Kama hofu inaua, wangapi walikufa kwa hofu baada ya ajali mbaya ya lori la mafuta Msamvu-Morogoro?

Kama hofu inaua, wangapi walikufa kwa hofu baada ya ajali mbaya ya lori la mafuta Msamvu-Morogoro?

lukoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2013
Posts
2,995
Reaction score
2,249
Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu wa kizazi hiki anaweza kukimbilia ajali ya lori likiangua liwe na maji, mafuta ya taa, diesel au petrol aliyeshuhudia iwe kupitia Tv au kwa macho eneo la ajali mbaya ya lori la mafuta iliyotokea Msamvi Moro. Hii ni kwa sababu ya hofu ya kuwaona binadamu wenzetu wakiungua kama kuni. Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha kwenye ajali ile.

Hata wendawazi, wavuta bange na machizi wa msamvi hivi sasa hawezisongelea lori likiangua hata kama lina maziwa. Hii yote ni kwa sababu ya hofu! Hofu husaidia, hofu inafaida nyingi kuliko hasara.

Wakati wa kuchukua hatua ndiyo sasa tusisubiri vita iishe wakati ndiyo imeanza. Tulipofika sasa pabaya tumepuuza mpaka hofu ya Mungu.

Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.
 
Hivi kweli tukishakuwa na hofu na corona bila kuchukua hatua stahiki ndio hatutakufa?

Jr[emoji769]
 
Kwaiyo unajaribu kusema kwamba wanaogopa kutoa statistics za uhalisia wa hali ilivyo sababu wanaogopa kuwa wanachi wao watapata hofu duu?
 
Wavuta bangi tunawekwa kundi moja na wendawazimu na machizi. Mbona walevi ni watu wa ovyo sana ila hawatajwi. Au kisa pombe zinachangia uchumi wa taifa kwa kulipa kodi?

Sent From Galaxy S9
 
Wavuta bangi tunawekwa kundi moja na wendawazimu na machizi. Mbona walevi ni watu wa ovyo sana ila hawatajwi. Au kisa pombe zinachangia uchumi wa taifa kwa kulipa kodi?

Sent From Galaxy S9
Machizi wengi walianzia kwenye bangi 😀 😀😀
 
Neno TAHARUKI silipendi kwa Kweli


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mwaka jana watu wameumwa sana ila hadi sasa hakuna hata uchunguzi uliyofanyika kujua walikuwa wanasumbuliwa na nini ila sasa toka ije ishu ya corona basi na kuoneshwa watu weupe wakifa huko basi imekuwa balaa kila kitu corona, cha ajabu corona yenyewe ina dalili kama ambazo walizokuwa nazo watu mwaka jana. Watu wanataka kujua tu idadi ya wanaoumwa na kufa wakati kuna megi yasiyoeleweka yanatakiwa yaeleweke kuliko hata kutaka kujua mmekufa wangapi.
 
Waliugua ila hawakufa sana kama sasa ulishawai zika watu namna hii acha uongo
Mwaka jana watu wameumwa sana ila hadi sasa hakuna hata uchunguzi uliyofanyika kujua walikuwa wanasumbuliwa na nini ila sasa toka ije ishu ya corona basi na kuoneshwa watu weupe wakifa huko basi imekuwa balaa kila kitu corona, cha ajabu corona yenyewe ina dalili kama ambazo walizokuwa nazo watu mwaka jana. Watu wanataka kujua tu idadi ya wanaoumwa na kufa wakati kuna megi yasiyoeleweka yanatakiwa yaeleweke kuliko hata kutaka kujua mmekufa wangapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio sahihi bora idadi itolewe...ili tujue tunajilindaje mbona wenzetu wanatoa idadi kamili na hawapati hofu ya kufa sisi ni nan hass
 
Back
Top Bottom