Kama hatujui kilichomo katika mkataba wa ujenzi wa Bwawa la Umeme huko mto Rufiji, tuna uhakika gani bei ya umeme itakuwa nafuu?

Kama hatujui kilichomo katika mkataba wa ujenzi wa Bwawa la Umeme huko mto Rufiji, tuna uhakika gani bei ya umeme itakuwa nafuu?

Hapana kiongozi, Rais Magufuli anauzalendo uliotukuka na uwazi upo

Uzalendo huonekana bila kuwa na madaraka ya urais, yuko serikali zote toka enzi za Mkapa, ni lini aliwahi kukemea mikataba ya wizi? Hata yeye hivi Sasa anafanya hivyo hivyo, ndio maana ni adui wa uhuru wa habari.
 
Ukishaona kiongozi anajifanya mzalendo lakini hataki uwazi, jua huyo ni mpigaji kama wapigaji wengine. Utasikia tunajenga mradi fulani kwa pesa za ndani, lakini fuatilia vizuri utakuta deni linapanda na hataki ifahamike hela anakopa wapi.
Na wewe nae ni mtu wa kuriri uongo wa Lissu? Yaani taarifa kuwa nchi imekopa huwa hazitolewi?
 
Attachments

  • Screenshot_20200912-200456.png
    Screenshot_20200912-200456.png
    26.8 KB · Views: 3
Na wewe nae ni mtu wa kuriri uongo wa Lissu? Yaani taarifa kuwa nchi imekopa huwa hazitolewi?

Wakati mwingine bora uwe unakaa kimya, kuna siku nilikuambia huo mradi wa reli kuna 3t+ imekopwa. Ukawa unalazimisha kuwa huo mradi ni fedha za ndani. Tena nikawa nashangaa iweje serikali ikakope huko huko bank ya China, wakati JK alikuwa ameshakubaliana na wachina kujenga huo mradi wa SGR kwa mkopo wa Exim bank ya China kwa $7b, kwa 100% ila kwa sharti kwamba kampuni ya ujenzi iwe ya China?

Kaingia Magufuli akabadili kampuni ya ujenzi, na uongo mwingi kuwa fedha ni za ndani, huku anakopa huko huko China kwa ujenzi wa vipande vipande.
 
Wewe dogo vuta kumbukumbu zako vizuri. Nilikuambia Dar Moro ndio kuna pesa ya ndani ilitumika.
Lakini Moro to Makutupora ndio hiyo 3tril ilikopwa tena openly tofauti na Tundu Lissu anavyowahadaa.

Reli aliyotaka kujenga JK ni reli ya Sgr ya kawaida kama ya Kenya ambayo inatoka Mombasa to Nairobi, na ule mkataba ulikuwa na mizengwe kwa hiyo acha upotoshaji.
 
Japo ni kweli kuwa umeme unaotokana na maji huwa ni wa bei nafuu kulinganisha na umeme unaotokana na vyanzo vingine kama vile mafuta, gesi,nuclear, n.k , lakini je,si kweli kuwa mkataba wa ujenzi wa chanzo husika cha umeme unaweza kufanya bei ya umeme kuwa kubwa kuliko inavyotarajiwa?

Kwa mfano, kama mkataba una kipengele kinachosema kiasi fulani cha fedha zitazotokana na mauzo ya umeme zitatumika kumlipa mjenzi/mkandarasi wa mradi, mkataba wa aina hii hauwezi kufanya bei kuwa kubwa kuliko inavyostahili?

Au kama mradi umejengwa na mkandarasi kwa gharama zake(awe amechukua mkopo au vinginevyo)huku akijilipa kwa kutumia sehemu ya fedha za mauzo ya umeme, hapa bei ya umeme haiwezi kuwa kubwa kuliko inavyotarajiwa?

Kwasababu ya kujiuliza ni mengi na kwakuwa hatujui kilichomo katika mkataba, ni bora tu tukawa walpole kuliko kuwa washangiliaji.

Tukumbuke ya gesi ya Mtwara na hatima yake kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Yan umezungumzia kwa mfano yani huna uhakika na unacho sema bora usinge kuja hapa
 
Sisi tunamuamini Rais Magufuli kila anachochosema Kwasababu ni mcha Mungu na wala hajatumwa na Wazungu kuja kuharibu Nchi km yule mgombea

Umeme utakuwa sawa na bwerere, tunamuomba Rais Magufuli awe makini na Chadema wasije wakabomoa bwawa
Hakuna mcha Mungu anayeteka watu, anayeua watu, anayepoteza watu wala kuamrisha wakosoaji wake wapigwe risasi.

Matendo ya Roho ni dhahiri. Nayo ni upendo, huruma, umoja, msamaha na kiasi.

Kimyume cha hayo ni chuki, kiburi, majivuno, dharau, utengano, uonevu na husda. Hayo ni matendo ya shetani. Kulotajanjina la Mungu kila mara haikufanyi uwe mcha Mungu.

Tusimshikamanishe Mungu na matendo ya shetani. Hiyo ni kulikufuru jina lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema mnaroho mbaya.kila jambo jema la nchi yetu mnaliwekea kisununu.
JPM aingie mikataba ya kizembe,hivi kile chuma unakijua au unakisikia tu kwenye taarifa ya habari?
 
Si bwawa la umeme tu mi sielewi hata hii mikataba mipya kibao tunayoingia na hawa mabeberu wa madini..hata sielewi kwa nini inafichwa fichwa wakati madini ni mali ya watanzania ?
Mali ya watanzania.....? nani kasema...?
 
Mwambie huyo mgombea wa Chadema aache uongo. Atapata aibu kubwa sana mwaka huu. Naweka ushahidi hapa chini kuonyesha malipo yanafanyika kwa awamu na sio kwamba mkandarasi atalipwa kutokana na mauzo ya umeme. Acheni siasa za uongo
Sawa
 
Back
Top Bottom