Kama hili la halikueleweka kwa walio wengi, je ni mangapi hayaeleweki?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,916
Reaction score
6,527

Nianze kwa kusema tu kwamba kuna baadhi ya maamuzi ya kawaida katika nchi yetu, yanatia mashaka kuhus maamuzi mengine magumu!

Ikiwa zoezi la sensa halikueleweka miongoni mwa walio wengi wakiwemo viongozi wa ngazi mbalimbali na wananchi wa kawaida hasa kuhusu muda wa kufanyika kwa zoezi hilo na umuhimu wa mapumziko; je ni mambo mangapi ambayo hayaeleweki kwa wananchi na viongozi?

Kwa miaka yote iliyopita sensa ilianza kufanyika siku ya jumapili na kuendelea kwa muda wa wiki moja au zaidi.

Swali ni je, wananchi wa kawaida na viongozi wanajua historia ya mambo mbalmbali yaliyowahi kufanyika na hatimaye kuyachukua kama rejea ya kufanya kwa ubora zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…