Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Hewa ina uzito kama wewe.

Sababu inayokufanya wewe usiruke juu na kutoka nje ya uso wa dunia, ndiyo hiyo hiyo inayofanya hewa isitoke nje ya uso wa dunia.

Gravity.

Ushaelewa?
 
Unajadili kipi sasa wakati majibu ya kisayansi yapo toka karne kibao tu nyuma
 
Hewa ina uzito kama wewe.

Sababu inayokufanya wewe usiruke juu na kutoka nje ya uso wa dunia, ndiyo hiyo hiyo inayofanya hewa isitoke nje ya uso wa dunia.

Gravity.

Ushaelewa?
Bado sijaelewa, nadhani gravity ni kitu cha kufikirika na hakina uhalisia
 
Ukiurusha mpira juu,hua unaenda juu na kupotelea huko juu au huo mpira huanguka chini coz ya Earth Gravitation Force?

Ukipata jibu hapa utakua umepata jibu la swali lako
Mpira lazima utarudi chini, na hiyo ni kutokana na uzito wa mpira, na eneo lipo wazi hakuna kizuizi, hivyo ni lazima mpira urudi chini
 
Ndege wanapaa angani na hawadondoki
That is a logical non sequitur fallacy.

Ukweli kwamba kuna vitu vinaweza kuishinda gravity haumaanishi gravity haipo.

Ukweli kwamba kuna wakati unaweza kula na kushiba usisikie njaa, haumaanishi kuwa njaa haipo.

Unamaanisha tu kwamba njaa haikupati wakati wote.

Ndege kuweza kupaa angani haimaanishi kuwa gravity haipo, inamaanisha tu kuwa kuna namna ya kuruka angani na kuishinda gravity.
 
Ndege ni physical object, hewa haionekani....

Ni kipi husababisha hewa ibaki ndani ya uso wa dunia na isifike juu?
 
Mpira lazima utarudi chini, na hiyo ni kutokana na uzito wa mpira, na eneo lipo wazi hakuna kizuizi, hivyo ni lazima mpira urudi chini
Kukufahamisha wewe sio kazi rahisi coz hua unabishana na kushindana na wanaokupa majibu,nakumbuka uzi wako wa hewa,mwisho niliamua kukuacha tu,

Kwani hukusoma kabisa? Elimu yako ikoje?
 
Kama ni kitu cha kufikirika kwa nini ukitoka nje ya obiti ya dunia ,ukiwa deep space, ukirusha kitu kinaenda juu zaidi tofauti na ukiwa kwenye obiti ya dunia?
Kurusha kitu kikaenda juu zaidi sio kwenye space tu, hata ndani ya maji pia.

Lakini binafsi sijawahi kuamini kama kuna mtu amewahi kutoka nje ya dunia(space)
 
Kukufahamisha wewe sio kazi rahisi coz hua unabishana na kushindana na wanaokupa majibu,nakumbuka uzi wako wa hewa,mwisho niliamua kukuacha tu,

Kwani hukusoma kabisa? Elimu yako ikoje?
Nilikimbia umande, ila ukiona nabisha basi ujue sijaridhika na majibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…