Kama hakuna Wamarekani waliouawa katika mashambulizi ya makombora ya Iran, basi Marekani haitokuwa na haja ya kujibu mashambulizi

Kama hakuna Wamarekani waliouawa katika mashambulizi ya makombora ya Iran, basi Marekani haitokuwa na haja ya kujibu mashambulizi

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,060
Mara tu baada ya mashambulizi kutekelezwa katika kambi mbili za kijeshi zinazotumika na majeshi ya Marekani nchini Iraq, Rais wa Marekani, Donald Trump alikuwa alihutubie taifa la Marekani kwa mujibu wa taarifa rasmi lakini mara baada ya kikao maalumu na maafisa wa ngazi za juu wa masuala ya ulinzi na usalama katika ikulu ya Marekani, White House alisitisha mpango wa kutoa hotuba hiyo.

Lakini hakuishia hapo bali Trump ali-tweet akisema kuwa;


"Kila kitu kipo sawa, kambi zetu mbili za kijeshi zilizopo Iraq zimeshambuliwa na Iran, tunafanya tathmini kujua kama kuna madhara yaliyopatikana au uharibifu wowote wa mali, yote kwa yote tuna vifaa bora vya kivita kuliko nchi yoyote ile Duniani, kwa mbali! Nitatoa tamko kesho asubuhi"

Mpaka sasa taarifa kutoka Marekani zinadai kuwa hakuna taarifa za vifo kwa wanajeshi wao huku Iraq pia ikisema vivyo hivyo, lakini Iran imedai kuwa mashambulizi yao yamefanikiwa kuwaua wanajeshi wa Marekani. Muda upo na tuendelee kuzisubiri taarifa zaidi hususani baada ya hiyo tathmini.

Ila kama hakuna Wamarekani waliouawa katika mashambulizi ya makombora ya Iran, basi sidhani kama Marekani atakuwa na haja ya kuyajibu kijeshi mashambulizi hayo kama Pentagon ilivyokuwa ikiweka wazi hapo awali na kama jambo hili ni kweli, basi wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kimataifa wanayaita mashambulizi haya yanayotajwa kama "kisasi" yaliyofanywa na jeshi la Iran kama hatua ya kuokoa nyuso zao (save face) mbele ya wananchi na dunia kwa ujumla.

Tuendelee kusubiri!

Mods sidhani kama kuna haja ya kuunganisha huu uzi, ni vyema ukabaki hivi hivi kama ulivyo.

Pia pitia mabandiko haya hapo chini kwa taarifa zaidi:

 
Marekani anatafuta sababu ya kuivamia Iran ili achukue mafuta kama alivyofanya Iraq, Libya, na alijaribu pia Venezuela, sasa anaitafuta Iran, kumuua general wao halafu wanatangaza wazi ili kuipa Iran hasira kisha akilipa tu kisasi, wanaingia jumla Iran kujichotea mafuta. Huu ni mtego, kwani wangemuua bila kujitangaza wangepungukiwa nini?
 
Marekani anatafuta sababu ya kuivamia Iran ili achukue mafuta kama alivyofanya Iraq, Libya, na alijaribu pia Venezuela, sasa anaitafuta Iran, kumuua general wao halafu wanatangaza wazi ili kuipa Iran hasira kisha akilipa tu kisasi, wanaingia jumla Iran kujichotea mafuta. Huu ni mtego, kwani wangemuua bila kujitangaza wangepungukiwa nini?
Venezuela pale alogonga mwamba aisee. Sijui wamerakani hawana roho wale mabwana yaani wao watu wengine wafe mradi wao Taifa lao lisimame.

Anyways.

Kila mtu ashinde mechi zake!
 
Venezuela pale alogonga mwamba aisee. Sijui wamerakani hawana roho wale mabwana yaani wao watu wengine wafe mradi wao Taifa lao lisimame.

Anyways.

Kila mtu ashinde mechi zake!
Ndio nationalism hiyo. Dunia ipo kwa ajili ya wanaoweza ku survive.

Wewe mnyonge wa Tanganyika huko usiyejulikana hata kwenye ramani ya dunia, endelea kuwa mnyonge kwa ajili ya "uzalendo" wa nchi yako!

It is the fittest who survive!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unalalamika na kulia nini? Kama hawajafa ulitaka aseme wamekufa? Mbona kule Kenya wamekubali kuhusu vifo na uharibifu?
Hata we jiulize mbona wako kimya ? sababu kipigo kikubwa walicho kipata haijawahi kutokea, yani wako wanafikiria wajibu uwongo upi ili Trump apate kusave uso wake. Hivi USA asijue mpaa mda huu hasara walio ipata kwani USA ni Tanzania.
 
:44 p.m.
U.S. ambassador to Israel says few U.S. casualties
JERUSALEM — U.S. Ambassador to Israel David Friedman said that early assessments of Iran’s missile strikes against U.S. forces suggested U.S. casualties may be limited.
“Initial assessments are positive and we pray these reports are true,” Friedman said before he addressed a forum on U.S. policy on Israeli settlements in Jerusalem Wednesday


Hahaha @ The washington post


22 a.m.
Iran claims dozens of U.S. deaths in missile strike
DUBAI — Iran’s Revolutionary Guard claimed Wednesday that dozens of U.S. soldiers were killed in a missile attack on Al-Asad base in Iraq. The U.S. military has said it is still assessing casualties.
In a statement to state television the elite Revolutionary Guard said 15 missiles hit 20 critical points killing 80 soldiers, wounding 200 and destroying large quantities of military equipment, including helicopters, according to the Mehr news agency.
 
Back
Top Bottom