Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Maana ya Gravity ni mkusanyiko wa maneno tu, nataka uthibitishe uwepo wa hiyo Gravity kwa kunipa mifano hai na sio kusema ukirusha jiwe juu linarudi
Mm sijaongelea kurusha jiwe nilikuambia kuhusu centripetal na centrifugal force huelewi, circular motion na rotational Dynamics hujui, maana ake huwezi kuelewa hata iweje najua ushalishwa matango pori huko unakuwa na fixed mind so bora ubaki na myth zako maana ukielewa au usipoelewa hamna kitu kitakachobadilisha uhalisia
 
Nyie watu wa arts mnasumbua kweli....so wewe unaona nimeuliza swali...

Ndugu ,ndege haielei yenyewe bali inatumia engine na mabawa kuzalisha force itakayo kinzana na Gravity....

Hata ndege kiumbe hutumika mabawa yake kuzalisha kinetic force ya kulingana na gravity....
Nilikuambia aache kuingilia taaluma za watu anakaza kichwa tu anahisi ku solve calculus ni kila mtu anaweza ee 😂😂
Sisi mbna hatuingilii utunzi wa diwani?
Kila mtu aheshimu taaluma ya mwenzake
 
Maana ya Gravity ni mkusanyiko wa maneno tu, nataka uthibitishe uwepo wa hiyo Gravity kwa kunipa mifano hai na sio kusema ukirusha jiwe juu linarudi
Unadhani kwa nini ukirusha jiwe juu haliendelei kwenda daima, ila linarudi chini?

You're not serious. Umepewa jibu halisi, umeishia kulibeza.
 
Mm sijaongelea kurusha jiwe nilikuambia kuhusu centripetal na centrifugal force huelewi, circular motion na rotational Dynamics hujui, maana ake huwezi kuelewa hata iweje najua ushalishwa matango pori huko unakuwa na fixed mind so bora ubaki na myth zako maana ukielewa au usipoelewa hamna kitu kitakachobadilisha uhalisia
Point yako ni ipi katika hayo maelezo yote?
 
Unadhani kwa nini ukirusha jiwe juu haliendelei kwenda daima, ila linarudi chini?

You're not serious. Umepewa jibu halisi, umeishia kulibeza.
Jiwe haliwezi kubaki juu kwasababu lina uzito na hakuna kitu kinachoweza kulizuia lisirudi chini....

Ni sawa na urushe jiwe juu ya bati, litabaki huko kwakua limekutana na kizuizi
 
Nikikaa barabarani lazima nitahisi navutwa endapo gari litapita karibu yangu, na hiyo ipo proved bila shaka.

Je, umeshawahi kuhisi au kuona namna ambavyo dunia inazunguka kwa kasi na kuvuta hewa upande wa globe?

Ni vipimo au namna gani hutumika kugundua na kushuhudia huo mzunguko na uvutwaji wa hewa? Nani aliwahi kuona hicho kitu?
Labda tuanzie hapa.

Dunia inazunguka ama haizunguki?

Kama inazunguka, tambua kwamba inazalisha kani tovu (centripetal force) na kani pewa (centrifugal force).

Kani hizi ndizo pia zinahusika na ufyonzwaji wa hewa (suction effect) na vitu vingine ili viendelee kubaki kwenye ukanda wa dunia.

Kama unaelewa kwamba kitu chochote kilicho katika mwendo huvuta vingine ili kuvilazimisha viondoke nacho, si vigumu hata kidogo kuelewa jinsi dunia inavyoburuta na kuambaa na anga lake pamoja nayo.
 
Dunia haizunguki
 
Acha kusumbua watu hapa mkuu,hutopata majibu ya kueleweka,Swali lako hilo liweke Kwa Lugha ya Kiingereza halafu uingie Google utapata majibu ya uhakika na Utaridhika

Tatizo hapa sio lugha; tatizo ni kuwa na back ground ya Physics hata kuielewa hiyo google kutategemea uelewa wake wa mambo ya sayansi (physics). Sasa kama mtu hajui hata Gravitation force, Density nk huoni itakuwa vigumu kumwelewesha labda mtu amsimulie tu juu juu kama hadithi...
 
Jiwe haliwezi kubaki juu kwasababu lina uzito na hakuna kitu kinachoweza kulizuia lisirudi chini....

Ni sawa na urushe jiwe juu ya bati, litabaki huko kwakua limekutana na kizuizi
Sawa kabisa. Usibadilishe chaneli. Baki hapa hapa.

Fikiria tumefanikiwa kutoboa shimo fulani kwenye dunia hadi upande wa pili, ili kuruhusu jiwe hilo liendelee kuzama na kushuka chini kwa kuliondolea kizuizi chochote kinacholishikilia.

Unadhani nini kitatokea?

Je, jiwe hilo litaserereka na kupitiliza hadi upande wa pili kwenye uso wa dunia (kama kutoka ncha ya kusini hadi kaskazini)?

Na kama ingetokea jiwe hilo likafika upande wa pili, lingeendelea kujongea katika uelekeo huohuo? Maana kwa mujibu wako, kizuizi kimeondolewa.
 
Fkiria tumefanikiwa kutoboa shimo fulani kwenye dunia hadi upande wa pili, ili kuruhusu jiwe hilo liendelee kuzama na kushuka chini kwa kuliondolea kizuizi chochote kinacholishikilia.

.
Hilo shimo linatobolewa kuanzia wapi mpaka wapi, unajua kwamba kwa mujibu wa hiyo sayansi, katikati ya dunia kuna kitu kinaitwa "inner core'?

Sasa unawezaje kutoboa shimo na katikati ya ardhi kuna joto na mvutano mkali?
 
Hapo Kuna hoja kuu Mbili
1. Gravitational force
Àmbayo NI force(kani au Ñguvu ) ya uvutano àmbayo chanzo chake NI Jua. Kani au Ñguvu inavyovisukuma Vitu katikati ya Dunia.
Dunia inatabaka kuu nne, Tabaka la Maji(Hydrosphere), tabaka la ardhi(Crust) hili hutambulika kama Biosphere, tabaka la hewa au anga(atmosphere)

2. Uzito (Density )
Uzito WA hewa unaongezeka kadiri unavyoliacha anga au uso wa Dunia
 
Jiwe haliwezi kubaki juu kwasababu lina uzito na hakuna kitu kinachoweza kulizuia lisirudi chini....

Ni sawa na urushe jiwe juu ya bati, litabaki huko kwakua limekutana na kizuizi

Uzito na ndege na jiwe unalolirusha unazungumziaje?
Mbona Ndege inauzito Mkubwa lakini inapaa na kuelea angani huku jiwe likianguka CHINI?
 
Hapo Kuna hoja kuu Mbili
1. Gravitational force
Àmbayo NI force(kani au Ñguvu ) ya uvutano àmbayo chanzo chake NI Jua. Kani au Ñguvu inavyovisukuma Vitu katikati ya Dunia.
Dunia inatabaka kuu nne, Tabaka la Maji(Hydrosphere), tabaka la ardhi(Crust) hili hutambulika kama Biosphere, tabaka la hewa au anga(atmosphere)

2. Uzito (Density )
Uzito WA hewa unaongezeka kadiri unavyoliacha anga au uso wa Dunia
Kama dunia ina tabaka kuu nne, tabaka ya kwanza kabisa iliyo chini ni ipi?
 
We jifunze kuheshimu taaluma za watu usitake kuwa mjuaji kwenye kila kitu
Sijaleta ujuaji, nimeuliza swali na watu wanatoa maoni yao, hata wewe pia nakushukuru kwa kuchangia maoni yako katika mada hii..
 
Dunia haizunguki
Ungesema mapema basi. Maana mambo mengi yanayojadiliwa hapa hutegemea uhalisia huo.

Kuna vithibitisho vingi kuhusu mzunguko wa dunia (revolution) na mzingio ama mviringiko wake (rotation).

Hebu tuanze na hii moja. Usiku na mchana hutokeaje?
 
Kuna vithibitisho vingi kuhusu mzunguko wa dunia (revolution) na mzingio ama mviringiko wake (rotation).
Vithibitisho gani hivyo? ni vipimo gani hutumika kupima au kuona mzunguko wa dunia?
 
Back
Top Bottom