Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,297
Unaweza kufa na nyumba ukaacha hapo, otherwise jenga bila haraka, kwa awamu na taratibu uta enjoy

Ukifikia level vitu vya kingereza uwiiiiii ni stress juu ya stress hasa kama unafosi nyumba kuisha na budget yako ni ndogo

Hongereni watu mnaomiliki mabangalooooo

Hongereni mnaomiliki ghorofa
 
Kama umejipanga wala usiogope Mkuu
Ila usijenge kwa pupa utapata headache
Mi sina stress coz sijachoka kupanga halafu sina familia yaani msela tupu ningeanza hata mwaka huu sema nabagua viwanja nataka cha kigamboni karibu na niwe na access ya kufika post mpaka kariakoo ... Vya mbali sana sitaki
 
Mbaka bati eeh? Upo mkoa gani? Budget yako ni pesa ngap mkuu!?

Mwenzio bado nahenya hapa chini
Niko Dar mzee nataka ya vyumba vinne haijalishi bajeti gani ila napiga mpaka bati then narelax coz nyumba nilipopanga pazuri na nalipa ndefu miezi sita.

Safi yaani sina wasi najenga coz ninatarajia mwakani mwisho nioe mpaka nikioa niwe nishafika kweny bati halafu naishi na mke nyumba ya kupanga mwaka au mwaka na nusu nahamia kwangu..it's my plan
 
Mimi pia nilikua natishwa hivyo hivyo ila kujenga ni rahisi sana mzee

Mbinu unayotakiwa kutumia kwanza usijenge kama adhabu alaafu pili punguza matumizi yasiyo ya lazima na uanze ku save, ukisha save tenga kiasi Cha akiba alafu Anza ujenzi hakikisha ujenzi wako usiguse kabisa pesa ya akiba uliyo nayo.

Kama uliamua akiba yako iwe laki 3 fanya ufanyavyo tafuta hela tupia kwenye ujenzi ila huo ujenzi usiguse hiyo akiba yako, tafuta fundi akupigie hesabu ya vifaa na gharama za ufundi mtoe chake afanye kazi ila akiba yako ibaki palepale.

Epuka kujenga kwa kutumia hela zote Hadi kumaliza akiba yako yote utateseka zaidi na ujenzi hautakiwi uwe ni mateso.

Mbinu hizi za ujenzi tunatumia sisi wagangaa njaa na ukiweza kutumia hiyo mbinu utajenga Kama tajiri kumbe huna utajiri wowote na jengo litaisha bila maumivu
 
Mbaka bati eeh? Upo mkoa gani? Budget yako ni pesa ngap mkuu!?

Mwenzio bado nahenya hapa chini
Umeona ehhh
Mimi nilijenga kakibanda kangu nikamaliza kabisa nikaweka mpangaji kabisa
Sasa hivi nakula kodi

Nikanogewa bwana nikaanza apartment nyingine ili niipangishe tena, hela niliyokuwa nayo nilijuwa nitagonga bati, lahaula nimeishia kwenye lenta hela yote ikaisha nimebaki mtupu mpaka najilaumu bora ningeacha tu, nimezika hela alafu saivi nateseka
 
Mbaka bati eeh? Upo mkoa gani? Budget yako ni pesa ngap mkuu!?

Mwenzio bado nahenya hapa chini
Umeona ehhh
Mimi nilijenga kakibanda kangu nikamaliza kabisa nikaweka mpangaji kabisa
Sasa hivi nakula kodi

Nikanogewa bwana nikaanza apartment nyingine ili niipangishe tena, hela niliyokuwa nayo nilijuwa nitagonga bati, lahaula nimeishia kwenye lenta hela yote ikaisha nimebaki mtupu mpaka najilaumu bora ningeacha tu, nimezika hela alafu saivi nateseka
 
👍😃😄
Vitu vya kiingereza... Blandering, skimming, plaster etc😄
Ujenzi si lelemama.

Sometimes i wish watu wa Nhc, wangekuwa wanajenga kwenye makazi ya kawaida ya watu kulingana na ramani ya mtu husika, then tunawalipa robo tatu au nusu. Robo ya gharama au nusu nyingine unalipa polepole.

Kuna watu kweli wanapata kiharusi (stroke) kwasababu ya ujenzi wanadhani ni kurogwa kumbe stress za ujenzi.

Na ukimpata fundi mwenye mawenge ndio balaa hatari. Anakutajia vifaa vingi ambavyo havitumiki vyote au anachanganya cement ratio isiyo sahihi., na ile inayomwagika chini haangaiki kuizoa.

Misumari ikidondoka kama hakuna wa kuokota imekula kwako. Bati au mbao zinakatwa vipande vipande bila mpangilio anajua una hela.
 
Mimi pia nilikua natishwa hivyo hivyo ila kujenga ni rahisi sana mzee
Mbinu unayotakiwa kutumia kwanza usijenge kama adhabu alaafu pili punguza matumizi yasiyo ya lazima na uanze ku save...
Mwenzio mimi nimetupia hela yote kwenye ujenzi, alafu sijafikia malengo ya kugonga bati basi ni stress juu ya stress
 
Hivi viwanja huko kigamboni au pembeni ya mji bei zipoje jamani?
Inategemea kule mbali Bei rahisi ila karibu huku Bei ndefu kingine ukinunua kwa muhusika sio pesa ndefu unaweza kupata kwa 35k per square meter uko mbali hata 20k kwa square
 
[emoji106][emoji2][emoji1]
Vitu vya kiingereza... Blandering, skimming, plaster etc[emoji1]
Ujenzi si lelemama.

Sometimes i wish watu wa Nhc, wangekuwa wanajenga kwenye makazi ya kawaida ya watu kulingana na ramani ya mtu husika, then tunawalipa robo tatu, au nusu na robi au nusu nyingine unalupa polepole.

Kuna watu kweli wanapata kiharusi kwasababu ya ujenzi wanadhani ni kurogwa kumbe stress za ujenzi.
Na ukimpata fundi mwenye wawenge ndio balaa hatari. Anakutajia vifaa vingi ambavyo havitumiki vyote au anachanganya cement ratio usiyo sahihi na ile inayomwagika chini haangaiki kuizoa.

Misumari ikidindika kama hakuna wa kuokota imekula kwako. Bati au mbao zinakatwa vipande vipande bila mpangilio anajua una hela.
Acha kabisa madam mafundi ndo wanaongeza stress zaidi, fundi anaweza kukukatia bonge ya dirisha ili amalize kazi yake haraka
Siku unakuja kuweka aluminium utaipenda
 
Mwenzio mimi nimetupia hela yote kwenye ujenzi, alafu sijafikia malengo ya kugonga bati basi ni stress juu ya stress
Hutakiwi kujenga hadi umalize pesa ya akiba yote, tenga akiba yako kwaajili ya dharura yoyote utakayo tokea alafu hela utakazo pata nje ya akiba yako ndo utupie yote kwenye ujenzi ukiona tu ujenzi unataka kugusa kiasi cha akiba ulicho panga kuwa nacho sitisha kwanza ujenzi, maana dharura zingine huwa zinakuja bila taarifa Kama utamaliza akiba Basi utajikuta umeingia kwenye madeni makubwa na hata hiyo nyumba inaweza kukushinda kabisa

Unaweza ukawa huna pesa nyingi ila ukijiwekea utaratibu wa ujenzi usiguse hela yako ya akiba niamin aise utajenga kwa raha sana usione aibu kusitisha ujenzi hata kwa miez 6 ikiwezekana jisahaulishe kabisa ili tu usiguse akiba, ukiweza hizo mbinu utajenga kama tajiri na bila maumivu na muda mzuri wa kujenga ni wakat ukiwa huna familia kubwa, unaweza kuanza kujenga taratibu kabla hata hujaoa
 
Back
Top Bottom