Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,916
- 6,527
Ikiwa tarehe 23 August ni mapumziko, je karani atazifikia kaya zote kwa siku hiyo?
Hilo zoezi la sensa litaendelea kwa siku sita kulingana na nilivyosikia mwanzo, na kila siku hapo karani wa sensa atakuwa na majukumu tofauti, kuna kujua hesabu ya watu waliolala kwenye kaya husika, kujua idadi na wazee, vijana, wanawake, watoto, na wanaume, n.k Naona kama wamelirefusha hilo...
Nianze kwa kusema tu kwamba kuna baadhi ya maamuzi ya kawaida katika nchi yetu, yanatia mashaka kuhus maamuzi mengine magumu!
Ikiwa zoezi la sensa halikueleweka miongoni mwa walio wengi wakiwemo viongozi wa ngazi mbalimbali na wananchi wa kawaida hasa kuhusu muda wa kufanyika kwa zoezi hilo na umuhimu wa mapumziko; je ni mambo mangapi ambayo hayaeleweki kwa wananchi na viongozi?
Kwa miaka yote iliyopita sensa ilianza kufanyika siku ya jumapili na kuendelea kwa muda wa wiki moja au zaidi.
Swali ni je, wananchi wa kawaida na viongozi wanajua historia ya mambo mbalmbali yaliyowahi kufanyika na hatimaye kuyachukua kama rejea ya kufanya kwa ubora zaidi?