Elections 2015 Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Wanabodi, hata janga hili la kirusi cha Corona japo ni janga la kimataifa, na Tanzania ni sehemu ya kimataifa, hali ya Corona kwa Tanzania ukilinganisha na nchi nyingine, ni uthibitisho mwingine kuwa Magufuli ni chaguo la Mungu kwa Tanzania. Kinachoendelea kwenye Corona kwa Tanzania, hatuwezi kujitapa ni preparedness ya taifa kuzuia, ni neema tuu za Mungu na baraka zake kwa taifa letu chini ya mtu wake aliyebarikiwa.

Kwanye Corona, Watanzania tuendelee kumshukuru Mungu sana kwa mpaka hapa tulipo fika kwa kutuepusha na tuendelee kumuomba Mungu aendelee kutukingia mkono wake.
P
 
Ni kweli kabisa Magufuli ile nafasi ya kuwa kiongozi wa malaika huko mbinguni atapewa
JPM amebarikiwa ni chaguo la mungu corona hiwezi kuisumbua TZ ya Magufuli

JPM na Makonda hawa ni chaguo la mungu
Italy USA waje wachukue baraka kwa JPM corona itaisha huko kwao
Jpm baba lao makonda baba lao
 
Narudia kukwambia tena mkuu paskal, Mungu Adhihakiwi apandacho mtu ndicho avunacho, tawala yenu ya kisukuma imekuwa chukizo kwa Mungu, mapigo ya adhabu yameanza na mnaenda kudondoka
Mkuu Ngonidema , Duh...!. I don't believe this!
P
 
Duh...!.
P
Kama mtaalamu wa nguvu ya akili, je, hii ndiyo karma uliyoitabiria kama serikali hii ni dhalimu?

Kama sivyo, tukubali ule upande mwingine kuwa nchi yetu imebarikiwa na kuneemeka na uwepo wa serikali hii?

Tuambie P kwani inaonekana sikuhizi unakwepa kujibu maswali ya wachangiaji kwenye threads zako.

Mwaka huu tukiacha ya miaka 4 iliyopita nchi iko kwenye mtanziko WA

Corona

Mafuriko ikiwemo kujaa maji maeneo ya mito, mabwawa na maziwa.

Waziri mkuu ofisi yake imeunda kamati ya jambo moja tu na LA mvua nyingi si tatizo na umma hawajaathirika kwa wingi! Ndivyo?
 
Ni nchi gani ya afrika imeathirika zaidi ya Tanzania, kuna nchi hazina hata mgonjwa
 


Mkuu bado unasimamia hili bandiko lako au umetengua kauli?
 
Kwenye hii Serikali dhalimu iliyotapakaa damu za Watanzania? Mie siyo mtu wa kununulika ili kuunga mkono udhalimu.
Hili la possibility ya serikali yetu kuwa dhalimu linazungumzwa sana na wapinzani for political scores, lakini tuhuma hii inapoletwa na mwana jf mwandamizi kama wewe Mkuu BAK, ukisema serikali dhalimu iliotapakaa damu za Watanzania, jee una ushahidi?.

P
 
Kuuawa kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na shambulizi la kutaka kumuua Lissu kwako wewe si UDHALIMU na kutekwa na kubambikiwa kesi Watanzania mbali mbali akiwemo Erick Kabendera na viongozi wa juu wa Chadema etc ni utani tu au ni UDHALIMU uliofanywa na MABEBERU.

Hili la possibility ya serikali yetu kuwa dhalimu linazungumzwa sana na wapinzani for political scores, lakini tuhuma hii inapoletwa na mwana jf mwandamizi kama wewe, ukisema serikali dhalimu iliotapakaa damu za Watanzania, jee una ushahidi?.


P
 
Mkuu pasco tupe tathimini yako ya miaka mitano ya serikali je ni laana au imebarikiwa??
Mkuu mliberali, simba Mwendo ni baraka kwa kwenda mbele, mfano kwenye hili janga la Corona, angalia majirani zetu maambukizi yanavyoongezeka na watu wao wanavyokufa kwa wingi, lakini huku kwetu update ya mwisho ilifanywa 17 days ago!, hakuna maambukizi mapya wala kifo chochote!.
No news is good news.
P
 
Kwanza maadam Ben Saanane haijulikani kilichomkuta, huwezi kusema kauwawa!.
Jee una ushahidi hata wa kimazingira tuu kuthibitisha serikali inahusika?.

The same applies to Azory Gwanda, hakuna uthibitisho wowote kuwa ameuwawa na hakuna ushahidi wowote hata wa kimazingira, wa uhusika wa serikali.

Kwenye shambulio la Lissu, kila mtu anajua limepangwa na limetekelezwa na watu wasiojulikana. Jee una ushahidi wowote wa serikali kuhusika?. Yaani ushahidi wa wasiojulikana ni serikali yetu tukufu?.

Nijuavyo mimi, wasiojulikana wa Lissu ni hawa

Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

P
 
Paschal, heshima kwako! Hebu in future jaribu kusummarize posts zako, watu hawana muda mwingi wa kusoma. Nawakilisha maoni ya wengi, jaribu kulifanyia kazi mkuu!
 
Paschal, heshima kwako! Hebu in future jaribu kusummarize posts zako, watu hawana muda mwingi wa kusoma. Nawakilisha maoni ya wengi, jaribu kulifanyia kazi mkuu!
Asante, hili nimeisha anza kulifanyia kazi kwenye bandiko hili nimelichinja. Mimi ni story teller, ila nakubaliana na wewe, Watanzania wengi ni wavivu kusoma, na sijui wangapi humu wana soma novels, au kuangalia telenovelas!.

Nitajitahidi sana kila bandiko langu in future kuwa na summary kwa ajili ya wavivu wa kusoma, halafu kuwe na long version ya wapenda mastori.

P
 
Mkuu The Boss, japo hoja yako hii ni ya zamani, lakini umetisha sana!. I think something was going to happen, ili kuzuia that something isi happen, ndio mkambidi mtu aitwe, achukuliwe na kuleta Suluhu ili kuleta suluhu ya hali iliyokuwepo!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…