Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hewa ina uzito kama wewe.Habari za jioni wadau....
Kama mnakumbuka nilileta mada kuhusu chanzo au asili ya Oxygen, Nashukuru wadau walinipa elimu nzuri kuhusu Oxygen na nikaelewa vyema.
Leo pia nina swali kuhusu Oxygen au hewa.
Kwa mujibu wa sayansi, asili ya hewa au mazingira yake ni lazima iwe katika eneo ambalo limefungwa, ndani yake kuwe na pressure na kizuizi ili hewa hiyo isitoke.
Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote na haina mwisho.
Je, inakuwaje mpaka duniani panakuwa na mgandamizo wa hewa ingali pande zote zipo wazi?
View attachment 3057848
Naomba wadau wa sayansi ya mazingira mnijuze kuhusu hili....
Sababu inayokufanya wewe usiruke juu na kutoka nje ya uso wa dunia, ndiyo hiyo hiyo inayofanya hewa isitoke nje ya uso wa dunia.
Gravity.
Ushaelewa?