Kama haujawahi kunywa energy drinks Hongera na Jiepushe nazo. Kama umezoea kuzitumia Tafadhali weka mpango wa kupunguza na kuacha

Mimi sio energy, nina tabu na Pepsi bariiiidi. Umekuwa ni ugonjwa sasa pia angalieni na hivyo vipombe kali vya kwenye makopo
 
Wewe ndo huelewi
Hiyo mo extra Ina caffeine tu ndo inayokosesha usingizi... caffeine hata kwenye vinywaji vya cola ipo Ila huwezi ukaiita ni energy drink
Halafu kuandika tahadhari siyo matakwa ya mo ni matakwa ya mamlaka zinazokagua vinywaji hivyo
 
Ukitumia kupita kiasi lazima upate madhara .

Then hivyo vinywaji ni kwa ajili ya WATU masikini ili viwasaidie kufanya kazi ngumu.

Na kuhusu kuumwa moyo na figo hiyo ni kweli watu wanaumwa Sana na kufa Sana Ila kwakuwa kundi kubwa ni WATU masikini huwezi kusikia hili jambo mahala popote.

Binafsi nimetumia Energy drink wakati nafanya maandalizi ya mitihani yangu ya mwisho Form four na form na six .
 
Kinywaji pekee nipendacho ni maji na juisi ya asili (ya kutengeneza na matunda og)

Nina miaka kadhaa sinywi soda wala kinywaji chochote cha kiwandani
Juicy pekee niipendayo ni ya miwa sijawahi kunywa energy Wala soda situmii miaka sasa
 
Kwa uzoefu wangu energy sio salama,nikinywa hata moja saa mbili usiku basi usingizi ntaupata kuanzia saa Tisa usiku,halafu ni kama inasisimua sana mwili ,lakini pia Ina addiction,najitahd sana kuachana nazo
 
Kwaiyo ata redbull ni mbaya au ni mo na azam energy tu ebu fafanua vizuri maana naona km umewalenga Mo na Azam engery

Najua ni mafundi na boda boda wachache sana wanaweza kununua redbull so mreta mada ugomvi wako ni energy drink zote au ni mo na Azam
 
Hakuna kisicho na madhara hasa ukikizidisha

Kuleni mboga za majani mbichi mbichi, nyama nyingi na mazoezi ya kukimbia kila siku
 
Kuna cocaine kwa mbaaili enewi ungewanunulia nyingi ungewawekea ktk friji wanyweee mpka waseme .poo alafu ungewaelezea mazara yake ila vijana wengi watapata magonjwa kama kiharusi stroke na mshtuko wa moyo uko mbeleni
 
 
Acha wajimalize
 
Duuh hatari Mimi nakamtindo ka kumix smart gin na energy kumbe najiandalia ka njia ka kwenda kukula bikra mbinguni
Kunywa sana. Sio mtu unakufa halafu viungo vyako vingine vizima kabisa! Inatakiwa unakufa maini, figo, mapafu hayatazamiki yapo nyang'anyang'a.
 
Huku kutishana kote ni mbinu za kukwepa kifo? Au maradhi?

Anyway ushauri wangu mimi ni kila mtu aishi atakavyo tusitishane maana kifo hakikwepeki kuna miaka kadhaa mbele sisi wote tunaokunywa energy na wasio kunywa wote hatutakuwepo, cha msingi kama unaifurahia we kunywa tu mkuu, tusiogopeshane...kila kitu ni hatari kwa afya yako hata hiyo sim unayotumia kuchati kutoa ujumbe nayo inaaminika ina mionzi ambayo ni hatari kwa Afya, hiyo bodaboda unayotumia nayo ni hatari kwa afya yako, hiyo gari unayotumia nayo ni hatari kwa afya yako, hilo gorofa unaloishi pia ni hatari kwa hatari kwa Afya yako.... TUSITISHANE WALA USIHARIBU BIASHARA YA MTU KWA KUPANDIKIZA CHUKI ZA KIJINGA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…