Kama hujui faida za raia wengi kuwa nchi za nje, angalia remittances EAC

Nailinganisha Tanzania na Rwanda:

Kwa mujibu wa takwimu z mwaka 2021, Rwanda yenye ukubwa wa kilomita za mraba 26,338, ilikuwa na watu 13,460,000. Kwa mwaka huo, raia wake walio ughaibuni walituma nyumbani jumla ya dola za Kimarekani 246,000,000

Kwa kuilinganisha na Tanzania yenye ukubwa wa kilomita za mraba 945,087 na makadirio ya watu 63,000,000 kwa mwaka huo wa 2021, raia wake walioweza kutumia jumla ya dola za Kimarekani 569,500,000

Ifahamike kuwa Tanzania ni kubwa kwa Rwanda mara 35.9, na kwa idadi ya watu, Tanzania inaizidi Rwanda mara 4.7

Pamoja na hayo, kwa mwaka 2021, Tanzania ilipata mara 2.3 pekee ya hela ambayo Rwanda ilipokea kutoka kwa diaspora wake.

Mwingine anaweza akafikiri tuliizidi Rwanda, lakini ukilinganisha na idadi ya watu wa Tanzania na Rwanda, utagundua ni Rwanda ndiyo iliizidi Tanzania.

Kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya watu wa nchi hizi mbili, Tanzania ilipaswa ipate alau dola bilioni 1.16 kwa mwaka huo.
 
Kwa muktadha wa takwimu iliyotokewa hapo juu, ni wazi kuwa kwa mwaka 2021, nchi zote 3: Rwanda, Uganda na Kenya zilipokea hela nyingi zaidi kuizidi Tanzania kutoka kwa raia wake walio nje.

Mpaka Rwanda ilituzidi! Nini siri ya hayo Mataifa? Ni halali nchi ndogo kama Rwanda kuizidi Tanzania?

Hiyo inaleta picha gani? Nchi ya Rwanda ina watu makini zaidi kuizidi Tanzania?

Au ni kwa sababu Rwanda imeridhia uraia pacha kwa raia wake?
 
Nchi pekee tuliyoipita ni Burundi. Yenyewe kwa mwaka huo wa 2021, ilipokea dola 45,600,000

Idadi ya watu Burundi mwaka 2021 ilikadiriwa kuwa 12,551,213.

Burundi ina ukubwa wa kilomita za mraba 27,830.
 
Siyo kweli mkuu! Namba hazidanganyi:

1. Kwa mwaka 2021, Botswana ilikuwa na watu 2,588,423. Ilipokea remittance ya dola million 60.584.

Ukiiweka katika uwiano na ya Tanzania kwa mwaka huo, itakuwa imeiacha Tanzania mbali sana. Kwa uwiano sahihi, Tanzania ilipaswa kupokea alau dola 1.5 badala ya dola 569.5 iliyopata mwaka huo.

Nini maana yake? Kwa uwiano, Botswana ina raia wengi zaidi ughaibuni kuizidi Tanzania.

2. Suala la ushoga ni la kitabia, na mtu mwenye hiyo tabia anaweza kufanya huo uchafu hata akiwa kijijini kwao Namtumbo.

Au unataka Tanzania iwarudishe nyumbani raia wake waliopo kwenye balozi za Tanzania ughaibuni kwa kuhofia ushoga?

Unataka Watanzania wasiende masomoni ng'ambo kisa ushoga?

Kwa kawaida, kusafiri kwenda nchi za nje ni dalili mojawapo ya mafanikio. Maskini hasafiri. Ndiyo maana kiuwiano, Wabotswana walio ughaibuni ni wengi zaidi kuwazidi Watanzania.
 
๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Ebwana nje wamejaa wabongo kibao (diaspora) wengine hata Bongo hawapajui wamezaliwa kule kule Ila ni wabongo
Ni kweli mkuu wapo, lakini hawafikii idadi ya Wakenya, Waganda, na hata Wanyarwanda(kiuwiano).
 
Akina dada na wamama wa kikenya wengi huwa busy kutafuta short cut ya maisha kwa kuolewa na wazungu huko nje,...........! Na wazungu wanajulikana kwa shughuli yao ya kula, small.
Hapo umewasifia au umewaponda?
 
Uko sahihi diaspora inawaingizia pesa nyingi sana za kigeni kuliko sekta nyingi tu. Ni wakati wa kubadili mtizamo na mfumo hapa kwetu ukizingatia ajira hamna, ni vyema kuwaanda vijana wakaenda kufanya kazi nje ili wawekeze nyumbani.
1. Kingereza kianze kutumika primary
2. Kuwekwe mikakati mahsusi ya kupeleke vijana nje kufanya kazi mbali mbali.
3. Kuwe na wizara inayoshughulika na diaspora.
4. Hadhi maalum ya wenye asili ya tanzania irasimishwe ili haki zao zilindwe.
 
Point๐Ÿ™
 
Kutokujua kingereza vizuri kunatufanya tuwe magoigoi [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Namba hazidanganyi mkuu! Una takwimu?

Ujue kama Watanzania wanafanya hivyo, kuna uwezekano wa Wakenya na Waganda nao kufanya hivyo pia.
 
Point๐Ÿ™
 
Dual citizen ina faida kwa nchi kubwa zenye uchumi imara kwa nchi masikini ni janga kubwa
Kivipi mkuu? Unataka uniambie nchi zote za Afrika Mashariki hazijaliona hilo?

Unajua katika jumuiaya ya Afrika Mashariki, ni Tanzania pekee ndiyo haijakubali uaraia pacha?

Unataka kutuaminisha kuwa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan na Congo DRC ni kubwa kuizidi Tanzania?

Unajua nchi zote hizo zimesharuhusu dual citizenship?
 
Tanzania hii ukitumiwa Hela kutoka nje bank wanaogopa kulipa Hadi utoe maelezo Hela imetoka wapi na ni yanini.??? Kazi tunayo
Nafikiri hilo lipo Tanganyika pekee. Sidhani kama unaweza kukutana na "ushamba" kama huo kule Zanzibar!
 
Point
๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ