Kama hujajenga pitia hapa usifanye makosa kwenye wiring yako

Kama hujajenga pitia hapa usifanye makosa kwenye wiring yako

Ngoja kwanza mbona unatupeleka mbiombio mwendo wa ngiri? Eenhe bado sijakuelewa japo nimependa mada
 
Kiongozi, tunaomba estimation ya umeme wa jua kwa majumbani tu, mfano nyumba inayotumja umeme wa 150,000Tsh kwa mwezi, 414.5 unit. Nahitaji investment ya kiasi gani ili nitumie umeme wa solar na Tanesco iwe ndio umeme mbadala ?
Kwa matumizi yako unahitaji 15M kwa umeme wa uhakika boss
 
Uhakika wa nishati ya umeme katika nyumba ni jambo muhimu kila mmoja anafaham hilo; Tunajua namna gani nishati hii imekua sio ya uhakika wakati mwngne, kwa kuzngatia hilo nikupe wazo wakati unajenga nyumba yako kukabiliana na hiyo hali ili isikuletee usumbufu siku za mbeleni.

Kuna namna mbili unaweza kuzitumia;
1. Kama vifaa vyako vinatumia mkondo mnyoofu (DC) basi utahitaji kusuka wiring ya solar itakayojitegemea tofauti na ile ya umeme wa kawaida (AC), hapa maana yake kuanzia taa itabidi ufunge mbilimbili kila chumba, moja ya umeme na moja ya solar , kwa upande wa vifaa kama redio, TV n.k, hakikisha unapokinunua kifaa husika kina mfumo wa DC na AC,, siku hizi vifaa vingi viko hivo ni wewe tu kuchagua.

Katika mfumo huu utahitaji ku install power station (battery, charge control n.k) karibu na mahali ambapo vifaa kama TV &Radio na vifaa vinavyohitaji current nyingi vitakapokaa.

Pointi kubwa hapo ni kwamba umeme wa mkondo mnyoofu hupotea kwa wingi kwa sababu husafiri katika voltage za chini kwa hivo current huwa kubwa hivo kupelekea umeme mwingi kubadilishwa kuwa joto kutokana na ukinzani wa vipitishi(conductor).

Kwa hivo inatakiwa distance kati ya chanzo na kitumiaji kuwa ndogo sana as well as possible huku ukitumia waya nene zisizo na ukinzani mkubwa kama shaba.

Hasara ya hii design ni kwamba kwanza mpangilio wa power station unaweza kukuhaibia mwonekano wa sebule yako mfano, kwa Sababu kitu kama TV kinakaa katka sebule na kwa sababu hakutakiwi kuwepo umbali mrefu kati ya chanzo na hiyo TV yako basi itabidi battery na vifaa vyake vikae hapohapo sebuleni (utakua umenielewa) lakini kama utaona una namna unaweza ku design vitu vkakaa poa ni wewe tuu.

Hasara ya pili huu mfumo unatumia gharama kubwa wakati ufanisi wake ni mdogo. Nimeshasema utahtajika kununua mfano taa ziwepo za kujitegemea tena zikiwa katika wiring ya peke yake, lakini pia swala la upotevu wa umeme kutokana na kanuni ya Power loss haitakwepeka japo utakua umepunguza pakubwa (hata siku moja nishati haiwezi kusafiri pasipo kupotea ila kwa hii design kiwango cha upotevu kinakua kwa kiwango kikubwa).

Hasara ya tatu, ikiwa utatumia Lead acid battery (hizi znazotumia sulphuric acid kama electrolyte) zinapojaa huwa zinatoa hydrogen na oxygen katika process wanayoita (gassing) sasa mfano charge control ipate hitailafu battery ita overcharge kupelekea over gassing ikitokea chanzo chamoto basi faham hydrogen ita react na oxygen kwa kuwaka (italipuka).

2. Njia ya pili ni ya kutumia wiring ileile ya umeme wa kawaida (AC) na kila kitu kitabaki katika hali yake. Utakachofanya hapa ni mara baada tuu ya kufunga power station yko ya sola utahitajika kuwa na inverter ambayo kazi yake itabadili umeme wa DC ule wa sola kuwa AC na ku step up voltages at the same time.

Hapa umeme wetu ukishabadilishwa kuwa AC na hiyo inverter ina maana tunaweza kuutumia kwa matumizi ya kawaida bila kuhitaji vifaa special vya DC wala nini. Utakachofanya kuuingiza umeme huo kwenye mfumo wa wiring ya nyumba yako utaupeleka kwenye main switch kupitia kwenye kifaa kinaitwa Change over switch hiki kinachukua input ya TANESCO na ile kwenye inverter yetu lakini inatoa output ya mojawapo kati ya hizo source mbili, yaani kama TANESCO imekata utainonyeza let say unaipeka juu ndio upande wa inverter na ukiipeleka chini ina disconnect inverter na kuunga TANESCO and vice versa.

Faida ya huu mfumo hauhitaji wiring ya kujitegemea, haihitaji chanzo kukaa karibu na vitumiaji (kwa hyo unaweza hata kuitengea sehem yke nje huko au stoo) haitaathiri mwonekano wa chumba chako kama sebule hivi.

pia upotevu wa umeme si mkubwa kama ule wa mwanzo kwasabab hapa umeme utasafiri katika voltage kubwa (230V) badala ya (12V) zile za mwanzo kwa hivyo current ztakua kidogo tuu.

Napendekeza zaidi huu mfumo wa pili.

Ahsante!
Ahsante mkuu
 
Kwa matumizi yako unahitaji 15M kwa umeme wa uhakika boss

Kitakachobakia hapo ni kubadili battery wastani kila baada ya Miaka mitatu au minne ktokana na brand ulkonunua hzo battery mkuu
 
Kiongozi, tunaomba estimation ya umeme wa jua kwa majumbani tu, mfano nyumba inayotumja umeme wa 150,000Tsh kwa mwezi, 414.5 unit. Nahitaji investment ya kiasi gani ili nitumie umeme wa solar na Tanesco iwe ndio umeme mbadala ?
Weeeee duh matumizi ya mwezi unatumia 150000,nyumba yako ni eneo la biashara au umefunga taa za barabarani ,mimi nina taa nyingi kila kona ila nimetumia umeme kwa mwezi ni elfu 70
 
Weeeee duh matumizi ya mwezi unatumia 150000,nyumba yako ni eneo la biashara au umefunga taa za barabarani ,mimi nina taa nyingi kila kona ila nimetumia umeme kwa mwezi ni elfu 70
ACs ndio mchawi, vioo hivi vinapunguza sana hewa since inakuwa ni kama nusu dirisha, AC zikiwashwa sehemu kama 3 hivi au nne ndio bills zinaruka ovyo ovyo.
 
ACs ndio mchawi, vioo hivi vinapunguza sana hewa since inakuwa ni kama nusu dirisha, AC zikiwashwa sehemu kama 3 hivi au nne ndio bills zinaruka ovyo ovyo.

Yeah ni kweli kama ni AC hujakosea, au funga feni
 
Solar iko poa kama kwako una matumizi ya kawaida(Hakuna Ac , Freezer,jiko la umeme wala fridge)...
 
Weeeee duh matumizi ya mwezi unatumia 150000,nyumba yako ni eneo la biashara au umefunga taa za barabarani ,mimi nina taa nyingi kila kona ila nimetumia umeme kwa mwezi ni elfu 70
Wazee mna viwanda?

Umeme wa 70k?
 
Wazee mna viwanda?

Umeme wa 70k?
Unit 7.5 ni nyingi of course nalifanyia kazi sio kama pia na likubali maana kila baada ya siku nne lazima niweke umeme ww elfu 10 nilishaomba wanibadilishie tariff wakasema kama matumizi yako yapo hivyo itakulazimu mwezi kabla haujaisha uniti nitakazo nunua za tariff nafuu basi itanilazimu nibaki bila umeme mpaka mwezi uishe duh nikaona hii nipata potea

Hivi ni vitu gani vya kuangalia kujua nyumba yako inavujisha umeme
 
Naomba uniambie uhalisia wa kitu hiki... Free flywheel energy, hii ikoje? Kuna uhalisia kwenye hili?
hata mm nafuatilia kuhusu hilo nikakutana na huyu jamaa katika link hiyo kuhusu hizo free energy... nishampa kazi anifanyie... nasbr mrejesho sasa
 
hata mm nafuatilia kuhusu hilo nikakutana na huyu jamaa katika link hiyo kuhusu hizo free energy... nishampa kazi anifanyie... nasbr mrejesho sasa
Mm nikiwa Chuo hii Project nilifanya na kufanikiwa Vzr ila n kitu Ambacho kinahitaj Muda Mwingi Sana
 
Mm nikiwa Chuo hii Project nilifanya na kufanikiwa Vzr ila n kitu Ambacho kinahitaj Muda Mwingi Sana
Ebana eeh kwa hiyo generator ilipiga mzigo wenyewe bila ya kuweka external fuel?

Hongera kwa kuniongezea imani
 
Back
Top Bottom