Katika mahusiano ya nchi na nchi hakuna kitu kama “kuaminika” wala “kuaminiana”. Hakuna “nchi rafiki” wala “nchi adui”. Kuna “maslahi” na “mikakati” tu. Ukikaa kijinga unaliwa tu hata na umdhaniaye rafiki.
Lugha kama “mabeberu”, “manyang’au”, n.k. zinatumika na viongozi wa nchi zisizo na mwelekeo wa maana kiuchumi, kisiasa, na kimkakati. Nchi ambazo zinafikiri bado tuko enzi za Cold War!
Badala ya kupanga karata zetu vizuri jinsi tutakavyoiweka Kenya sawa ili tupate maslahi ya maana kiuchumi, tunaendekeza kutangaza uadui na kumimina mipasho kibao dhidi yao. Tunaonyesha hasira na jazba zisizo na maana. Heri Mama SSH kaenda kuweka taswira mpya.
Kenya wanachofanya ni kuendelea kutumwagia tabasamu la kinafiki hata kutupigia magoti ikibidi almuradi waendelee kuhodhi soko la Tanzania katika kila nyanja. Wanamiliki ardhi kubwa tu nchini kwetu. Wana-export mazao yetu muhimu kama kahawa na maparachichi hata mahindi. Wanafaidi vivutio vyetu vya utalii, n.k. Ikibidi, penye udhia wanapenyeza rupia.