Kama haujawahi kunywa energy drinks Hongera na Jiepushe nazo. Kama umezoea kuzitumia Tafadhali weka mpango wa kupunguza na kuacha

Kama haujawahi kunywa energy drinks Hongera na Jiepushe nazo. Kama umezoea kuzitumia Tafadhali weka mpango wa kupunguza na kuacha

Watu wa boda boda wanakipenda kweri kweri

Ova
 
Nikajua umekuja na utafiti, kumbe ni porojo tu!
 
  • Thanks
Reactions: FWC
Kinywaji pekee nipendacho ni maji na juisi ya asili (ya kutengeneza na matunda og)

Nina miaka kadhaa sinywi soda wala kinywaji chochote cha kiwandani
Hata hizo juice siyo salama pia, kula matunda kwa kiasi

Ukinywa juice ya chungwa unakamua machungwa mangapi?
 
Majibu tyari mtaani ingawa mdo mdo sana. Kijana wa 20s au below alipata shida kwenye moyo wake muhimbili wakamuwahi kisa hvo vdude.
 
Kinywaji pekee nipendacho ni maji na juisi ya asili (ya kutengeneza na matunda og)

Nina miaka kadhaa sinywi soda wala kinywaji chochote cha kiwandani
Ila hiyo haitakufanya usife mkuu maana mademu unagegeda bila ndom na unazama kunako chumvi sasa si bora mnywa energy tu hapo
 
Hizo zina watu wake.
Wale tunaotumia nguvu nyingi kufanya kazi ndo zetu
 
Acha kutisha watu kisa Mo hajawahi kunywa, nini faida ya kufa na kuzikwa ukiwa na afya njema?
 
hizo kitu hazifai

niligida vikopo viwili, aisee ilikuwa kidogo nikate moto aicee.

mapigo ya moyo yalipanga ghafla nikahisi kama Izraeli mtoa roho yuleee ananingoja

ilikuwa naelekea kuzimika laivu.

saivi kama lazima ninywe ivo vidude basi lazma nichanganye na vitu vingine kama maji soda nk
 
Marekani wanaoongoza kwa kufanya kazi duniani wanapiga 5hr energy shots na zingine stronger zaidi ya hiyo ya Mo mara 10 miaka na miaka na kuna redbull hadi za nusu lita na hawajaona hiyo hatari we na vibarua wako mmeona hd kuanzisha thread? Umetumwa kuua biashara za watu? Sio mbaya fanyeni utafiti kwa emperical data then conclude sio kutazama vijana wako watano kuja kuanzisha uzi wa kuharibu maelfu ya ajira za watu na kodi!
 

Attachments

  • IMG_7375.png
    IMG_7375.png
    3.3 MB · Views: 8
  • IMG_7374.png
    IMG_7374.png
    743.3 KB · Views: 8
Ila hiyo haitakufanya usife mkuu maana mademu unagegeda bila ndom na unazama kunako chumvi sasa si bora mnywa energy tu hapo
Mimi sio shabiki wa uvinza, kuhusu ndom situmii ila kuna vipimo, na mimi mtu wa kubadili mademu,
 
Kipindi nipo Law School nilikuwa lazima ninywe Mo Xtra mbili nazimix na Hills Water. Aisee nkishika kitabu cha Dr. Tenga na Dr. Mramba tutakutana asubuhi hapo.

Ila nashukuru Mungu nilikuja kuacha baada ya ile shule ngumu kuisha.
 
Mimi sio shabiki wa uvinza, kuhusu ndom situmii ila kuna vipimo, na mimi mtu wa kubadili mademu,
Vipimo vinakudanganya ndani ya masaa 72 aliye pata maambukize anaweza kuambukiza mwingine lakini ndaniya masaa 72 HIV test kit haiwezi kusoma ikakupa ya +ve
 
Too much of anything is harmful , mimi ni mtumiahi wa energy drinks wa siku nyingi tangu enzi hizo za red bull hayo madhara sijawahi kukutana nayo sabab nakunywa kwa sababu maalumu mara mbili au tatu hivi kwa mwezi.

Japo hayo madhara hata mimi nimeyshuudia kwa watu wengi wanaotumia sana
 
Peace,

Awali ya yote niweke wazi andiko langu halina kusudi la kuhafifisha au kuathiri biashara ya mtu yeyote ila ni ushuhada wa kweli na dhairi wa watu wanaonizunguka.

Nimekua nikisikia na kuona vijana wengi wakipendelea vinywaji vya kusisimua mwili alimaarufu "energy drinks" ziko za aina mbali mbali na bei tofauti. Vijana kama boda boda, wanafunzi na vibarua wa kazi za mikono wamekua watumiaji sana wa vinywaji hivi.

Nilipata kusikia na kwa sasa nimeshuhudia kua vinywaji hivi vina uraibu mkali sana na pia athari za moja kwa moja kwa watumiaji wa mara kwa mara. Nina mifano mingi ila nitataja michache kwa lengo la kujenga hoja na kujifunza kwa pamoja.

Kuna vijana kwenye maegesho ya boda boda nimekua nawasikia kua ili siku iende sawa lazima wanywe energy wengine wamekua hata na utaratibu wa kununua za ziada na kuifadhi ili anapoamka tu cha kwanza ni kunywa energy ndio hujiisi utayari wa kuanza kazi.

Mwezi uliopita nilikua na project ya ujenzi nikawa napita kutazama mradi unakwendaje kulinganisha na report ya msimamizi wa mradi ajabu pale site palikua na makopo ya mo-energy na azam energy mengi sana wala sikujali ila cha kushangaza kuna siku nilikuta wamepiga kazi kwa makisio ya kua mbele ya estimated target kwa zaidi ya kama 25% nilifurahi sana nikaamua kuwalipia bili zao za chakula kwa siku tatu.

Mshangao ulikua wangu waliponisihi sana sana niwaongezee bajeti kucover pia "energy" nilipohoji kulikoni msisitizo ule wakajibu "yani hata chakula hakina maana kama hakuna energy" looo !! Nikasema sawa nitaongeza bajeti ya kinywaji hicho kwa kila mmoja aise shangwe walilopiga ni kubwa mara dufu ya nilipowapatia ahadi ya kulipia chakula. Vijana wako adicted mbaya.

Kuna classmate wangu kwa sasa ni muajiriwa shirika fulani la uma kama afisa manunuzi anakiri bila kunywa energy drink anajihisi kupoteza umakini na uwezo wa kuconcetrate mpaka apate vinywaji hivi.

Sasa hivi karibuni amekua analalamika kuhisi kutetemeka hasa kipindi cha usiku na kifua kuuma na kuhisi moyo kwenda mbio sana hasa anapopata wasiwasi wa jambo hata dogo tu na kuhisi kizunguzungu mda wa jua kali akanishirikisha basi nikajaribu kubrowse mtandaoni ya kwamba nini hasa kinaweza kupelekea matatizo haya ajabu ajabu kote majibu yanahusishwa na matumizi ya kupindukia ya energy drinks.

Nikamshirikisha jamaa akasema pia yeye alikua anahisi watatizo hayo yanahusiana na vinywaji ya kusisimua mwili kwa kua matatizo yote hayo yanapomkuta na basi akapata fursa na akipiga energy mbili chap chap anakua fresh kabisa aise jamani tujihadhari.

Nikaona nifanye ufuatiliaji wa jambo hili nikawafuata boda boda nikawauliza kama kuna nyakati wanajihisi kutetemeka mikono, au kuhisi moyo kwenda mbio au kuhisi kupoteza umakini au kifua kuuma na kizunguzungu.

Kwa mshangao wakasema yote hayo yanawakuta kwa nyakati tofauti ila wakanishangaza kwa mara nyingine kwa kuniambia yote hayo yanapowakuta hununua energy ya baridiiii na kunywa na shida zote na mashwahibu hayo hupotea kwa sekunde chache tu.

Ikumbukwe vinywaji hivi havina hata muda wa miaka 10 sokoni lakini madhari yake yameanza kushuhudiwa punde tu mtumiaji anapotumia je matumizi ya muda mrefu yatakua na madhara kiasi gani ?!

Mimi sio daktari wala sina ujuzi wowote wa kitabibu lakini naona viashiria dhahiri vya madhara ya vinywaji hivi. Niliwahi kuona clip fupi ya Mo Dewji akisema hajawahi kuonja ladha ya vinywaji vyake, (jambo fikirishi sana)

Karibuni tujadili nini uzoefu wako katika matumizi ya vinywaji hivi ?


View attachment 2906241
Mimi sio mnywaji wa mara kwa mara wa hivi vinywaji lakini ikitokea nimekunywa huwa napata hali ya kutetemeka na mwili kushtuka shtuka
 
Back
Top Bottom