Elections 2015 Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Mama Samia amekuja kukamilisha kazi ya Magufuli, hizi neema na baraka nilizozitaja hapa, sasa zinakuja kukamilishwa na Mama Samia.

Huu utumbuaji wa leo, ni uthibitisho sasa kupitia kwa Mama Samia, Tanzania itapata neema, mafanikio na maendeleo makubwa ya ajabu kwa sababu ya baraka za Mungu zitakuwa juu yake, nchi yetu inakwenda kageuka kuwa ni ile nchi ya ahadi ya maziwa na asali.
Paskali
 
Sema safari hii Ukuu wa Wilaya lazima Kaka yangu ondoa shaka usinisahau kwenye Ufalme wako...
 
Pascal nasikitika kukuambia kuwa
Hua nashindwa kukuelewa unashindwaje kuielewa CCM jinsi inavyowatendea wapinzani kinyume kabisa na matakwa ya katiba na wewe unakaa kimya tu.
Mkuu lee van cliff , karibu mitaa hii uone kimya changu.
P
 
Wanabodi,

Leo siku ya Machi 17 ndio siku Taifa tulipotangaziwa kifo cha Shujaa wetu JPM, hivyo katika kumkumbuka, na kumuenzi, mnaonaje tukijikumbusha baadhi ya mabandiko ambayo tulimshauri JPM na ushauri huo ukafanyiwa kazi, kwa kutaja Bandiko, ulishauri nini, na nini kilikuja kufanyika kwa ushauri huo, na jee kulisaidia JPM? Kulisaidia nini?

Kwa vile JPM alikuwa ni mbabe kwa kufanya baadhi ya mambo kibabe, hadi kutafsiriwa ni dikiteta, hivyo baadhi ya ushauri kwa JPM pia ulitolewa kibabe kwa kumpiga Spana za kutosha, ila tukubali tukatae, Spana za JF zilimsaidia sana JPM na kulisaidia taifa.

Kumuenzi JPM, naomba tujikumbushe baadhi ya mabandiko, tuliwahi kushauri nini kwa kuandika nini na kutoa ushauri wa nini kifanyike, na kufuatia ushauri huo, nini kilifanyika na jee kilimsaidia JPM?kilimsaidia kivipi?. Jee kililisaidia taifa?, kililisaidia kivipi?

Hili ni moja ya mabadiliko hayo ambalo limemsaidia sana na kulisaidia taifa.

Na mwisho kwa vile sasa Samia ndie Rais wetu, JF tunapaswa kuendelea kutimiza wajibu wetu kwa kumsaidia Samia, kwa vile JPM alikuwa ni rais mbabe vivyo hivyo ushauri ulitolewa kibabe, lakini Samia no Mtaratibu, mstaarabu, jee licha ya utaribu na ustaarabu, Mama Nate tumpige Spana kama za JPM? au twende naye taratibu kama alivyo, kwa Mama iwe ni kumkuna tuu, na tusimpare kama alivyo shauri mwenyewe, kuwa ukinikuna vizuri nitakukuna ila ukinipara, nitakuparua?

Mabandiko mengi ya kuwakumbuka marehemu huishia kwa RIP kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi kwavile wanakuwa hawajui marehemu yuko wapi,, lakini mimi kwa vile tayari nimeisha kulishwa JPM yuko wapi Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani bado kuna haja ya kuendelea kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi huku tayari najua yuko peponi?.

Pumzika Magufuli Pumzika! Tutakukumbuka Daima!

Paskali!
 
Kulikuwa na udhalimu gani? Maana ukisema udhalimu, je wewe ukuwahi kuandika au kukosoa kipindi hicho?

Na huyo anayemuita dhalimu alikuwa akujua? Na alikufanya chochote kibaya?

Tusipende kuongeza chumvi kama alikuwa kiongozi katili na hafai
Karibu
P
 

Hili ni bandiko la kauli ya Lowassa baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015.
Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Kada wa Ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…