Wanabodi,
Leo siku ya Machi 17 ndio siku Taifa tulipotangaziwa kifo cha Shujaa wetu JPM, hivyo katika kumkumbuka, na kumuenzi, mnaonaje tukijikumbusha baadhi ya mabandiko ambayo tulimshauri JPM na ushauri huo ukafanyiwa kazi, kwa kutaja Bandiko, ulishauri nini, na nini kilikuja kufanyika kwa ushauri huo, na jee kulisaidia JPM? Kulisaidia nini?
Kwa vile JPM alikuwa ni mbabe kwa kufanya baadhi ya mambo kibabe, hadi kutafsiriwa ni dikiteta, hivyo baadhi ya ushauri kwa JPM pia ulitolewa kibabe kwa kumpiga Spana za kutosha, ila tukubali tukatae, Spana za JF zilimsaidia sana JPM na kulisaidia taifa.
Kumuenzi JPM, naomba tujikumbushe baadhi ya mabandiko, tuliwahi kushauri nini kwa kuandika nini na kutoa ushauri wa nini kifanyike, na kufuatia ushauri huo, nini kilifanyika na jee kilimsaidia JPM?kilimsaidia kivipi?. Jee kililisaidia taifa?, kililisaidia kivipi?
Hili ni moja ya mabadiliko hayo ambalo limemsaidia sana na kulisaidia taifa.
Na mwisho kwa vile sasa Samia ndie Rais wetu, JF tunapaswa kuendelea kutimiza wajibu wetu kwa kumsaidia Samia, kwa vile JPM alikuwa ni rais mbabe vivyo hivyo ushauri ulitolewa kibabe, lakini Samia no Mtaratibu, mstaarabu, jee licha ya utaribu na ustaarabu, Mama Nate tumpige Spana kama za JPM? au twende naye taratibu kama alivyo, kwa Mama iwe ni kumkuna tuu, na tusimpare kama alivyo shauri mwenyewe, kuwa ukinikuna vizuri nitakukuna ila ukinipara, nitakuparua?
Mabandiko mengi ya kuwakumbuka marehemu huishia kwa RIP kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi kwavile wanakuwa hawajui marehemu yuko wapi,, lakini mimi kwa vile tayari nimeisha kulishwa JPM yuko wapi
Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani bado kuna haja ya kuendelea kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi huku tayari najua yuko peponi?.
Pumzika Magufuli Pumzika! Tutakukumbuka Daima!
Paskali!