Kama hali ikiendelea hivi bila mvua mpaka mwezi wa Sita, mwaka huu utakuwa mgumu sana

Kama hali ikiendelea hivi bila mvua mpaka mwezi wa Sita, mwaka huu utakuwa mgumu sana

Ila ww kweli hamnazo hayo maji ya kumwagilia nchi nzima mtayavuta bahari ya Hindi,,
Vyanzo vya maji (mito) inakauka kabisa nenda vijijini utajua!!!
Duuuu poleni Simanjiro (Manyara) kwa ukame unawakumba mpaka mifugo inakufa
Mtoa comment ana hoja.
Amekwambia huo uwekezaji utumie vyanzo vya maji ya vijito vya msimu?
Nchi yenye mziwa makuu kama hii unaweza ukawaza kufanya miradi ya kitaifa kwa udhaifu wa namna hiyo?
 
Kwenye Ile mikoa ambayo msimu wa Masika unaanza mwezi wa 11 hali ni mbaya mingine mpaka sahivi hakuna mvua ni msimu wa mvua. Na hii mikoa ndo mingi inayozalisha chakula kingi

Tofauti na Ile inayopata mvua mwezi wa tatu mpaka mwezi wa Sita mwanzoni

Kama una hela weka akiba ya hela kwa sababu ya scarcity vyakula vitaenda kupanda, kama unaakiba ya chakula weka akiba ya chakula, Kuna uwezekano hali ikawa mbaya sana kuanzia June na kuendelea

Watumishi wa kiroho huu ni mda wa kuombea mvua msisubiri Hali ikiwa mbaya mkasema mlitabiri sababu viashiria vyote vimeshaonekana
Hii picja ina maana sana
Hao wa hio mikoa wakiambiwa wapande miiti hawapandi na wanazidi kuikata iliopo acha ng'ombe wao wafe na njaa baadar wataanza kufukiwa wao.
Mnataka nani awasaidie kutunza mazingira.
 
Miti bila mvua ni maigizo!
Mti kuutunza hadi ukaimarishe mizizi yake unahitaji mvua yakutosha.
Mkuu tumepata mvua miaka mitatu mfululizo haikutosha kuotesha miti.
Kinachowasumbua watanzania wengi ni umajununi
Watanzania kuchoma misitu hovyo kwao ni jambo la kawaida sana.
Nimeona tbc makamu wa raisi akiwafokea wataalamu kushindwa kulinda miti walioipande bonde la dodoma ambayo imechomwa na wafugaji.
Unaotusumbua ni uzembe tu na uhayawani.
Yani
Warabu wamepanda miti jangwani sisi tunashindwa nini?
Kuna mzee wa Africa magharibi ameoneshwa na aljazeeera jinsi alivyo panda baobao tree, huwezi amini wanakijiji wakiafrika walikuwa wanamcheka na kumdhihaki kuwa ni chizi, sasa hivi wao wamegeuka chizi wanaenda kuvuna majani kwa mzee kwa ajili ya kulisha mifugo yao.
 
Kama huamini kwenye Mungu ni sawa, lakini wako wanaoamini kwenye Mungu usilazimishe watu waamini unachoamini,
Kama huamini kwenye Mungu ni sawa, lakini wako wanaoamini kwenye Mungu usilazimishe watu waamini unachoamini,
Unataka Mungu aje ukupandie miti kwenu?
Watu wameharibu mazingira halafu siluhu mnaitafuta kwa mungu.
Mungu aliweka kila kitu mahali pake. binadamu kujitia ujanja wa kukata mbao, kuni nk halafu hapandi miti mingine, hio mvua itatoka wapi? Hata mkeshe mnaomba haitanyesha maana kileta mvua mmemikata.
 
Kwenye Ile mikoa ambayo msimu wa Masika unaanza mwezi wa 11 hali ni mbaya mingine mpaka sahivi hakuna mvua ni msimu wa mvua. Na hii mikoa ndo mingi inayozalisha chakula kingi.

Tofauti na Ile inayopata mvua mwezi wa tatu mpaka mwezi wa Sita mwanzoni

Kama una hela weka akiba ya hela kwa sababu ya scarcity vyakula vitaenda kupanda, kama una akiba ya chakula weka akiba ya chakula, Kuna uwezekano hali ikawa mbaya sana kuanzia June na kuendelea

Watumishi wa kiroho huu ni mda wa kuombea mvua msisubiri Hali ikiwa mbaya mkasema mlitabiri sababu viashiria vyote vimeshaonekana
Tulishatoa ushauri mapema Sana kwamba Serikali izuie chakula kuuzwa nje ila akina Bashe wanajifanya wanajua Sana.

Mwaka huu mikoa mingi hususani ya Kati,kaskazini hakutakuwa na mvua za uhakika.
 
Kwani maji ya mito yanatokana nini, mfano Kilombero ifakara mito imekauka na chemchem zimekauka sababu ya uhaba wa mvua.

Mito na chemchem zinategemea sana mvua ili zititiririshe maji ndo maana jangwan hamna mito wala nchemchem
Jangwani kuna Mto Msimbazi
 
Muda huu hangaya anawaza mikopo na kusutana.
Kwa akili zako kisoda unadhani kwenye Hali ya ukame utapandisha Kodi au utapata fedha wapi kuokoa watu zaidi ya mkopo?

Serikali isipokopa Ili kuwasaidia na kuziba pengo la fedha mtakufa kama wanyama
 
Hii picja ina maana sana

Hao wa hio mikoa wakiambiwa wapande miiti hawapandi na wanazidi kuikata iliopo acha ng'ombe wao wafe na njaa baadar wataanza kufukiwa wao.
Mnataka nani awasaidie kutunza mazingira.
Mwaka huu ni kote mvua ni za kusuasua na za msimu
 
Ukame unakuja Mzee we endelea kusema bia tamu utajua hujui
 
Mvua zitakuja tu, hii ndio maana halisi ya mabadiliko ya hali ya hewa...
 
Umesahau na macheif nao waombee mvua

Kabla ya dinintukikuwa na wazeee wetu na hizo ndo zilikuwa kazi zao
 
Kwani maji ya mito yanatokana nini, mfano Kilombero ifakara mito imekauka na chemchem zimekauka sababu ya uhaba wa mvua.

Mito na chemchem zinategemea sana mvua ili zititiririshe maji ndo maana jangwan hamna mito wala nchemchem
Mikoa ya Singida na Dodoma kiasili ni jangwa, lakini aridhini pana maji mengi kuliko ziwa Victoria.
Kuna mabwawa na maziwa kila pande ya nchi.
Sasa hivi ni ukame ila kuna nyakati mvua zinasababisha mafuriko hadi kujaza maji majumbani mwa watu. Kwanini kusijengwe miundombinu ya kuvuna, kuhifadhi na kutumia maji ya mvua?
 
Kwenye Ile mikoa ambayo msimu wa Masika unaanza mwezi wa 11 hali ni mbaya mingine mpaka sahivi hakuna mvua ni msimu wa mvua. Na hii mikoa ndo mingi inayozalisha chakula kingi.

Tofauti na Ile inayopata mvua mwezi wa tatu mpaka mwezi wa Sita mwanzoni

Kama una hela weka akiba ya hela kwa sababu ya scarcity vyakula vitaenda kupanda, kama una akiba ya chakula weka akiba ya chakula, Kuna uwezekano hali ikawa mbaya sana kuanzia June na kuendelea

Watumishi wa kiroho huu ni mda wa kuombea mvua msisubiri Hali ikiwa mbaya mkasema mlitabiri sababu viashiria vyote vimeshaonekana
Upo sawa mkuu, hali ni tete kuna waliomba likizo fupi kwa ajili ya kwenda kulima lakini wiki 2 zimekwisha hivihivi hata tone la mvua! Wamerudi mjini na stori mbaya ! Hili jambo serikali ijipange na iwapange pia wananch wake kuna uwezekano tukapita kipindi kigumu sana cha njaa!
 
Back
Top Bottom