Mwana wa Adam aka Mwana wa Mungu aka Mkombozi aka Kristo au mpakwa mafuta aka Neno aka Mwana kati ya watatu waundao Mung nk. Kama kuna mtu mwenye ushahidi anayejua siku au tarehe aliyozaliwa Yesu––––kama kweli aliwahi hata kuwepo––––atusaidie kutujuza siku au tarehe hiyo. Ukisoma Biblia na Quran, hazielezi alizaliwa au kufa lini zaidi ya stori za Pwagu na Pwaguzi, Chizi na Mchizani. Je Yesu alizaliwa tarehe ngapi wanangu?
Huwezi pata tarehe yoyote,ni kumbukizi tu.
 
Ndiyo muwe mnayauliza kila mwaka kipindi sikukuu inapokaribia tu?Huwa hamna maswali mengine?Mkiitwa sadusts mtakataa?Roho zenu zinaonesha ni namna gani hampendi watu wawe na furaha kwa mambo yao.
Usihukumu tena kijinga usije hukumiwa. Kama hujui, jinayamzie tu mwanangu,.
 
Siku chache zijazo, waumini watasherehekea kuzaliwa kwa Yesu aka Kristo aka Issa Masihi aka Mwana wa Joseph aka Mwana wa Maria aka Issa bin Mariam aka Son of Man aka Mwana wa Adam aka Mwana wa Mungu aka Mkombozi aka Kristo au mpakwa mafuta aka Neno aka Mwana kati ya watatu waundao Mung nk. Kama kuna mtu mwenye ushahidi anayejua siku au tarehe aliyozaliwa Yesu––––kama kweli aliwahi hata kuwepo––––atusaidie kutujuza siku au tarehe hiyo. Ukisoma Biblia na Quran, hazielezi alizaliwa au kufa lini zaidi ya stori za Pwagu na Pwaguzi, Chizi na Mchizani. Je Yesu alizaliwa tarehe ngapi wanangu?

Kwanza Yesu si Issa bin Mariam.
Ukiona tofauti hiyo unaweza kupata majibu sahihi.
 
Back
Top Bottom