Tatizo la sasa kwa vijana ni.moja tu:- Hawakuwahi kufundishwa kwa kina kabisa ili wajue kwamba 1. Ngono SIO mapenzi 2. Wewe mwanaume ujue unapodhani mwanamke atakupenda kwa sababu ya utajiri wako, UNAJIDANGANYA. Unaweza kujikuta unachapiwa na kibega wa Kariakoo shimoni japo una mamilioni ya dola, rolls royce, na maghorofa kadhaa. 3. Kama wakati unatafuta ajira unafanya dua na sala, basi ukitaka kuoa usiache kuweka dua na sala tena kwa nguvu kuliko dua za kutafuta kazi. Kazi utadumu nayo miaka 35 lakini mke utakuwa nae hadi utakapoingia kaburini 4. Kila mvulana anataka apate mke mzuri sana kwa mwonekano wa nje (very beautiful) lakini hakai akawaza kwamba ni mara chache sana uzuri wa nje umeambatana na uzuri wa tabia na moyo wenye wema. Tena hataki kukubali kwamba kama yeye amemtamani, wapo pia na wanaume wengine, wenye uwezo kuliko wake wamtamani pia. 5. Kijana usifanye haraka kuoa. Tena hakikisha msichana wako anajua kwamba kabla hujamvika pete unao uhuru wa kwenda out na wengine. 6. Jaribu kila uwezalo kuchunguza historia na tabia za msichana uliyekutana nae barabarani. Inawezekana alikuwa na "mtu wake wa kudumu" chuoni wakati hapo hapo alikuwa na "zee la posho" mjini, na hapo hapo ana mchumba kijiji. Halafu wooote hao, (pamoja na wewe), mmeshaonjeshwa "asali" yake. Vijana ambao bado hamjaoa, kuweni makini, zingatieni sana mambo haya.