Kama huamini kwamba Yesu alikufa Msalabani, unapitwa na baraka hizi

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Wasioamini kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu, wanakosa baraka nyingi ambazo Mungu ametupatia kupitia mateso, kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo. Zifuatazo ni baadhi ya baraka hizo kuu:

1. WOKOVU WA ROHO ZETU
Biblia inasema wazi:
"Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16).
Kupitia kifo cha Yesu, sisi tuliokuwa tumetengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi, tunapokea msamaha na kuunganishwa tena na Mungu. Msamaha umeishatolewa lakini ili uupate ni lazima uamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yako.

2. UPONYAJI WA MAGONJWA
Kifo cha Yesu msalabani kilibeba sio dhambi tu, bali pia maumivu yetu.
"Kwa kupigwa kwake sisi tumepona" (Isaya 53:5). Wale wanaomwamini Yesu wanapokea uponyaji wa kiroho na kimwili kwa Jina lake. Mimi binafsi nimepona magonjwa mengi sana kwa kuyakemea kwa Jina la Yesu.

3. MAMLAKA JUU YA SHETANI
Yesu alizishinda nguvu za giza kwa kufa na kufufuka kwake (Wakolosai 2:15).
Kila anayeamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu, anapewa mamlaka juu ya shetani, wachawi na mapepo na kuishi mbali na hofu.

4. MIUJIZA KWA JINA LA YESU
Wanafunzi wa Yesu walitenda miujiza kwa jina la Yesu aliyefufuka: Petro akamwambia kiwete: "Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende" (Matendo 3:6).
Leo hii bado jina la Yesu lina nguvu ya kutenda miujiza katika maisha ya watu wanaomwamini. Mungu amenitendea miujiza mingi ya kifedha, ya kikazi na kifamilia katika maisha yangu. Miujiza hii ni matokeo ya kuamini kifo cha Yesu msalabani.

5. UHAKIKA WA UFUFUO NA MAISHA YA MILELE
Yesu alisema: "Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye, ajapokufa, atakuwa anaishi" (Yohana 11:25). Kwa hiyo, wale walioko ndani ya Kristo hawana hofu ya kifo tena, maana kuna tumaini la ufufuo. Maandiko yanatuambia, Yesu atakapokuja atawafufua wale tu waliolala(waliofariki) katika Bwana (1 Wathesalonike 4:13–16). Wasioamini hawana tumaini hilo.

Hizo ni baadhi tu ya baraka tunazozipata kutokana na kifo cha Yesu msalabani na kufufuka kwake. Baraka hizi, shetani hapendi tuzipate, ndio sababu anakazana usiku na mchana kuwadanganya watu kwamba eti Yesu hakufa msalabani, eti kifo kile kilikuwa cha kisiasa tu. Tumpinge shetani kwa Jina la Yesu, asituzuie kupata baraka hizo. Amen
 
Mimi binafsi nimepona magonjwa mengi sana kwa kuyakemea kwa Jina la Yesu.
 
Duh ujinga huanzia pale unapoamini kitu bila kuwa na evidence
 
Huyo ni Mungu wa Waisraeli aliyemtoa mwanae kafara. Mungu wangu hana shida na kafara, ana uwezo uliokamilika. Ufufuko ni hadithi tu za sungura.
 
Hakuna la kushangaza yesu kufa msalabani,

Hukumu ya msalabani ilikua ni Kwa wahuni wote WA kiyahudi, yesu akiwemo.

Ndo maana pale msalabani hakuna peke yake, walikuepo vibaka pande zote mbili.

Ebu acheni kukuza mambo
 
Duh ujinga huanzia pale unapoamini kitu bila kuwa na evidence
Kifo na kufufuka kwa Yesu havikutokea gizani. Kuna ushahidi wa:
Kihistoria: Maadui wa Yesu na wanahistoria kama Josephus, Tacitus walikubali kuwa alisulubiwa
Maandishi ya mitume: Wengi walishuhudia kuwa walimwona Yesu aliyefufuka.
Kubadilika kwa maisha ya watu: Wale waliokuwa waoga (kama Petro), walibadilika wakawa mashujaa wa imani baada ya kumwona Yesu aliye hai.
Miujiza na uponyaji unaoendelea kwa jina lake hadi leo ni ushahidi tosha.
 
Kila anayeamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu, anapewa mamlaka juu ya shetani, wachawi na mapepo
Ni kwanini watumishi wengine wakifukuza majini wanakemea wee mpaka jasho linawatoka
 
Wasioamini kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu, wanakosa baraka nyingi ambazo Mungu ametupatia kupitia mateso, kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo. Zifuatazo ni baadhi ya baraka hizo kuu:

1. WOKOVU WA ROHO ZETU
Biblia inasema wazi:
"Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16).
Kupitia kifo cha Yesu, sisi tuliokuwa tumetengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi, tunapokea msamaha na kuunganishwa tena na Mungu. Msamaha umeishatolewa lakini ili uupate ni lazima uamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yako.

2. UPONYAJI WA MAGONJWA
Kifo cha Yesu msalabani kilibeba sio dhambi tu, bali pia maumivu yetu.
"Kwa kupigwa kwake sisi tumepona" (Isaya 53:5). Wale wanaomwamini Yesu wanapokea uponyaji wa kiroho na kimwili kwa Jina lake. Mimi binafsi nimepona magonjwa mengi sana kwa kuyakemea kwa Jina la Yesu.

3. MAMLAKA JUU YA SHETANI
Yesu alizishinda nguvu za giza kwa kufa na kufufuka kwake (Wakolosai 2:15).
Kila anayeamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu, anapewa mamlaka juu ya shetani, wachawi na mapepo na kuishi mbali na hofu.

4. MIUJIZA KWA JINA LA YESU
Wanafunzi wa Yesu walitenda miujiza kwa jina la Yesu aliyefufuka: Petro akamwambia kiwete: "Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende" (Matendo 3:6).
Leo hii bado jina la Yesu lina nguvu ya kutenda miujiza katika maisha ya watu wanaomwamini. Mungu amenitendea miujiza mingi ya kifedha, ya kikazi na kifamilia katika maisha yangu. Miujiza hii ni matokeo ya kuamini kifo cha Yesu msalabani.

5. UHAKIKA WA UFUFUO NA MAISHA YA MILELE
Yesu alisema: "Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye, ajapokufa, atakuwa anaishi" (Yohana 11:25). Kwa hiyo, wale walioko ndani ya Kristo hawana hofu ya kifo tena, maana kuna tumaini la ufufuo. Maandiko yanatuambia, Yesu atakapokuja atawafufua wale tu waliolala(waliofariki) katika Bwana (1 Wathesalonike 4:13–16). Wasioamini hawana tumaini hilo.

Hizo ni baadhi tu ya baraka tunazozipata kutokana na kifo cha Yesu msalabani na kufufuka kwake. Baraka hizi, shetani hapendi tuzipate, ndio sababu anakazana usiku na mchana kuwadanganya watu kwamba eti Yesu hakufa msalabani, eti kifo kile kilikuwa cha kisiasa tu. Tumpinge shetani kwa Jina la Yesu, asituzuie kupata baraka hizo. Amen
Kwanini mungu alimtoa sadaka mwanaye ili kumaliza dhambi badala ya kumuua shetani ambaye ndio chanzo cha dhambi kwa mujibu wa biblia?
 
Baraka nyingine ni zipi?
 
Huu ni wakati mwafaka wa kujikumbusha tena mada hii muhimu
 
Karibuni nyumbani, tufurahie msosi wa Pasaka
fruits.jpeg
food.jpeg
 
Back
Top Bottom