Elections 2015 Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali kuhusu figisu figisu za kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, ambapo kila anayeshindwa, hakubali kushindwa kihalali kwenye sanduku la kura katika uchaguzi huru na wa haki, na badala yake huja na tuhuma za kuibiwa kura, kupokwa ushindi halali, na kususia matokeo, hivyo bandiko hili ni swali, Kama Tuhuma Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu? iliyoingia madarakani kwa hila, udhalimu na ulaghai?. Kama ni kweli, then Hukumu ya Karma ii juu serikali yetu na viongozi wake waliohusika na udhalimu huu kwa karma kuwashughulikia. Na kama sii kweli, ni uzushi tuu, then tutamshuhudia huyu mzushi anayemzushia rais Magufuli na serikali yake kuwa ni madhalimu, kwa kumtwisha tuhuma za udhalimu, akitandikwa na bakora za karma, kwake yeye binafsi na kwa chama chake, huku Rais Magufuli, Chama chake na serikali yake, wakibarikiwa, nchi yetu ikibarikiwa na kupata neema na ustawi.

Naomba kuanza na angalizo. Hli ni bandiko swali la dhana tuu ya kufikirika, hypothetical situation kuwa if A is true, then B is true, if A is not true, then B is not true!. Hivyo kwa wenye uelewa wa mashaka mashaka wa wengi wetu humu, msije kushangaa wakashindwa kukiona hicho kitangulizi cha "kama ni kweli", na kupelekea kudhania nimesema serikali yetu ni serikali dhalimu!, ninachosema hapa ni kama hii tuhuma iliyotolewa leo na Edward Lowassa ni kweli, then..

Tuhuma yenyewe imetolewa hapa
Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais - JamiiForums


Kama tuhuma hii ni kweli, then serikali ya rais Magufuli itakuwa ni serikali dhalimu, iliyoingia madarakani kwa njia ya udhalimu na uharamu, na udanganyifu wa kwenye sanduku la kura, kitu ambacho sio kizuri kwa mustakabali mwema wa nchi yetu, taifa letu na watu wake, kwa mujibu wa sheria ya karma. Karma ina uzuri wake na ubaya wake, uzuri wa karma ni lazima italipa!, ubaya wa karma, haiitandiki serikali as serikali, kwasababu serikali sio natural being, bali karma itawatandika viongozi wa serikali, waliohusika na udhalimu huu. Tatizo kubwa la karma katika kuwatandika, ni haina Mswalie Mtume wa kujali nani ni nani, ikianza kutembeza kichapo cha bakora, ni bakora tuu kwa kwenda mbele bila kujali nani ni nani!. Ubaya wa karma, haijulikani utalipiza lini, ila ikitokea alietenda udhalimu huu, ameitwa kuondoka duniani kabla ya kulipa deni lote la karma, then deni hili linahamia kwa familia yake!, kitu ambacho its not fair kwa mtu asiye na hatia kubebeshwa kufidia makosa ya mtu mwingine!.

Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ndiye rais chaguo la Mungu kwa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.

Kupitia kwa Magufuli, Tanzania itapata neema, mafanikio na maendeleo makubwa ya ajabu kwa sababu ya baraka za Mungu zitakuwa juu yake, nchi yetu inakwenda kageuka kuwa ni ile nchi ya ahadi ya maziwa na asali.

Neno litasimama, mambo mengine yote yatapita, lakini neno litasimama!.

Mungu ibariki Tanzania.

Paskali

Kwa rejea mambo ya karma, karibu mitaa hii
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili
"Bora Katiba", Tuikubali!, Tusiichukie CCM!, Kwa Sababu
When Karma comes calling, she stings like a bitch
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanaz
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa
 
Mungu ndio msemaji wa mwisho ...tutafunga kwa maombi na sadaka tutatoa Mungu akapate kujidhihirisha
 
So sad wametutukana malofa, kura wametuibia wazi wazi, mabomu wametupiga, sehemu nyingine ubunge wamechukua kwa nguvu, zanzibar wamedhulumu kwa nguvu na ushindi wamechukua kibabe. Waliofanya haya hukumu yao ni ya kifo.

Ee baba Mungu uwalipe ujira wao bila kuwapunja. Amen
 
wewe hukuwah mpenda Magufuli, ulivuka mipaka na kujiita Nabii kuwa Rais ajaye n Eddo, wananch tumemkata na amekaaaa, swal rahis hiv Eddo apate kura zote hzo toka wapi?mikoa ipi labdba? mbona hana wabunge kabsaa? angekubalika kwa kiasi hko tungewaona wabunge 100+ toka Ukawa.......


wachaw wa Edo

Chadema kwa kumchafua miaka 7 iliyopta
Gwajima a.k.a mshenga kuwa msemaj wake kampotezea kura nying za waslam
safu yake ya kampein Mbatia, Sumaye< mbowe na Mrema hawa n watu wa jamii moja, pale wanaposimamia issue ya kitaifa na kuonekana n sura zile zile hutilia shaka hata jamii nyingne kujilinda, na hiki ndicho wana lake zone na mikoa mingne walchokifanya.... Eddo kapigwa na wanzania wote kasoro wapemba
 
Amen !

 
anatangazwa mshind siku hyo hyo anaadhimisha siku yake ya Kuzaliwa hajaona tu kuw huyu ndiye chaguo la Mungu
 
Pasco hivi mwenzako Ocampor four na Mussa Allan vp wanaendeleaje! nasikia wame commit criminal offense! ndo maana Mzee Ruksa aliwashauri msipende kuvuka mipaka haya ndo madhara yake! eti mahaba nyambafff
 
Mkuu Inauma Sana, Amwachietu MUNGU Atamlipia Kwa Wote Walio Usika Kuipotoa Haki Ya Walio Wengi, Malipo Ni Hapa Hapa, Haki Ya Mtu Haipotei. Ikiwa MUNGU Amemridhia Kuwa RAIS Itakuwatu.
 
Mm nimeshaanza KUFUNGA KWA MAOMBI....!!! Kama ni ushindi wa haki, MUNGU hatatoa ADHABU...!!!

Kama ni USHINDI wa DHULUMA, MUNGU ataangamiza watu, hadi wakome...!!! Narudia, Mungu ataangamiza wahusika hadi wakome...!!!

In Jesus name...!!!
 
Edward Lowassa ni nani?

Wewe Pasco nnakusihi kaa kimya na ukubali matokeo.

Amini.
 
Last edited by a moderator:
Wewe kijana ni mpumbavu na lofa kabisa. Yaani ni loofaaa. Rais wako ni Dr Magufuli!

Binti, Tumia Basi Maneno Yenye Utu Kwa Ndugu Zako, Sote Ni Watanzania Hatuna Budi Kueshimiana Ndiyo Utamaduni Ulio Wakitanzania Mkuu Wangu, Kila Mtu Anao UHURU Wa Kutoa Maoni Yake Bila Kuvunja Sharia Na Kueshimu Utu Wa Wengine Uo Ndio Ustaarabu Ndugu.
 
angekubalika na wananchi si tungeona majimboni angepata kura za kutosha ivi jaman kwa lile gape alilopigwa loaswa kwa mtu mwenye akili as great thinker unaweza kuisini kweli CCM imechota au tunafosi ushindani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…