Kama kweli Mo kaitoa hiyo ahadi ni sawa kwa upande wala asilaumiwe anatakiwa apongezwe. Kumalaumu kwa sababu ya kutoa ahadi ni kumwonea tu kwani yeye kwa upande wake ametimiza wajibu wake kwa kuleta hamasa kwenye timu na kuinua morali upya kwani wachezaji walikuwa wameshapoteza matumaini kabisa.
Suala kubwa hapa ni jee benchi la ufundi limejiaandaaje kukabiliana na dhahama ya Kaizer Chief? Kwani wale jamaa wako vizuri sana maumbo yao makubwa, mpira wanauweza sana, wana kasi sana na benchi lao la ufundi lililizidi mbinu kwa mbali sana benchi la ufundi la Simba kwenye mchezo wa kwanza kule Afrika Kusini. Sitashangaa sana Simba akipigwa tena goli za kutosha na hapa nyumbani.